Kadi yangu ya CCM niifanye nini?

Kwa upande mwingine namshukuru muumba kwa kuniepusha na nyinyi emu. Wakati ule wa JKT tulilazimishwa kujiunga na Umoja wa vijana na nilikuwa na kadi kwa huo mwaka lakini nahisi niliitupia quarter guard siku ya kutoka maana sijawahi kuiona kamwe tangu wakati huo. Sikuona na hata sasa sijaona mantiki ya kujiunga na chama cha siasa kwa TZ.
 
I flash chooni mapema kabla hujachanganyikiwa na masuala ya hicho chama
 
Badala ya na nyie kulalamika lalamika si mpeleke kauli hizi kwenye vikao halali vya chama? Kulalamika humu kuwa chama kina angamia haisaidii chochote. Aidha uache kuwa mwanachama au uwe mabadiliko ndani ya chama chako.
 
Sasa kuna kamwanga kanajitokeza kwa mbaaaaaali, huenda nikafanikiwa kuithaminisha upya kadi yangu ya chama. Wana-ccm wenzangu vipi, imani kwa KIKWETE bado ipo?
 

the word in italics sounds crazy!
 
Acha unafiki wako kwani ulipoenda kuzilipia ulilazimishwa na nani
 

Acha unafiki kwani kuna mtu alikulazimisha kwenda kulipia hiyo kadi.
 
usitupe mbona wimbo wa Komba bado mzuri ule wa ccm ccm oooh chama cha mapinduzi ccm namba wani" au na nyimbo umezichoka mimi bado nazipenda hasa chorus
 
the word in italics sounds crazy!

Mapinduzi ndani ya ccm yamefanikiwa kuiondoa sekretarieti ya Makamba kwa kutumia kauli mbiu ya 'kujivua gamba'. Juzi Nape kachokoza mada ya kumng'oa JK kwenye nafasi yake ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, pale aliposema '....hata mtu anapooga anaanzia kichwani' na kichwa chenyewe kinachozungumziwa hapa ni kinara wa ufisadi au fisadi namba 1 katika list of shame, kazi bado mbichi. Lazima JK ang'oke kwenye nafasi yake ya uenyekiti wa ccm....ili chama kijivue gamba completely!
 

Ushanunua hisa,subiri gawio!
 
Kadi yako baki nayo we mwenyewe si uliinunua kwa mapenzi yako..,Baki bayo tuu ila utubu kuwa utakuwa mtu mwema..!
 


Ningekuwa mimi ni wewe ningeenda kuichambia chooni
 
hiyo ni hazina kubwa. hakuna chama chenye nia ya kweli ya kumkomboa mtanzania kama CCM. Itunze kadi yako na hakikisha unaitumia kushauri mazuri ya kufuata na kutekeleza. mara zote lipia kwa vipindi vya miaka 4, kwani 4800 ni sawa na bia 3 tu za dakika 40 lakini unakuwa hai kwa miaka 4
 
mpambanaji, wewe ni mpambanaji kwelikweli, na nimeupenda sana ushauri wako. Kibwagizo; Chama chetu cha Mapinduzi chajenga nchi x2, Nyerere, aaaah! Kawawa wajenga nchi. Karume, aaaaah! Sokoine, wajenga nchi. Bahati mbaya saaana wana-CCM wa ukweli tumebaki wapweke, maana viongozi wetu wote ni marehemu...kondoo wametawanyika, wamebaki bila mchungaji .... CCM yajenga nchi, Nyerere aaaah, Karume wajenga nchiiii! My take: Nchi haijengwi na marehemu!
 
Kadi yangu iko ndani ya briefcase inanikumbusha mbali tulivogawiwa kwa lazima. Nimeiweka karibu na kadi yangu mpya ya cdm. Zitajuana humo ndani ya briefcase,najua itakuwa inazomewa sana na kadi yangu niliyoinunua elfu na miatano wakati ile nlipewa bure ila cha ajabu ile ya kijani ina risiti ya malipo sijui alilipia nani. Pia ile ya kijani unisaidia kulinda kibarua changu mara moja moja ila hawajui kuwa huwa nawapiga changa la macho. Wenye kadi izo,najua na prof Azaveli Lwaitama kadi anayo,ila ameitunza. Tutunze kadi zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…