Kadogosa: Tutarejesha safari za treni kati ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha ndani ya muda mfupi

Tanzania Railways Corp

Verified Member
Mar 23, 2018
138
500
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndg. Masanja Kungu Kadogosa ametembelea kipande cha reli kati ya stesheni za Buiko na Hedaru mkoani Kilimanjaro ambacho kimefunikwa na maji kwa zaidi ya juma moja baada ya mafuriko yaliyosabishwa na mto Pangani kujaa kutokana na mvua zinazonyesha katika maeneo ya mkoa wa Kilimanjaro na nchi jirani ya Kenya hivi karibuni Mei 2020.​
Mkurugenzi mkuu wa TRC aliambatana na timu ya Wahandisi na watumishi wa Shirika la Reli akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya reli na Ujenzi Mhandisi Faustin Kataraia​

Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Ndg. Focus Makoye Sahani, Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti wa ajali katika reli, Mhandisi Maizo Mgedzi na Mhandisi ujenzi kanda ya Tanga Bw. Shadrack Massawe.​

large-1590932217-_DSC1338.JPG
Kutokana na mafuriko hayo, kipande cha Reli chenye urefu wa KM 1.6 kimepelekea Shirika la Reli kusitisha kwa muda safari za treni za abiria na mizigo kati ya mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.​

“Tumekuwa na mafuriko haya kwa muda wa karibu siku ishirini sasa tangu tarehe 10 ya mwezi Mei, 2020 na ilipelekea kufunga huduma zetu kwa maana ya treni za abiria na mizigo, lakini mpaka hivi sasa kina cha maji kimeshuka sana kiasi kwamba tunaweza kufanya lolote, unaweza ukaona sehemu kama hazina mvua lakini maji haya ni mengi, yanatoka bwawa la Nyumba ya Mungu” alisema Ndg. Kadogosa.​

Licha ya kupungua kwa kiasi cha maji baadhi ya sehemu bado hakuna usalama kwa treni kupita. Mbali na miundombinu ya reli, mafuriko hayo yalisababisha maafa kwa zaidi ya familia 3000 wilayani Same, mkoani Kilimanjaro.​

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndg. Kadogosa ameongeza kuwa kuna uwezekano shughuli za umwagiliaji zinazoendelea karibu na eneo hilo zinasababisha kasi ya maji kutopungua.​

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshajji Bw. Focus Sahani amesema kuwa kutokana na mafuriko hayo kumekuwa na athari kubwa katika uendeshaji wa huduma za reli ambapo kwa sasa hakuna huduma ya treni ya abiria ambayo inafanya safari, sambamba na treni za mizigo ambapo hadi sasa jumla ya safari 22 zimesitishwa na hivyo kuathiri usafirishaji wa bidhaa za viwandani hasa Saruji kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Tanga kuelekea Arusha.​

Halikadhalika Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti ajali katika reli, Mhandisi Maizo Mgedzi ameeleza, katika kipande hicho chenye urefu wa km 1.6 ni Mita 400 tu ndizo zinazoweza kupitika kwa sasa na ili kufanya ukarabati ni lazima kiasi cha maji kishuke chini.​

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu na Ujenzi Mhandisi Faustin Kataraia amesema kuwa Kutokana na tathmini iliyofanywa na wataalam kutoka TRC, ili kurejesha njia hiyo katika hali ya usalama na hatimaye safari za treni kuelekea Moshi na Arusha kuanza tena kutahitajika matengenezo ya njia ya mchepuko kwa kuwa kusubiri maji yapungue kunaweza kuchelewesha zaidi kurejea kwa safari za treni katika njia hiyo.​

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la reli Tanzania amesema kuwa njia hiyo ya mchepuko itakayokuwa na urefu wa KM 2 itasaidia kurejesha huduma ya usafiri wa Treni kwa haraka lakini pia itatoa mwanya kwa kipande hicho kilichofunikwa na maji kufanyiwa marekebisho na kuboreshwa zaidi na amewaahidi wananchi wa mikoa ya Kaskazini kuwa huduma ya usafiri wa treni itarejea baada ya muda mfupi.​

“Treni hii ilikuwa imeshapotea kwa muda mrefu sana, sasa wanapoona tatizo kama hili wanaweza wakafikiri kwamba yameanza tena, nataka niwaahidi wananchi wa Kilimanjaro, Arusha na maeneo jirani kuwa treni yao tutairudisha baada ya muda mfupi na tutaendelea na uendeshaji kama kawaida, na kama dhamira ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, inavyosema kwamba treni ya Kaskazini lazima iendelee kufanya kazi, na sisi watendaji jukumu letu ni kutekeleza maagizo”​

Reli ya Tanga hadi Moshi ilifunguliwa mwezi Julai mwaka 2019 na kuzinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambapo imerahisisha usafiri na kuchochea maendeleo ya Taifa kupitia treni za mizigo zinazorahisisha usafirishaji bidhaa kadha wa kadha zikiwemo za viwandani kwa gharama nafuu.​
 

mjenziwakale

JF-Expert Member
Sep 24, 2015
540
1,000
Yaani wabongo kwa urasimu ....naona kila mkurugenzi aliyetajwa hapo anakaimu........na hii ni katika taasisi nyingi, shenzi sana
 

jacana

Senior Member
May 24, 2020
186
250
Aise!? hakika mungu yupo pamoja nami,leo nilikuwa najianda kuliwa hela yangu,lakin sasa kila kitu nishajua asante sana kwa kuleta huu uzi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom