Kadhia ya Makonda: Dhana ya bunge halina ‘’meno’’ inakufa kifo cha mende.

Kuna methali inayosema, Mwanga mpe mtoo alee. Methali nyingine inasema, Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu.

Mpaka sasa inavyoonekana wapinzani hawajalielewa somo la siasa za CCM ndani ya bunge na nje ya bunge.

Kwa muda mrefu, wapinzani waliisumbua sana CCM kwa kutumia dhana ya ufisadi. Kila mara CCM walikuwa wakishambuliwa kuwa ni mafisadi.

Kwa kutumia dhana ya mwanga mpe mtoto alee, CCM walitengeneza mazingira yaliyowafanya wapinzani kumchukua na kumlea mtoto wa CCM ambaye alikuwa ni nembo ya dhana ya ufisadi nchini.

Siku ambayo Lowassa alihamia CHADEMA ilikuwa ni siku ambayo hoja ya ufisadi kutoka upinzani ilikufa kifo cha mende mpaka hata neno ufisadi likaondolewa kwenye makabrasha ya upinzani.

Baadaye iliibuka hoja ya ‘’bunge la sasa halina meno’’ kutoka kwa wapinzani wakafikia mpaka hatua ya kuweka karatasi kuziba midomo yao.

CCM wamehangaika na hoja hii lakini kwa kutumia dhana ya ‘’ndege mjanja hunaswa na tundu bovu’’ wameanza kuiua kwa umakini mkubwa.

Tumeona na kusoma kwenye vyombo vya habari jinsi ambavyo baadhi ya wapinzani wakishangilia kuitwa kwa Makonda anayedaiwa ni ‘’kiongozi aliyekaribu’’ na Rais Magufuli kwenye kamati ya kudumu ya Bunge inayoshughulika na Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili ‘’akasulubiwe’’ baada ya wabunge kutoa azimio la pamoja.

Kwa maana nyingine kimantiki wanatuambia Bunge lina meno kwa sababu limeweza kumuita kiongozi ambaye wapinzani wanadai ni ‘’sauti ya Rais Magufuli’’ ili wamsulubu. Kwa maana nyingine, kuisulubu ‘’sauti ya Rais Magufuli’’ ni kumsulubu Rais Magufuli.

Wapinzani bila kujua wanachofanya ni kuua dhana ya ‘’bunge la sasa halina meno’’ pale ambapo masuala ya msingi kwa taifa yatakapojiri bungeni siku sijazo.

CCM wanafahamu vizuri kuwa mashitaka ya Makonda hayana athari zozote kwake na kwa CCM badala yake yanaifanya CCM na serikali yake kuimarika zaidi katika macho ya Watanzania.

Kuna ‘’wajinga’’ wasiojua taratibu na kanuni za bunge wanashangilia wakidhani Makonda atasimama ndani ya ukumbi wa bunge na kuanza kuhojiwa na wabunge. Hawafahamu kuwa mahojiano yatafanyika ndani ya ofisi za kamati yenye wajumbe 15 ambao kati yao kuna wabunge wa CCM 9.

Kikubwa zaidi, mashitaka ya Makonda hayawezi hata kutengeneza hoja ya kikanuni kumshauri Rais Magufuli amfute kazi badala yake, Kamati ya kudumu itatoa onyo/ushauri na biashara itaishia hapo.

Kwa mtu anayeangalia masuala ya kisiasa kwa kutumia 3D thinking atatambua kuwa suala la Makonda linaenda kuimarisha zaidi CCM na serikali yake huku likiwaacha wapinzani hawana hoja mbadala katika siku zijazo.

Politics is a dirty game!
Matatizo ya CCM bado ni mengi tu. kinachojitokeza hasa katika hii kadhia ya Makonda kuitwa bungeni, ni CCM wenyewe kuwa na utengano. hoja hii isingepita kama wabunge wa CCM wasingeiunga mkono. kwa hiyo tutarajie kuona mgawanyiko zaidi katika CCM
 
Lafudhi ni Kiswahili kilichosanifiwa, lafdhi ndiyo Kiswahili asli (asili).

"Kaake waona lile piji? Kaake lile si piji ule ni mforojo lawa maji".

Tafuta Mpemba akutafsirie, hicho ni Kiswahili kwa lafdhi na madaha ya Kipemba.
Kwa hiyo zote lafudhi wewe umetumia ya kipemba na yeye kutumia ya kikurya kosa liko wapi
 
Msema Ukweli nimepitia kwa kina sana comment zako, nimekulewa kwamba kama vile unajaribu kuwatahadharisha Upinzani kwamba wanachofanya kitawanufaisha CCM badala ya kuimaliza CCM, Nilichoshindwa kukuelewa ni; Sijaona mahala popote uliposhauri "nini kifanyike", badala yake umeishia kulaumu tu na wewe binafsi kulalamika tu, lakini mtu mkomavu hutoa ushauri wa nini kifanyike ili kuepukana na kile anachoamini kuwa hakiendi vizuri. Nakushauri kila unapopost hoja toa na "wayforward".
 
Hawa wabunge uchwara mimi siwaelewi wanadai wasiingilwe kwenye bunge lao wakati huo huo wao wanataka wamuingilie rais kwenye uteuz wake
 
Msema Ukweli nimepitia kwa kina sana comment zako, nimekulewa kwamba kama vile unajaribu kuwatahadharisha Upinzani kwamba wanachofanya kitawanufaisha CCM badala ya kuimaliza CCM, Nilichoshindwa kukuelewa ni; Sijaona mahala popote uliposhauri "nini kifanyike", badala yake umeishia kulaumu tu na wewe binafsi kulalamika tu, lakini mtu mkomavu hutoa ushauri wa nini kifanyike ili kuepukana na kile anachoamini kuwa hakiendi vizuri. Nakushauri kila unapopost hoja toa na "wayforward".

Asikupige upofu,tangu lini uvccm akatoa ushauri kwa upinzani?
 
Wapinzani tunaponzwa na viongozi wetu
Mkuu unaona mbali sana. Kuna baadhi ya viongoz wanakurupuka na ajenda na kuiacha njian, wanakamata mpya mbio kwenda wasikokujua, kisha wanaposhtuka uchaguzi umefika wanahamia huko na kusahau ajenda ya nyuma iliishia wapi! Kama wangetulia,wakashirikiana, wakapanga mikakati na kutekeleza kwa mtiririko na mshikamano, hakika ccm leo isingekuwa ofisin. Viongozi wa UKAWA, bila kujijua wanagonganishwa na ccm. bila kuvuta subira na kuchunguza jambo, wanaanzakulumbana na kujikuta wamemeguka kila MTU na uelekeo wake. Binafsi naumia sana ninapoona kiongozi wa UKAWA anavurugana na kiongoz mwenzie. Hii hupunguza nguvu ya kupambana na adui zetu. Mungu inusuru UKAWA.Iko siku UKAWA itasimama mbele za umma na kuongoza nchi.
 
IMG-20170210-WA0013.jpeg
 
Back
Top Bottom