Mh, nataka kuripoti bila ushabiki ila sitaweza bandugu. Naomba tu mwingine ajaribu.
Tibaijuka anaongea kwa kigugumizi cha mtu muongo sana. Halafu ni dhahir kuwa huyu mama hajazoea uongo!
Ka Kafulila sijui kanajiamini nini maana kana confidence hapo pembeni na kanamwangalia mama huku kakijua kabisa anadanganya.
Mama anasema, Rugemalira ana haki ya kuuza hisa zake, na alipewa yeye 1.6 kwa ajili ya shule. Ruge account iko Mkombozi, na account ya shule haiko mkombozi, hakutaka kusumbuka kuhamisha hela hivyo akaamua kupitisha kwa mama Tiba kama mmoja wa viongozi wa shule.
Kafulila anasema, Prof anavosema aliahidiwa kupewa hela bila kujua kiasi inatia shaka maana 1.6 billion ni hela nyingi sio tu TZ lakini dunia nzima. Kupewa tu dolla mill 1 bila taarifa inatia shaka.