Kadhia ya Makonda: Dhana ya bunge halina ‘’meno’’ inakufa kifo cha mende.

Nilikuwa namtetea sana magufuli kwa sasa nimebadili uamuzi sitaki tena huwezi kuruhusu hadi mkuu wa mkoa adharirishe watu kiasi hiki tena anashindwa hata kumkemea, nchi inaendeshwa kibabe sasa hatutaki ngoja 2020 tutaonana kwenye sanduku
Halli inatisha wala huyu si dicteta ni.......
 
Je bunge la bajeti linaloanza mwezi wa nne lina uwezo wa kuibua suala la bashite na kumshinikiza mkulu huyo kuchukua hatua dhidi ya RC huyo? Je bunge linaweza likaweka historia ya kumuwajibisha Waziri mkuu kwa Mara ya kwanza tangia Uhuru?

Je bunge lina uwezo wa kuihoji serikali juu ya matumizi mabovu ya fedha yasiyo na Baraka za bunge?

Je bunge litakuwa na uwezo wa kuhoji ukiukwaji mkubwa wa katiba unaofanywa na raisi bila raisi mwenyewe kuwa na mhemko na kuwatishia wabunge wa chama chake?

Je kwa wanaomfahamu raisi, atajibuje atakapoulizwa alipopeleka fedha za ajira ya mwaka 2016/2017? Fedha ya ongezeko la mishahara? Fedha ya kupandisha madaraja kwa watumishi wa umma?.

Jibuni kwa wanaomfahamu, mheshimiwa atajisikiaje suala la kupeleka madaktari 500 Kenya wakati zahanati za serikali hawana hata wakunga?

Atajisikiaje pale atakapoulizwa kuhusu elimu bure utekelezaji wake, shule hazina walimu ni magofu tupu, hakuna vitabu walimu hawana morali ya kazi tena!

Ongezea na wewe mambo ambayo raisi akiulizwa leo atakosa majibu yake na kuishia kujing'ata ng'ata kama lile swali aliloulizwa na Paskali Mayalla.
 
Nadhani mjinga ni wewe na hao waliokutuma kueneza injili ya kipumbavu kama hiyo. Kama atakataa kutii kwa vile kapewa kichwa na huyo business partner mwenzake ziko njia zingine. Na hilo la ufisadi sijakuelewa sawasawa. Ni nani ktk ccm ambaye Siyo fisadi mpk dkk hii ninapokujibu? Kama yupo nitajitoa jf sasa hivi
 
Kuna methali inayosema, Mwanga mpe mtoo alee. Methali nyingine inasema, Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu.

Mpaka sasa inavyoonekana wapinzani hawajalielewa somo la siasa za CCM ndani ya bunge na nje ya bunge.

Kwa muda mrefu, wapinzani waliisumbua sana CCM kwa kutumia dhana ya ufisadi. Kila mara CCM walikuwa wakishambuliwa kuwa ni mafisadi.

Kwa kutumia dhana ya mwanga mpe mtoto alee, CCM walitengeneza mazingira yaliyowafanya wapinzani kumchukua na kumlea mtoto wa CCM ambaye alikuwa ni nembo ya dhana ya ufisadi nchini.

Siku ambayo Lowassa alihamia CHADEMA ilikuwa ni siku ambayo hoja ya ufisadi kutoka upinzani ilikufa kifo cha mende mpaka hata neno ufisadi likaondolewa kwenye makabrasha ya upinzani.

Baadaye iliibuka hoja ya ‘’bunge la sasa halina meno’’ kutoka kwa wapinzani wakafikia mpaka hatua ya kuweka karatasi kuziba midomo yao.

CCM wamehangaika na hoja hii lakini kwa kutumia dhana ya ‘’ndege mjanja hunaswa na tundu bovu’’ wameanza kuiua kwa umakini mkubwa.

Tumeona na kusoma kwenye vyombo vya habari jinsi ambavyo baadhi ya wapinzani wakishangilia kuitwa kwa Makonda anayedaiwa ni ‘’kiongozi aliyekaribu’’ na Rais Magufuli kwenye kamati ya kudumu ya Bunge inayoshughulika na Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili ‘’akasulubiwe’’ baada ya wabunge kutoa azimio la pamoja.

Kwa maana nyingine kimantiki wanatuambia Bunge lina meno kwa sababu limeweza kumuita kiongozi ambaye wapinzani wanadai ni ‘’sauti ya Rais Magufuli’’ ili wamsulubu. Kwa maana nyingine, kuisulubu ‘’sauti ya Rais Magufuli’’ ni kumsulubu Rais Magufuli.

Wapinzani bila kujua wanachofanya ni kuua dhana ya ‘’bunge la sasa halina meno’’ pale ambapo masuala ya msingi kwa taifa yatakapojiri bungeni siku sijazo.

CCM wanafahamu vizuri kuwa mashitaka ya Makonda hayana athari zozote kwake na kwa CCM badala yake yanaifanya CCM na serikali yake kuimarika zaidi katika macho ya Watanzania kuwa bunge lina meno yake. Kusema bunge halina meno ni porojo tu.

Kuna ‘’wajinga’’ wasiojua taratibu na kanuni za bunge wanashangilia wakidhani Makonda atasimama ndani ya ukumbi wa bunge na kuanza kuhojiwa na wabunge. Hawafahamu kuwa mahojiano yatafanyika ndani ya ofisi za kamati yenye wajumbe 15 ambao kati yao kuna wabunge wa CCM 9.

Kikubwa zaidi, mashitaka ya Makonda hayawezi hata kutengeneza hoja ya kikanuni kumshauri Rais Magufuli amfute kazi badala yake, Kamati ya kudumu itatoa onyo/ushauri na biashara itaishia hapo.

Kwa mtu anayeangalia masuala ya kisiasa kwa kutumia 3D thinking atatambua kuwa suala la Makonda linaenda kuimarisha zaidi CCM na serikali yake huku likiwaacha wapinzani hawana hoja mbadala katika siku zijazo.

Politics is a dirty game!
Aibu! Suala LA Bashite liimarishe sisiyemu! Yaani kutumia cheti fake kunaimarisha sisiyemu! Kutumia vita ya madawa ya kulevya kujinufaisha binafsi kwa Bashite kunaimarisha sisiyemu! Hongereni!
 
Back
Top Bottom