Kaduma amrushia kombora JK, CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Saturday, 21 May 2011 21:43
kaduma.jpg


Balozi Ibrahim Kaduma aliyekuwa Waziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere akizungumza katika mahojiano maalumu na Gazeti hili jijini Dar es Salaam jana.Picha na Fidelis Felix

Elias Msuya

BALOZI Ibrahim Kaduma, ambaye alikuwa Waziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, ametilia shaka utekelezaji wa mkakati kujivua gamba kwa madai kuwa CCM na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete hawako makini kwa sababu wanashindwa kuwachukulia hatua wanaotuhumiwa kukivuruga chama.Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu jijini Dar es Salaam jana, Kaduma ambaye ameitumikia serikali kwa muda mrefu, alisema mkakati wa CCM kujivua gamba utafanikiwa endapo Kikwete na chama chake watakuwa na dhamira ya kweli.

"Kujivua gamba kwa CCM kutawezekana kama wakiwa ‘serious' (makini). Kwa sababu, wakati wetu hakuna mtu aliyeshutumiwa akabaki kwenye Kamati Kuu ya chama," alisema Kaduma na kuongeza:"Kama rais ana msimamo huo awatoe kwenye chama wanaotuhumiwa. Kwa nini awaseme tu au anataka wajiondoe wenyewe? Anasema mawaziri wana harufu ya wizi lakini wamo kwenye baraza, kwa nini asiwatoe?"

Huku akitaja sifa za kiongozi bora, Kaduma alisisitiza kuwa kutokana na kukosekana maadili kwa sasa, taifa limepoteza mwelekeo.

"Mpaka sasa hatuko kwenye ‘right truck' (njia sahihi) kwa sababu tumeshapoteza maadili. Baadhi ya sifa za kiongozi bora ni kuwa mcha Mungu na kupambana na rushwa kama alivyokuwa Sokoine.
"Viongozi wawe na huruma ya kweli, wanyenyekevu na wawe tayari kujikosoa na kukosolewa. Je, viongozi wa sasa wana sifa hizo?" alihoji na kusisitiza: "Sioni hali hii kwa utawala wa sasa".

Akizungumzia kuanguka kwa Azimio la Arusha na kuingia kwa Azimio la Zanzibar,Balozi Kaduma alisema hali hiyo ilisababishwa na ubinafsi wa viongozi wenye tamaa ya mali."Ufisadi ni zao la ubinafsi, walioshindwa Azimio la Arusha walikuwa wabinafsi. Mtu kama huwezi kufanya kazi uondoke serikalini, kwani hatukulipi mshahara hata ukashindwa kututumikia (wananchi)?"alihoji.

Akikumbuka uongozi wa Mwalimu Nyerere, Kaduma alisema, rais huyo wa kwanza wa Tanzania, alifanya viongozi waaminike katika jamii kwa sabahu alikuwa mkali."Mwalimu alikuwa ‘strict' (mkali). Aliwahi kutoa mfano wa mke wa Cesar (Kaisari) ambaye alipewa talaka kwa kutuhumiwa tu. Mke wa Kaisari hakupaswa hata kutuhumiwa," alieleza Kaduma na kuendelea:"Wakati ule ukifanya kosa unajiondoa mwenyewe, maana ukingoja (Nyerere) atakufukuza tu.

Ndiyo maana enzi za Mwinyi wafungwa walipokufa Shinyanga, alijiuzulu. Jenerali Natepe pia alijiuzulu kwa matatizo yaliyotokea Gereza la Ukonga." Balozi Kaduma ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC 1997), alisema viongozi wa sasa wamejaa ubinafsi ndiyo maana ni mafisadi.

"Moja kati ya ahadi za mwanachama wa Tanu ni 'binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja' maneno tisa tu," alisema na kuendelea:"Biblia katika Zaburi 133 inasema ‘Tazama jinsi ilivyo vema ndugu wakikaa pamoja kwa umoja'. Kiongozi akishayajua haya hutakuwa mbinafsi."

Aliendelea, "Kiongozi ni mtumishi siyo mtawala, kila analofanya linufaishe jamii. Anapaswa kujitoa kwa ajili ya watu. Ufisadi ni zao la ubinafsi. Tuzitafakari ahadi 10 za mwana Tanu."Kuhusu kulegalega kwa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ameshauri kuwapo kwa serikali moja akisema kuwa hilo ndilo lilikuwa kosa la Mwalimu Nyerere.

Hata hivyo aliwatahadharisha wananchi wanaotaka muungano uvunjwe akisema kuwa watatafakari kwanza hasara zake kabla ya kuchukua maamuzi."Kosa kubwa la Mwalimu Nyerere lilikuwa ni kukataa kuunda serikali moja akiogopa kuimeza Zanzibar. Karume alikuwa tayari kabisa. Nadhani hiyo ingemaliza matatizo yote".

Alisema muungano unaharibiwa na tamaa za viongozi ambao nao hutaka kuwa na madaraka bila ya kujali maslahi ya wananchi.
Kaduma alipinga wazo la baadhi ya watu kutaka kuwe na serikali tatu akisema kuwa hili litaongeza mzigo wa gharama za uendeshaji.

"Ni gharama kubwa, leo kuna wilaya mpya zimeanzishwa, umeona kuna ma DC? Lengo la kuunganisha Tanu na ASP lilikuwa kuunda serikali moja, lakini utashangaa kusikia Wazanzibari wanang'ang'ania serikali yao, sikatai, lakini watafakari" alisema. Kwa mujibu wa Kaduma kama viongozi wa sasa wangemsikiliza Mwalimu Nyerere, nchi isingefikia hapa ilipo.

Alisema licha ya kwamba wakati Nyerere anastaafu mwaka 1985, nchi ilikuwa na hali mbaya kiuchumi, alifanikiwa kuijenga katika maadili."Kama Nyerere angesikilizwa, maadili yake ndiyo yangekuwa uhuru wa Afrika yote. Ili nchi ikue inahitaji mambo matatu; uhuru wa bendera, uhuru wa kichwa (mind), uhuru wa kiuchumi. Hili ndilo lengo la Azimio la Arusha.

"Nyerere alifanikiwa mambo mawili akabakiza suala la kukuza uchumi."Balozi Kaduma ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati wa Mwalimu Nyerere, alisikitishwa na Umoja wa Afrika kwa kushindwa kumkemea kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, kwa kuua raia wake.
 
well said ila kwa mkuu wa kaya yanaingia sikio la kulia na kutokea sikio la kushoto!
 
Bravo Ibrahim Kaduma... Leaders come in many forms, with many styles and diverse qualities. There are quiet leaders and leaders one can hear in the next country. Some find strength in eloquence, some in judgment, some in courage !!!
 
..hivi kuna mwanachama yeyote wa CCM ambaye mpaka leo hii haelewi kwamba Kikwete,Lowassa,na Rostam, ndiyo vinara wa ufisadi ndani ya chama chao?

..kwa mtizamo wangu utaratibu wa kujivua gamba hautakuwa na maana yoyote ile kama Kikwete,Lowassa,na Rostam, hawatavuliwa uanachama wa CCM kwa wakati mmoja.
 
Bravo Ibrahim Kaduma... Leaders come in many forms, with many styles and diverse qualities. There are quiet leaders and leaders one can hear in the next country. Some find strength in eloquence, some in judgment, some in courage !!!
nnguu007, naungana na wewe huyu Kaduma has guts!. Yeye ni miongoni mwa wana CCM wa ukweli ambao ni Nyerere type. Hivi karibuni anatarajia kutoa chapisho lake la kuilaani CCM kwa kupitisha Azimio la Zanzibar lililo zika Azimio la Arusha.
 
is this the same kaduma aliyeanzisha nico?naona kama picha sio ya kwake...
its obvilious kuwa jk amepoteza muelekeo,bt more disappointing ni hii sanaa ya kujivua gamba.angejikakamua akawachukulia hatua magamba angeweza kutoboa.nahofia hali inazidi kuwa tete.
 
Ushauri mzuri sana lakini nijuavyo mimi kwa walengwa utaingilia sikio la kulia na kutokea sikio la kushoto immediately na mambo yanakuwa business as usual.
 
Kwa mtazamo wangu, ukiona kila mtu anaongea na kutoa nasaha kwa raisi na serikali kwa ujumla basi ujue kuna jambo kubwa ambalo limefanya kila mtu kukata tamaa na raisi pamoja na serikali yake. Sijui kama nchi hii itarudi itarudi kwenye mstari sahihi tena, oooh Mungu tusaidie
 
nnguu007, naungana na wewe huyu Kaduma has guts!. Yeye ni miongoni mwa wana CCM wa ukweli ambao ni Nyerere type. Hivi karibuni anatarajia kutoa chapisho lake la kuilaani CCM kwa kupitisha Azimio la Zanzibar lililo zika Azimio la Arusha.


katika hili anapoteza wakati wake..

Azimio la Zanzibar lilipitishwa mwaka 1992/1993 kama sikosei na Mwalimu akiwa hai...alipiga kelele haikusaidia...ubinafsishaji ulianza na Mwinyi ukashamiri na Mkapa...Mwalimu alikuwepo na hakuweza kuzuia..hapa nitaje mfano wa benki ya NBC wakati mzee wa ANBEM alipoamua kuiuza kwa makaburu, Mwalimu aliwaka sana lakini chinga alitia pamba masikioni watu wakala wakatulia, iliuzwa kwa Tsh Bn 15 hivi; wakati huo Nic Anelka anatoka Arsenal kwenda Real Madrid Kwa Tsh Bn 23 hivi, Ulimwengu aliandika katika Rai, 'Anelka ghali kuliko NBC'.

Kimsingi CCM ni chama kilichopitwa na wakati na ilivyo kila zama zina mambo yake ni muhali kuiona CCM ikibadilika kwenda na matakwa na matarajio ya wananchi(matakwa ya zama hizi) maana si msingi wa kuasisiwa kwake, msingi wake ni chama kushika hatamu na wananchi kuwa chini ya twaa ya chama(wananchi kwenda na matakwa ya chama)..kwa hiyo hata hii kujivua gamba ni jaribio zuri ambalo haliwezi kufaulu kwa sababu ni kinyume na the very existence ya chama chenyewe.

Kaduma, Warioba, Salim, Butiku wanatawaliwa na ghera ya kupenda kuiona CCM ya baba yao Mwalimu ikiendelea kutawala, walau ni katika vitu vichache alivyoasisi Mwalimu ambavyo vingalipo duniani(vingi ni marehemu)...bahati mbaya sana kwao wakti umepita na kupigana nao ni kupoteza wakati.

Ni mtazamo tu...nawakilisha!!!!
 
sidhani kama uwajibikaji, uaminifu na uadilifu alivyosema huyu babu ni marehemu.....CCM ya sasa imeshindwa changamoto za vyama vingi hivyo inatumia kila mbinu nzuri na chafu ku-cling in power. Ufisadi ulitungiwa sheria ya takrima baada ya kuone sera zao za kijamaa hazina mashiko.....Mpeni nakala ya haya maneno Nnauye jr maana dogo kichwani ni mtupu na ni kasuku
 
Back
Top Bottom