Kagame: Nagombea urais kwa mara ya mwisho.

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
25,685
2,000
KIGALI, Rwanda

RAIS Paul Kagame amewaambia wafuasi wake wa Chama cha Rwandan Patriotic Front (RPF) kuwa atagombea urais kwa mara ya mwisho.

Kagame alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akitoa hotuba yake ya shukrani baada ya kuchaguliwa kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 3, 2017.

Katika mkutano mkuu alichaguliwa kwa kura 1,929 kati ya kura 1,930 zilizopigwa. Kura moja iliharibika.
Katika hotuba yake Kagame alisema,”Natoa wito kwamba ama tofauti au vizuri zaidi au tufanye kazi kwa bidii sana ili katika kipindi cha miaka saba kiwe kama cha mpito.

Aliwahimiza vijana kujiunga na siasa lakini aliwataka wachukue tahadhari.
“Jihadharini huku.
Si suala la kuwa rais tu. Si suala la kuwa na haki ya kuwa rais. Rwanda inataka na kwa dhati inahitaji rais sahihi,” aliongeza.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wageni kutoka nchi za China, Ethiopia, Afrika Kusini na Uganda.
 
Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
5,996
2,000
I like Kagame. Since he is doing good, let him be.

Si Kila linaloapply Ulaya, linaapplication Africa.

Si Kila linaloapply Tz linaapplication Rwanda....
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
23,570
2,000
KIGALI, Rwanda

RAIS Paul Kagame amewaambia wafuasi wake wa Chama cha Rwandan Patriotic Front (RPF) kuwa atagombea urais kwa mara ya mwisho.

Kagame alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akitoa hotuba yake ya shukrani baada ya kuchaguliwa kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 3, 2017.

Katika mkutano mkuu alichaguliwa kwa kura 1,929 kati ya kura 1,930 zilizopigwa. Kura moja iliharibika.
Katika hotuba yake Kagame alisema,”Natoa wito kwamba ama tofauti au vizuri zaidi au tufanye kazi kwa bidii sana ili katika kipindi cha miaka saba kiwe kama cha mpito.

Aliwahimiza vijana kujiunga na siasa lakini aliwataka wachukue tahadhari.
“Jihadharini huku.
Si suala la kuwa rais tu. Si suala la kuwa na haki ya kuwa rais. Rwanda inataka na kwa dhati inahitaji rais sahihi,” aliongeza.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wageni kutoka nchi za China, Ethiopia, Afrika Kusini na Uganda.
NEVER ON EARTH, INAWEZEKANA, KAMA KUNA MTOTO WAKE AMEMUANDAA, HIVIHIVI HATOKI DICTATOR OF THE HIGHEST DEGREE
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom