#COVID19 Kadi chanjo ya COVID-19 kulipiwa Sh 20,000 Zanzibar

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
Unguja. Wakati idadi ya watu waliopata chanjo ya corona Pemba na Unguja ikifikia 10,000, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema waliochanja na kukamilisha dozi zao watapewa kadi maalumu kwa kulipia Sh20,000.

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui aliileza Mwananchi juzi kuwa kadi hiyo itatolewa baada ya kukamilisha taratibu zote za kupata chanjo, japo sio lazima kulipia isipokuwa kwa anayehitaji.

“Kwanza achanje, kisha anaingizwa kwenye system (mfumo), atapewa namba anakwenda benki kulipia Sh20,000, akishalipia atapata ujumbe kwamba asante sana kwa malipo yako, njoo tarehe fulani ukachukue kadi yako,” alisema Mazrui.

Pia, alisema fedha hizo zitalipwa kupitia akaunti ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) au kwenye simu na watu wameanza kupata ujumbe huo.

Alisema tayari wizara imeshaanza kuzitayarisha kadi hizo kulingana na kiwango cha chanjo walichonacho na hadi sasa kuna chanjo 55,000 za Sinavac na chanjo 30,000 za Sputnik Light 5.

Alisema hadi kufikia Agosti 12, tayari watu 10,000 walishapatiwa chanjo hizo visiwani humo, huku akiwasisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Uviko-19 kwa kunawa mikono, kuvaa barakoa na kuepuka misongamano isiyo ya lazima.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali Mtandao (E-Goverment), Said Seif alisema kadi hiyo itakuwa na namba maalumu za siri za mhusika kutokana na masuala ya kiafya kuhitaji usiri.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema hali hiyo itawafanya wananchi wengi kubaki njiapanda, maana kiwango cha fedha ni kikubwa ikilinganishwa na maisha halisi ya Mzanzibari.

“Najua kama afya ni gharama, lakini naiangalia jamii inayopata mkate kwa chai, kweli watazimudu hizi gharama?” alihoji Masoud Mzee.

Neema Mohmed alisema kulipisha kadi hiyo kwa gharama ya Sh20,000 ni kubwa ambayo watu wengi watashindwa kuimudu.

Alishauri watu wangeambiwa wachangie Sh 2,000.

Mwananchi
 
Kwa nini wanaongeza idadi ya cards kwenye wallet ya mwananchi. Kitambulisho cha ukaazicau cha taifa(NiDA) kingetosha. Wangeweza kuongezea data za chanjo ya covid kwenye database ya NIDA.
 
Watu wakiisasambua corona na siasa zake za uzandiki wanaonekana punguani, sasa ya nini mtu kuchanjwa halafu ulipie gharama wakati huugui na mwilini hakuna tishio la ugonjwa huo? Corona ni ugonjwa wa kisiasasiasa tu na ujanjanja wa kulaghai watu
 
Hio kadi wanasema ni hiari ila makazini,sehemu za hosp etc itakua lazima uionyeshe upate huduma husika
 
Unguja. Wakati idadi ya watu waliopata chanjo ya corona Pemba na Unguja ikifikia 10,000, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema waliochanja na kukamilisha dozi zao watapewa kadi maalumu kwa kulipia Sh20,000.

Utasikia Bara nao wameiga.

Yaani nchi hii, kila kitu wananchi wanakihitaji sana serikali inaona fursa ya kutukamua tozo! Hawa dawa yao ni kuwafanyia ugaidi wa kweli tu, sio huu wa kusingizia.
 
Kwa nini wanaongeza idadi ya cards kwenye wallet ya mwananchi. Kitambulisho cha ukaazicau cha taifa(NiDA) kingetosha. Wangeweza kuongezea data za chanjo ya covid kwenye database ya NIDA.
Database yenyewe ya nida ina makosa wakati ule wa online copy database zilikuwa zinafukuliwa sana na kugunduliwa makosa kibao...
 
Unguja. Wakati idadi ya watu waliopata chanjo ya corona Pemba na Unguja ikifikia 10,000, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema waliochanja na kukamilisha dozi zao watapewa kadi maalumu kwa kulipia Sh20,000.

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui aliileza Mwananchi juzi kuwa kadi hiyo itatolewa baada ya kukamilisha taratibu zote za kupata chanjo, japo sio lazima kulipia isipokuwa kwa anayehitaji.

“Kwanza achanje, kisha anaingizwa kwenye system (mfumo), atapewa namba anakwenda benki kulipia Sh20,000, akishalipia atapata ujumbe kwamba asante sana kwa malipo yako, njoo tarehe fulani ukachukue kadi yako,” alisema Mazrui.

Pia, alisema fedha hizo zitalipwa kupitia akaunti ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) au kwenye simu na watu wameanza kupata ujumbe huo.

Alisema tayari wizara imeshaanza kuzitayarisha kadi hizo kulingana na kiwango cha chanjo walichonacho na hadi sasa kuna chanjo 55,000 za Sinavac na chanjo 30,000 za Sputnik Light 5.

Alisema hadi kufikia Agosti 12, tayari watu 10,000 walishapatiwa chanjo hizo visiwani humo, huku akiwasisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Uviko-19 kwa kunawa mikono, kuvaa barakoa na kuepuka misongamano isiyo ya lazima.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali Mtandao (E-Goverment), Said Seif alisema kadi hiyo itakuwa na namba maalumu za siri za mhusika kutokana na masuala ya kiafya kuhitaji usiri.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema hali hiyo itawafanya wananchi wengi kubaki njiapanda, maana kiwango cha fedha ni kikubwa ikilinganishwa na maisha halisi ya Mzanzibari.

“Najua kama afya ni gharama, lakini naiangalia jamii inayopata mkate kwa chai, kweli watazimudu hizi gharama?” alihoji Masoud Mzee.

Neema Mohmed alisema kulipisha kadi hiyo kwa gharama ya Sh20,000 ni kubwa ambayo watu wengi watashindwa kuimudu.

Alishauri watu wangeambiwa wachangie Sh 2,000.

Mwananchi
Hii taarifa ina walakini.yaani ulipie cheti.au unalipia chanjo yenyewe? sidhani kama na huku Bara italetwa hiyo story
 
Back
Top Bottom