Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,885
Mwaka 2015 nchi zote za EAC zilikubaliana kuwa ifikapo mwaka 2019 nchi zote zipige marufuku uagizaji wa nguo na viatu vya mtumba kutoka nje. Sababu walisema kuwa ni fedheha watu kuvaa mitumba na ili kukuza viwanda vya ndani vya kuzalisha nguo. Na watu walipredict kuwa baada ya 10 EA itakuwa inaexport nguo za kama $3bln kwa mwaka.
Sasa, muuzaji mkubwa wa mitumba duniani ni Marekani, akifuatiwa na Uingereza na nchi zingine. Inasemwa kuwa sekta ya mitumba Marekani inaajiri karibia watu elfu arobaini.
Tarehe ya kupiga ban mitumba ilipokaribia Marekani chini ya Trump wakasema nchi itakayopiga ban mitumba itaiondoa kwenye mpango wa AGOA, (mpango wa nchi maskini za Africa kuuza vitu kwa ushuru mdogo Marekani). Viongozi wakakaa kuona wanafanyaje, viongozi wengine wakafyata mkia. Kagame akawahimiza sana kuwa hilo ni swala muhimu kufanya hata kama litawaumiza kwa muda lakini wakagoma.
Inasemekana kuwa Kagame akapiga ban peke yake. Hilo lilisababisha kelele nyingi sana kati yake na Marekani. Sijajua kwa sasa status ya jambo lile iko vipi.