Kadi za CHADEMA zagombewa kama njugu Mtwara.

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katika hali inayoonyesha kampeni ya M4C mikoa ya kusini imevunja rekodi wananchi mbalimbali hususan vijana wamekuwa wakigombea kadi za CDM na wengine kuzisaka sehemu mbalimbali mjini Mtwara.

Hali hiyo imeanza kujidhihirisha tangu juzi siku moja baada ya viongozi wakuu wa CDM kutoa hotuba kali katika mkutano uliovunja rekodi ya kisiasa mkoani Mtwara katika viwanja vya Mashujaa.

Mbali na maelfu ya watu waliochukua kadi za CDM siku hiyo lakini jana tu na juzi karibu kila kijana aliyeonekana mjini Mtwara alikuwa anaonyesha kadi ya CDM.Siku ya mkutano wa kwanza wanachama wa CCM waliorudisha kadi walikuwa 1500 CUF kadi 50 na NCCR kadi 53.Katika mkutano huo wananchi walikichangia chama hicho shilingi milioni 1.5 kusaidia kuendeleza vuguvugu la mabadiliko.

SOURCE:MTANZANIA UK 8
 
....."Tunakwenda Mtwala na Lindi kwa ziara ya siku 15,Habaki mtu,haponi mtu"....Kauli ya Mhe,Mbowe akiwa katika viwanja vya Chadema square(Jangwani) tarehe 26 may 12 Jiji Dsm

Hakika inatia moyo sana.
 
Moto ni ule ule makanda! Msichoke na kukatishwa tamaa na mamluki kama shibuda! Kazeni buti twaikaribia neema!
 
Katika hali inayoonyesha kampeni ya M4C mikoa ya kusini imevunja rekodi wananchi mbalimbali hususan vijana wamekuwa wakigombea kadi za CDM na wengine kuzisaka sehemu mbalimbali mjini Mtwara.
Hali hiyo imeanza kujidhihirisha tangu juzi siku moja baada ya viongozi wakuu wa CDM kutoa hotuba kali katika mkutano uliovunja rekodi ya kisiasa mkoani Mtwara katika viwanja vya Mashujaa.Mbali na maelfu ya watu waliochukua kadi za CDM siku hiyo lakini jana tu na juzi karibu kila kijana aliyeonekana mjini Mtwara alikuwa anaonyesha kadi ya CDM.Siku ya mkutano wa kwanza wanachama wa CCM waliorudisha kadi walikuwa 1500 CUF kadi 50 na NCCR kadi 53.

SOURCE:MTANZANIA UK 8

Yule mtayarishaji wa CCM blog yuko wapi akanushe na hili?????!!!!
NyinyiEM bye bye; NyinyiEM bye bye!!
 
....."Tunakwenda Mtwala na Lindi kwa ziara ya siku 15,Habaki mtu,haponi mtu"....Kauli ya Mhe,Mbowe akiwa katika viwanja vya Chadema square(Jangwani) tarehe 26 may 12 Jiji Dsm

Mkuu nukuu hii ni tamu mno!
 
Arusha haifikii Mtwara hata punje kwa sasa naona mapinduzi yataanzia kusini kwenda kaskazini hawa jamaa wapo fit zaidi ya G8
 
Yule mtayarishaji wa CCM blog yuko wapi akanushe na hili?????!!!!
NyinyiEM bye bye; NyinyiEM bye bye!!

Maana alisema wamekwaa kisiki,aje tena maana nimepitia nyinyiem blog hamna kitu,ngoja tumsubirie vuvuzela nape aje kukanusha hii taarifa.
 
Back
Top Bottom