KADA CCM: Rais Magufuli ameacha mtafaruku Zanzibar

KADA CCM: Rais Magufuli ameacha mtafaruku Zanzibar

Rais anakuwa mpambe wa Jecha na kwa njia hiyo anawaunganisha wazanzibari. Tafakari.
 
Mkuu kuna kitu hakipo sawa, lazima tuseme bila kuogopa, zile sio kauli za Raisi wa nchi, tukimwacha aendelee kutoa kauli kama hizi atachafua nchi
Nadhani alihutubia kama mwenyekiti wa thithiemu na kama ni hivyo basi mikutano yote ya vyama imepigwa marufuku sasa hii ikoje mkuu au anavaa jezi ya serikali kwa kusemea chama?
Jamani huu si uonevu
Tukalilie wapi na yeye ndio mfalme
 
Rais yupo sahihi kabisa kuzungumza vile.
Ebu niambieni
1: Seif kutompa mkono Dr Shein ilikuwa sahihi? If not mbona mlimpongeza?

2:Je kitendo alichofanya Seif kilikuwa sahihi?

3:Is Seif matured enough in leadership ethics?

-Seif alionyesha chuki za dhahiri,sasa MTU kama huyo ya nini kujibembeleza kwake?

-Tunaoamini kauli ya "Qutayba lykhum Qisas" wala hatupati tabu na kauli za Mh. Rais.

Viva Magu viva
 
Mi nadhani hizi ngonjera awe anaimbiwa na Seif pia sababu ana wafuasi wengi tu huko Pemba.

Siyo Seif akionesha vitendo vya kuwagawa wazanzibar mnakenua na kumpongeza kwamba siyo mnafiki halafu ikipigwa count attack mnaanza kulialia.
 
Anandika Chilumba (yule mpiga zumari wa JPM)
Matamshi aliyoyatoa Ndugu Rais leo hapa Unguja sikuyatarajia yatoke kwenye kinywa cha mkuu wa nchi, Haya yanamwagia mafuta kwenye moto.
Suala kama la pensheni au matibabu ya mtu aliyewahi kuwa Kiongozi ni la kisheria siyo hiyari ya mtu, Yaan hata umfumanie na mkeo Sheria inakutaka usaini na apewe. Mengine mmalizane wenyewe.
Na kwa kuwa Tumesema siasa zimeisha Basi tujitahidi kuzimaliza kweli, sare za vyama, vijembe na maneno ya ngebe kwenye mikutano ya serikali inawagawa raia.
Siku zijazo wasio wana CCM wanaweza kuacha kuhudhuria mikutano ya Kiongozi mkuu wa nchi kwa sababu wanajihisi wanyonge na wakiwa.
Tuzungumze Maendeleo, kufanya kazi na kubadili maisha yetu, hawa Wakosoaji na wapinzani watakuwepo daima, kuwashambulia katika jukwaa lililolipiwa kodi na watu wote ikiwemo wao si jambo la kiungwana.
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Hotuba za Ndugu Rais katika ziara yake visiwani hazijanivutia wala kusisimua. Zimeiacha Zanzibar katika mtafaruku ule ule au mkubwa zaidi.
☝☝☝☝
Waswahili husema _"kenge huwa hasikiagi hadi damu imtoke masikioni"_. Masikio ya Chilumba yameanza kuonesha dalili za damu
Hachekewi mtu kinafiki!
Maalim amepewa za uso, anyoe au afuge ndevu.
Kwa vyovyote vile , mbele ya viongozi wa kitaifa Maalim ni nuksi, pengine ahudhurie skiketi nyuma kabisa.
 
Mkuu kuna kitu hakipo sawa, lazima tuseme bila kuogopa, zile sio kauli za Raisi wa nchi, tukimwacha aendelee kutoa kauli kama hizi atachafua nchi
Kama Donald Trump atashinda katika uchaguzi ujao wa Marekani ndipo nitaamini Magufuli yuko sahihi maana kauli zake ni mbovu na mbaya kuliko za Trump.

Nakubaliana nawe pia kwamba kuna kitu kibaya sana hatujakigundua katika utawala huu wa JPM ambacho bila kukipiga STOP huko mbeleni tutajuta. Kwa kweli yale si maneno ya kutamkwa na mkuu wa nchi mbele za wananchi wake.
 
Ilibidi Seif aambiwe ukweli.....inaonekana huwa mnavutiwa na hotuba za Rais sababu kila kukicha mnamnukuu.....inapendeza sana hii.
Si kila knachoangaliwa huwa ni kizuri. Hata "mizoga" watu wanaangalia. Na "knyesi" nacho hakikosi washangiliaji. Kuwa mwana falsafa.

Kama unaafiki mtu kuleta mambo binafsi ya nyumbani kwenye stahiki za kikatiba na kisheria, basi hiyo ni confirmation ya kauli za Lissu. Na kwa kuwa mikutano ya Rais anaposimama kama Rais inapambwa kiCCM, hiyo inamaanisha wasio wa CCM hawana sababu ya kumsikiliza Rais, maana all the time yeye anasimama kama mwenyekiti wa CCM
 
Mpaka sasa sijaona mantiki ya ziara yake Zanzibar.!
 
Anapenda kunyeyekewa anatumia ofisi za umma vibaya kwa matakwa yake banafsi hana toafaut na mla rushwa kushinikiza jambo flani lifanyike kwa matakwa yake binafsi afungue ofisi yake ila asainishe malipo yake kwa watu wake sio pesa za umma kutumia fimbo ya kumchapia aliekosa madaraka takukuru anzeni nae huyo.
 
Nakosaga muda wa kumwangalia au kumsikiliza maana ntavunja tv au radio na nshaacha kuangalia taarifa ya habari siku hizi
 
Back
Top Bottom