Kada mkongwe VUTA NKUVUTE yuko wapi?

Kada mkongwe VUTA NKUVUTE yuko wapi?

Thread zako zilikuwa zikifanya kila mwenye kusoma arudie mara mbili mbili ili aweze kupata ladha ya uandishi wako adhimu na mpangilio wa vina.

Ni kitambo sasa mambo mazito yanatokea lakini hauonekani kutuleta taarifa kama ambavyo ilikuwa desturi yako.

Je intelijensia ya CCM imekung'amua na hivyo kukunyima "access" ya kupata taarifa mbali mbali za chamani na hasa ofisi ndogo ya Lumumba ambazo ulikuwa akituwekea hapa jukwaani?

Wana jukwaa nawauliza: Amepotelea wapi Kada huyu wa CCM wa ofisi za Lumumba na Mwanachama wa TLS.

VUTA NKUVUTE jitokeze sasa utupe yale yanayoendelea huko Lumumba. Kama na wewe unaisoma namba basi tuhabarishe wanajukwaa japo kwa whatsapp tutaendelea kuugulia huku tulipo kimoyo moyo.

Kinyungu.
Yupo Dodoma na Rais wa TLS
 
Isije ikawa yule kada wa CCM aliyewekwa ndani kwa zaidi ya miezi miwili sasa kwa makosa ya kimtandao.
 
Akiweka mada lazima aseme yuko engo ipi ya nchi,Lumumba,Arusha,Dodoma
 
Back
Top Bottom