Kagame: Nagombea urais kwa mara ya mwisho.

Kagame: Nagombea urais kwa mara ya mwisho.

Kwanini wasiwe na katiba kama ya Urusi, rais na waziri mkuu wanabadilishana viti mpaka mwisho wa maisha yao, Kagame muhula ukiisha wananchi kwa mara nyingine watakusanya saini zao wakimtaka aendelee na yeye kama kawaida yake kwa shingo upande atakubali tena. Democracy African style.
 
That was not a voting, it was rubber stamping... Ila ni bora Kagame aendelee mana nilichojifunza kwa hawa watu, ni wagumu sana kuongozwa na pia' sio watu wanaopenda amani'. So inabidi wapate mtu anayeweza ku command peace kama Kagame...
 
Well said, naona yanayo endelea kwa M7 yatakuja kuwa replicated kwa PK - wote wamejitahidi kuendeleza nchi zao lakini wasijiharibie kwa kutaka kuwarithisha vyeo watoto wao - Ufalme ufanyike Uraiani siyo Serikalini.
Kwani Mwanae anamuelekeo huo!!
 
Ivan cymoro kagame ana miaka 27 sasa maana yake miaka 7 ijayo atakuwa 34 atakuwa gentomani kuongoza nchi hehehe

Kagame mjanja
 
Kwa wale wenzetu wanaokaa marekani na kujua sera za kiuchumi ndani ya marekani ,haina tofauti sana na hawa ndugu jirani zetu. Marekani kuna zile familia za Rockfeller na wengine wanajulikana kuweka misingi ya kunyonya raia wengine wote kupitia mfumo wa credit cards, bidhaa kuwa expensive ndani ya marekani eti wanataka kufanya life standard yao iwe juu ,mfano kitu kimetengenezwa marekani ila kikiuzwa ndani ya US kibakua expensive kikiuzwa nje kinakua cheap. Hizo excess of money charged wanajua zinaenda kuliwa na familia gani huko marekani. Kwa majirani zetu (Rwanda) huo mfumo upo ,ila watu hawajui,kwa mfano bei ya pikipiki boxer kule kwao ni around 2.7millions Rwf,hiyo ni sawa na 8 millions Tshs, Unga wa ngano wa kawaida kg moja ni 3000 Rwf hiyo ni sawa na 9000 Tshs. Hizo ni bidhaa ambazo mtu mmoja alikuja akaziona hapa akashangaa bei ilivyo ya chini kupita kiasi. Nadhani kuna zaidi ya over-priced products nyingi. Je hizo excess zinaenda wapi,mifukoni mwa watawala au kulipa wenzetu walitukabidhi nchi kama wale wenzetu aki Tony Blair wanajifanya ni washauri. Ila mwache jamaa amalizie maigizo yake ya uchaguzi,ila nadhani ndugu zake anawakaba na kamba shingoni kimya kimya. Namtakia utawala mzuri
 
KIGALI, Rwanda

RAIS Paul Kagame amewaambia wafuasi wake wa Chama cha Rwandan Patriotic Front (RPF) kuwa atagombea urais kwa mara ya mwisho.

Kagame alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akitoa hotuba yake ya shukrani baada ya kuchaguliwa kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 3, 2017.

Katika mkutano mkuu alichaguliwa kwa kura 1,929 kati ya kura 1,930 zilizopigwa. Kura moja iliharibika.
Katika hotuba yake Kagame alisema,”Natoa wito kwamba ama tofauti au vizuri zaidi au tufanye kazi kwa bidii sana ili katika kipindi cha miaka saba kiwe kama cha mpito.

Aliwahimiza vijana kujiunga na siasa lakini aliwataka wachukue tahadhari.
“Jihadharini huku.
Si suala la kuwa rais tu. Si suala la kuwa na haki ya kuwa rais. Rwanda inataka na kwa dhati inahitaji rais sahihi,” aliongeza.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wageni kutoka nchi za China, Ethiopia, Afrika Kusini na Uganda.

Umemsahau mgeni mmoja ambaye ni Tanzania. Kagame hawezi kufanya jambo lolote jema nchini Rwanda halafu asiwaalike Watanzania tena hasa kipindi hiki ambacho aliye madarakani ( Rais Dkt. Magufuli ) anakubalika, kupendwa na kuheshimiwa mno na Rais Paul Kagame na hata Wanyarwanda wote kwa ujumla wao.
 
Hapa sijakusoma Ndugu
 
Kama kuna mtu anasubiri kumuona Kagame anaondoka eti baada ya miaka 7 ijayo anajidanganya big time,He is there to STAY,ndivyo nionavyo mimi.
 
Kama kuna mtu anasubiri kumuona Kagame anaondoka eti baada ya miaka 7 ijayo anajidanganya big time,He is there to STAY,ndivyo nionavyo mimi.
Kwahiyo alicho kisema sicho?
 
Back
Top Bottom