Kadhia za wanyamapori kuvamia makazi na mazao, nini Serikali ifanye?

Raphael Thedomiri

JF-Expert Member
Sep 1, 2019
442
728
Habari zenu wana JF wenzangu.

Niende moja kwa moja kwenye majadiliano ninayo yaleta mbele yenu.

Sasa imekuwa ni kama kawaida kila iitwapo leo katika vyombo vya habari kuna ripotiwa majanga chungu nzima ya madhila ya wanyamapori wanayofanya katika jamii, tembo wanaharibu mazao, juzi kati tuu hapo kumeripotiwa watoto waliouwawa na fisi, hivi karibuni kabisa huko Tanga, tembo wameharibu mazao na kutishia hata maisha ya wananchi wenzetu.

Sasa mimi nimejaribu kuyatafakari madhila yote hayo, nikajaribu kufikiri yatatatulika vipi matatizo hayo? Tunazihitaji maliasili zetu lakini tunahitaji ustawi wa raia wenzetu.

Hilo limekuwa swali gumu mno kwangu. Nikasema niiwasilishe hii hoja kwenu wakuu, ni upi unaweza kuwa mwarobaini na suluhisho na utatuzi wa changamoto hiyo?!

Screenshot_20220829-082613_M-Paper.jpg
 
Back
Top Bottom