hizi taasisi zote na asasi za kiraia NGOs zinatakiwa zisajiliwe:iwe mashule, vyuo vikuu, makanisa misikiti n.k. ili zifanye mambo kwa mujibu wa kanuni za nchi na kwa Ustawi wa jamii. Ndio lengo la kuzisajili.Ni kama vile bidhaa yenye TBS, kupitia kuzisajili kuna wapa manufaa fulani kama ruzuku, uhakika wa kukopa n.k.
Nikitoa mfano: Serikali yetu haiwezi kusajili kikundi chenye jina la "Muslim brotherhood", hata serikali ya Saudiarabia ama ya Egypt, haiwezi kusajili chama kama hiki kwani ni chama cha kigaidi.Hili swala nchi kama Qatar wameshaanza kugundua pia.
tUkirudi kwenye hoja ya kadhi: haiwezi kujijengea hoja binafsi na ikafanikiwa:Ila kwasababu ni hoja inayogusa jamii kubwa wanaichukulia kama ni jambo la kuzungumuza. Ni kama wale wa-adzabe waliosema ili waisikilize serikali, inabidi wachinjiwe Nyama Ya Punda wale .mwishowe serikali iliwachinjia.Ili tu kujenga maelewano.
kimsingi hii hoja haina mashiko kwa nchi ya kisecular kama Tanzania yenye lengo la kujenga umoja wa kitaifa.Nchi zote duniani zimekuwa ziki-attempt kutenganisha serikali na dini kuepusha ukiukwaji wa haki za binadamu. Ni changamoto sana kusimamia haki za binadamu kupitia mifumo ya kidini. pia sheria hii inaweza kudhohofisha ukuaji wa ukristo na demokrasia pia kuleta migogoro mikubwa kwenye jamii. nadhani
Kikwajuni One unatakiwa uliangalie hili kwakina ikiwemo dhamira ya waleta hoja hizi jinsi walivyo. Usipumbazwe na changamoto za utandawazi kwenye mataifa ya arabuni. Uislamu ni serikali tosha.
vivyohivyo ukristo. sasa kama tunatofauti za kiitikadi inabidi tutenganishe dini na serikali hasa katika kuingiza mambo ya kidini ambayo wangeweza kuyasiimamia wenyewe kwenye dini zao. wakristo wa Ulaya walifanya hivyo kwenye mwaka wa 500 na imewasaidia kupiga hatua kubwa kidemokrasia na kimaendeleo.Ni swala la hekima zaidi.