Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,990
- 31,371
Jumamosi kama ilivyo kawaida ni siku ambayo kunakuwa na harusi nyingi,bahati nzuri mimi ni mmojawapo kati ya wageni waalikuwa kwenye harusi moja kubwa ambayo niliichangia fedha nyingi kiasi, kwasababu Bwana harusi ni mtu wangu wa karibu.
Nafika getini [Arusha City Park] nakumbana na walinzi wanaodai kadi ya mwaliko nawakabidhi kadi bila kusita,walinzi wanakagua kadi kwa makini dk mbili tatu zinapita wananirejeshea kadi yangu na kuniambia huwezi kuingia ndani kwasababu kadi yako ni feki walinzi wengine wananiambia kadi yangu ni ya kichina !!!!!!!!!!.Bahati nzuri mwanakamati moja anapita getini na kuwaelekeza walinzi waikubali kadi yangu bila kuelezwa sababu za kudhalilishwa kiasi kile.Wachina kweli wakali yaani mpaka kadi za mwaliko tunawasingizia