Kafulila akwaa kisiki tena Mahakamani

Kafulila akwaa kisiki tena Mahakamani

Nadhani ile nguvu ua 4billioni kama siyo 2b ikiyotolewa bila kupitishwa na bunge sasa inaonekana matumizi yake ktk kutoa maamuzi mahakamani.
 
Mahakama ya rufaa leo hii imetupilia mbali rufaa ya aliyekuwa mbunge wa kigoma kusini, ndugu Kafulila kwa kukosa nguvu ya kisheria.

Kafulila alimkatia rufaa mbunge wa Kigoma kusini Ndugu Husna Mwilima kwa kudai kuwa aliporwa ushindi.

Mahakama imemtaka ndugu Kafulila kulipa gharama zote za kesi hiyo.

Chanzo: Azam news
Huyu jamaa mpaka aseme poo!
Vinginevyo asubiri 2020
 
Mahakama ya rufaa leo hii imetupilia mbali rufaa ya aliyekuwa mbunge wa kigoma kusini, ndugu Kafulila kwa kukosa nguvu ya kisheria.

Kafulila alimkatia rufaa mbunge wa Kigoma kusini Ndugu Husna Mwilima kwa kudai kuwa aliporwa ushindi.

Mahakama imemtaka ndugu Kafulila kulipa gharama zote za kesi hiyo.

Chanzo: Azam news
Huyu mzee wa mawese njaa itamuua.kwani lazima awe mbunge?
 
Tumbili bhana,miti yote imeteleza.

Aufanyie kazi ushauri aliowahi kuwapa watu wa Kigoma,aanzishe chama cha mawese!!
 
Wewe kafulila ni msukuma unatafuta nini kigoma kwa waha
Kumbe wabunge huwa wanawakilisha makabila badala ya wakazi wa jimbo husika! Mkimaliza huu ubaguzi wenu wa waziwazi, mnarudi na uongo wenu wa kuwashutumu wasiohusika kuwa ni wakabila....!?!
 
Team Bombadia bana, mmewehuka kabisa kama misukule iliyofunguliwa mlango itoke nje kupunga upepo. Kifupi lesi bado ipo jikoni, chumvi tu ilikosekana ili ladha ipatikane.
 
Ukiona kimya hivyo ujue kaliwa mwanahabari huruuu (siyo huru)!!!!!!!
Usishangae hata Msoma Bulaya naye Leo kashindwa kutoa ushahidi kabanwa na vifungu toka kwa Mtalemwa...that's why no updates leo.....kama msemo unaotumika"kinachojili kesi ya Bulaya Mahakamani chini ya Wakili MSOMI"(MWENYE MASTERS LKN MSOMI KULIKO PROFESSOR AU DR'S)
Tanzania hiiii hadi raha yani

Natamani sana kumfahamu Advocate Mtalemwa
 
Ajipange tena kwa ajili ya uchaguzi wa 2020.

Nadhani akigombea kupitia ACT wazalendo atashinda.
Machali aliyegombea kupitia ACT alishinda? ACT ndio sumu katika kesi hii kisa tu mtu alikataa kuwa mgombea wenu? Hiyo kesi haijaisha mkuu, nitawashauri Mawakili husika kuomba Review ili HAKI ITENDEKE NA IONEKANE KUTENDEKA! ACT kaeni na fitna zenu!
 
Hakuna vifungu vya sheria vinavyosindikiza madai yake pasi na shaka.
Hii ni kesi ya madai hivyo haihitaji kifungu cha sheria kitakacho sindikiza madai yake pasi na shaka bali ni on the balance of probabilities...
 
Back
Top Bottom