Kada wa CCM Arusha atangaza kumvaa Lema

Kada wa CCM Arusha atangaza kumvaa Lema

buswelu moja

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2014
Posts
226
Reaction score
183
Joto la ubunge katika jimbo la Arusha mjini limezidi kupanda mara baada ya Kada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoani Arusha,Kim Fute kutangaza rasmi kuwania ubunge katika jimbo hilo endapo akipewa ridhaa na chama chake kugombea.

Kim,amejitokeza kutangaza azma hiyo ikiwa ni siku chache baada ya makada wengine wa CCM ambao ni Phillemon Mollel,Victor Njau,Thomas Munisi,Deo Mtui,Godfrey Mwalusamba kutangaza nia ya kuwania jimbo hilo linashikiliwa na mbunge wake,Godbless Lema ambaye tayari ametangaza kugombea tena.

Akizungumza na gazeti hili jijini hapa,Fute alisema kuwa amesukumwa na dhamira ya kuwania ubunge katika jimbo hilo mara baada ya kutathmini na kubaini ya kwamba jimbo hilo linakabiliwa na tatizo la ombwe la uongozi.

Alisema kwamba amejipima vya kutosha na kubaini ya kwamba ana sifa za kutosha za kuwawakilishi wakazi wa jimbo la Arusha mjini ambao alidai kwa muda mrefu wamekuwa wakikosa viongozi bora wa kuwawakilisha.

Kada huyo alisisitiza kwamba miongoni mwa mambo ambayo atakwenda kuyafanyia kazi pindi akifanikiwa kuwa mwakilishi wa jimbo hilo ni pamoja na kushughulikia suala la usalama wa mji wa Arusha ambalo alidai tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 mji huo umeandamwa na matukio mbalimbali kama maandamano,vurugu na mambomu.

Alisema kuwa mji wa Arusha ni mji wa kimataifa na pia una fursa nyingi kama kitovu cha utalii hapa nchini na duniani hivyo atajikita kuhakikisha anasimamia hali ya kurejea kwa usalama ili biashara hiyo iweze kufanyika kwa uwepesi kwa kuwa inachangia pato kubwa la taifa.

"Arusha ni mji wa kimataifa na una fursa nyingi kama biashara ya utalii ambayo inachangia pato kubwa la taifa lakini usalama ni hafifu na unaharibu kwa kiasi kikubwa hivyo nitajikita kuhakikisha hali ya usalama inarejea"alisema Kim

Hatahivyo,alibainisha kwamba mbali na usalama pia atahakikisha anakutana na makundi mbalimbali ya viongozi wa dini zote,waandishi wa habari pamoja na wadau wa maendeleo jijini hapa ili kuangalia namna ya kuuweka mji wa Arusha katika hali ya utulivu.

"Tunahitaji mtu sahihi wa kuunganisha siasa na uchumi mzuri, endapo nikifanikiwa kuwa mwakilishi nitahakikisha ninakutana na makundi mbalimbali ili kujadili kwa kina changamoto zetu na kubadili fikra na mtazamo kwa wakazi wa Arusha"alisisitiza Fute

Mwisho.
 

Attachments

  • KIM FUTE.jpg
    KIM FUTE.jpg
    1.6 MB · Views: 1,035
Hahahaha, tangazeni mkinaliza mje mtaani mkutane na nguvu ya umma. Jamani eleweni arusha hatuwezi tukarudi nyuma tena na kwenda kwa hawa wezi. Wamekuwa na hili jimbo for more than 30 years, nothing done leo wana leta midomo. Too late to catch the flight.
 
Kwa arusha labda angeenda jimboni handeni au msoga jimbo la chalinze atapoteza rasilimali zake bure aje kujuta
 
ccm na act njooni mgombee Jiji la Arusha mjini mburuzwe na CHADEMA.
 
By the way anachemsha, arusha tatizo kubwa si usalama kama inavyovumishwa, tuna matatizo ya miundo mbinu, na huduma nyingine za kijamii, so hata hajui shida za waarusha. Kazi za ulinzi awaachie police.
 
Tusimkatishe tamaa mwache naye ajaribu bahati yake, lakini ningemshauri atafute jimbo lingine!
 
Watuletee hela walizofisadi angalau tupate Neema. Tunazipiga kama za Batilda Kisha tunamalizia Kazi kwa kumrudisha Lema.
 
yaani ccm hata aje Kikwete Arusha akijitahidi saba atapata kura 5000...
 
yaani ccm hata aje Kikwete Arusha akijitahidi saba atapata kura 5000...
Kuna jamaa yangu ananiambia Arusha magamba yana vikao km miaka 3 visivyoisha kutaka kukubalika na wanywa pombe na mishangingi ya CCM (Madalali wa nafasi za CCM -si unajua JK alisema mwenyewe kuna madalali wa uwaziri)..sasa hawa wana CCM ambao huwa ktk baa fulani fulani wanazokunywa wafanyabiashara wanaochangia ccm ili kukwepa kodi...wana vikao vingi...halafu wanaambiana ujinga kwamba Lema hana kitu ni maandamano tuu wananchi wameshachoka....kwa hiyo wamebaki hujumiana tuu na kukamuana hela.Kwa ujumla utasikia vita...wengine wamejaribu toa hela ili wakutanishwe na "headache ya CCM" kwa vile wanaamini ndiye atakuwa rais na mwenye ushawishi.
 
Back
Top Bottom