"Kachero" na Hatima ya CCM 2020

Kama kweli fisiem mna akili timamu ebu jaribuni ku figure it out ule wizi mlioufanyya uchaguzi wa 2015.... sasa image jazba hasira na ugwadu za watanzania zimeongezeka mara 10 juu yetu... Hamtoki hata kwa nini... Next yahya jamme is coming up 20/20... Hilo hali itaji akili za ziada kabisa kabisa yaani...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je,Swala la bombadier inawezekana ni kachero ndo kaiweka hadhari?[/QUOTE]
Ewaaaa!! Umepiga penyeww
 
Uzi huu pamoja na habari mbalimbali kwenye vyombo vya habari unaweza fikiri uchaguzi mwezi ujao? Hii inasikitisha sana vyama vingi vinafanya mambo ya maendeleo kumezwa na siasa pia huanzishwaji miradi ya kifisadi kuliko uwekezaji wa kwenye kilimo. Tunashindwa tumia ukubwa wa ardhi Tanzania kuzalisha chakula cha kutosha kuna masoko Congo , Sudan, Somalia , Rwanda na nchi nyingine tunafikilia nani kuwa raisi haaaaaaaaa. Hadi Leo naamini bila uwekezaji mpana kwenye kilimo kama taifa maendeleo yatachukua mda sana
 
Naamini Membe yuko vizuri na hakosi watu wake ndani ya vile vyombo visivyoonekana. Kwanza jamaa kadandia treni tuu kwa mbele na anapambana na kukata miti yenye mizizi mirefu. Angekuwa mjanja hiki kimya cha wazee wakongwe angeshtuka,kwenye siasa za ndani ya chama kimya huwa ni tishio kubwa, na alichomfanyia Nape kitam cost sana
Wajinga nyie hata mlisema Mkapa kawa kimya kwa KIKWETE
 
Inaonyesha jinsi gani hamjui hata ukubwa wa cheo alichonacho Raisi wa Jamhuri,yani huu uharo ulioandika hapa wewe uwe na taarifa nao JPM asijue?.. Halafu,nadhani mna matatizo kibao huko kwenye chama chenu,kwa style hii ndo maana mpaka July 2015 mlikuwa ndani ya CDM na UKAWA hamjui mtamsimamisha nani kuwa mgombea wa uraisi,maana mnakaa kipindi chote hiki mnapiga blah blah tu kuhusu CCM,na wewe tukuulize ya CDM,mwenye chama na mnunuzi wa chama LOWASSA atakubali LiSSU apitishwe kugombea uraisi na hali yeye kashatangaza akiwa KENYA?,huoni huo ndo mtiti wa kujadili hapa namna moto utakavyowaka kuliko kujadili ya upande wa pili?
 
Kuliko Membe bora Jpm mara millioni

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
 
Naamini Membe yuko vizuri na hakosi watu wake ndani ya vile vyombo visivyoonekana. Kwanza jamaa kadandia treni tuu kwa mbele na anapambana na kukata miti yenye mizizi mirefu. Angekuwa mjanja hiki kimya cha wazee wakongwe angeshtuka,kwenye siasa za ndani ya chama kimya huwa ni tishio kubwa, na alichomfanyia Nape kitam cost sana
Una hisi Nape au Membe wanaweza wakamfanya nini Rais mkuu.Kama walimmaliza Mkuu wa makachero/usalama Kombe iweje kachero tu wa Ikulu awaumize kichwa?Huyo wakitaka kumalizana na ma dakika tu na ukiona ana survive ujue sio threat kwao.

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
 
Membe ni garasa. Garasa la kutupa tu. Hamna kitu pale yaani empty kabisa. Membe hawez kuwa rais wa tanzania hata kama tanzania imekuwa kichwa cha mwendawazimu lakini si haki kufikia kuongozwa hata na watu ambao ni hopeless kabisa.

Magufuli hawez nyimwa usingiz na membe. Mwandishi wa hii thread ni membe mwenye au mdada wa karibu yake. Maana tulioko huku tunajua membe hana impact yoyote ccm hata mkoani kwake tu. Alikuwa akibebwa na ndugu yake kikwete lakini kwa sasa ameshasahaulila na hakuna wazee wenye akili wanaoweza kumtaka membe awe rais. Hakuna.

Ni watu wachache ambao mkapa huwaita wapumbavu ndo wnaweza luwa na mawazo ya kipuuzi kama yako. Nchi hii rais angekuwa membe ningeenda kuomba uraia sudan au somalia niepukane na aibu ya karne hii.



Na Dr. Musa Leonard Mdede

BENARD CAMILLIUS MEMBE : “Kachero“ anayemtesa JPM sirini

Akiwa na Uzoefu wa kufanya kazi ya “ukachero” katika Ikulu ya magogoni takribani miaka kumi (1978 - 1989 ) na mwanadiplomasia aliyehudumu katika ubalozi wa Tanzania jijini Ottawa,Canada kati mwaka (1992 - 2000) kabla ya kurejea nchini na kuhudumu kama mbunge wa mtama kwa miaka 15 (2000 - 2015 ) na na Naibu waziri wa Makazi,Nishati na Madini na baadaye Waziri wa Mambi ya Nje na Uhusiano wa kimataifa

Duru za kisiasa kutoka “corridor” za Lumumba yalipo makao makuu madogo ya CCM jijini Dar es Salaam zinadokeza kuwa hamkani mambo si shwari chamani.KACHERO Membe hayuko kimya kama wengi wanavyodhani bali yupo kazini kimkakati kuhakikisha 2020 “anakwaa” ugombea ndani ya chama hicho

Si yeye Membe binafsi bali Wazee ndani ya Chama ambao wengi wameamua kukaa kimya na hatuwasikii tena tangu awamu ya tano iingie madarakani na ahadi tele tele ambazo zimegeuka kuwa mithili kusubiri “Ferry” stendi ya Ubungo

Mwaka 2015 mara tu baada ya uchaguzi “Kachero” Membe alipata kuzungumza na wanahabari jijini DSM akikosoa namna mfumo wa “kukurupuka” unaotumika serikali ya awamu ya tano unavoharibu misingi iliyojengwa na watangulizi kama hivi sasa tunaposhuhudia Sakata la “Bombadier” na “ACACIA“

Press ya Membe ilidhihirisha kuwa haungi mkono “ukurupukaji” ambao mpaka sasa unaligharimu Taifa pakubwa.Kwa mara ya pili tena mwanzoni mwa mwaka 2016 Taarifa zilisambaa kupitia mitandao ya kijamii kama atazungumza na wanahabari katika kile kilichoonekana kutokukubaliana na hali ya mambo,ingawa hakuna ajuaye nini kilitokea kwani Press hiyo haikufanyika

Akiwa miongoni mwa tano bora kwa wagombea Urais ndani ya CCM mwaka 2015,Membe baada ya kushindwa kupata nafasi ya “Kupeperusha Bendera” ya CCM alitangaza kustaafu Siasa na kusaidia chama kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,Je,litekeleza ahadi yake hiyo kila mmoja anajua nini kilitokea kampeni za chama tawala 2015.Kwa sasa hali inaonekana kuwa tofauti kwani “wazee“ wamesikika wakisem “Bora tungempa Membe” ingawa wengi wanaongea kwa sauti ya chini kwa hofu ya kushughulikiwa

Upande wa pili,pangua pangua imeanza,kuwaondoa wale wote waliomuunga mkono na wanahofiwa watamuunga mkono wakati ukifika.Pangua pangua hii inaanzia ktk nafasi nyeti serikalini,Baraza la Mawaziri,Wakuu wa mikoa na wilaya na chamani pia ambapo tumeshuhudia baadhi ya mikoa kama Mwanza ambapo watu maalumu wameandaliwa kuwakabili wale wanaoonekana kuwa ni “watu” wa “Kachero Membe” haya ni maagizo yanayotekelezwa kutoka mamlaka ya juu zaidi

Wazee chamani “wanahaha” kukiokoa chama kwa kua wanajua chama kitaweza kupoteza uungwaji mkono katika chaguzi zijazo,ndomaana wengi hawasikiki tangu uchaguzi mkuu maaka 2015 kwani hawaridhishwi na hali ya mambo,kwani imeshuhudiwa baadhi ya nafasi ktk chaguzi ndani ya chama zikikosa wagombea kitu ambacho si cha kawaida kwa chama hicho kikongwe

Propaganda kadhaa za kujihami zimeandaliwa mahususi ili kudhibiti “vugu vugu” la kumkataa “JPM” chamani.JPM BAKI MPAKA 2030,PICHA YA BANGO UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA IKIONESHA JPM Rais(2015 - 2025),JPM ASIPINGWE 2020 CHAMANI & KATIBA YA CHAMA IBADILISHWE JPM AWE MGOMBEA “automatically“ 2020 BILA KURA ZA MAONI hizi ni propaganda zilizoandaliwa mahususi kuzima “vugu vugu“ la mbadala wa JPM

Wafanyabiashara,Wakuu wa mashirika ya umma na watumishi ktk nafasi nyeti wanaohisiwa ni “Watu wa Kachero” wanashughulikiwa kiaina ili kupunguza nguvu ya uungwaji mkono wa “Kachero” ndani ya Chama.

Mkulu anajua wazi kuwa atakuwa na wakati mgumu hapo mbeleni kwa kuwa hata moja ya familia ya Rais mmoja mstaafu “imejiapiza” kumfanya Rais wa muhula wa mmoja (one term president) kwa gharama yoyote na familia hii ina nguvu ndani ya chama na inatajwa kuwa na uhusiano na“Kachero”,hivyo mkulu baada ya kuona upepo unamwendea vibaya amefanya uteuzi wa mmoja wa familia hiyo ili kupunguza “munkari” wa kudhibitiwa,duru zinaonesha kuwa Baraza litapanguliwa ili mmoja wa wana familia kukalia moja ya wizara,ingawa bado hilo haliondoi “kiapo“ cha kuhakikisha kigingi kinawekwa kumzuia 2020

Wazee chamani wananena kwa sauti ya chini ili chama kipone lazima “Kachero” akalie “kiti cha enzi” kwa kuwa wanaona eti ana busara kuliko yule waliyempigania kwa jasho na damu na sasa wanadhihakiwa na watu wake waliokalia “viti vya enzi”naye,ingawa hawakumpigania yaani wanavuna wasichopanda,Katika kile Nape Nnauye alichokisema,“Wakati sisi tunaumia katika kutafuta KURA za CCM huko vijijini wengine walikua wanakunywa BIA Bar” hii inadhirisha kuwa kuna “Opportunist” wanaofaidi kuku kwa mrija na hali hawakupigania Chama.

Kisiasa hii ina afya kwa kua inamkosesha usingizi mkulu na angalau itamfanya aweze ku “behave” akijua fika hicho kiti ni cha moto kesho na kesho kutwa anaweza kalia mwingine

Hofu ya wafia chama ni kuwa juhudi zisipotumika chama kinaweza kikazama katika tope na kupata mkwamo wa kudumu jambo ambalo wafia chama hawataki kitokee kwa kua wanajua fika itawagharimu pakubwa kukirejesha katika mstari kwa kuwa kila kona ni malalamiko yanayoashiria uungwaji mkono haupo miongoni mwa walio wengi.

Wanaomfahamu Kachero Membe wanadai ni mtu aliyekaa magogoni kwa kipindi kirefu kama “Kachero” si wa kupuuzwa na ukimya una mshindo mkuu utakaohanikizwa na Hali ya kukosa dira ya awamu ya tano ambapo hata sasa kuna mkwamo mkubwa huku tukishuhudia sakata kadhaa zikitafuna serikali kuanzia “Uteuzi wa upendeleo wa ukabila na ukanda,Visasi kwa wafanyabiashara wakubwa,Ubadhirifu wenye sura ya kudhibiti vyombo vya habari kuripoti ukweki na uhalisia,“ACACIA na MAKINIKIA“ na sasa Sakata la fidia ya “BOMBADIER Q400 huko Canada

Je, Lumumba patakalika ama mambo yatakua tafarani zaidi ya 2015,tusubiri muda ni mwalimu mzuri...!!!@yale mabwabwa ya lumumba yata coment ujinga.

C&P from FB

My take;
J
ee hii yaweza kuwa ndio sababu ya kiwewe kingi cha mzee na kuwa na maamuzi ya kushangaza? imani imemuishia kwa wale walio mzunguka?
Na jee style hii ya hasira na chuki inamsaidia kuwakomoa wapinzani wake wa ndani ya chama na nje au ndio inazidi kumharibia?
 
Huyu 'kacheru' ndio alisema maadui zake watakimbilia kenya ? na sasa hivi namuona 'Elinino' akienda enda 'umasaini' ya nchi jirani sasa na yeye 'kacheru' ataenda ziwa Nyasa kuogelea
 
wewe unona ni mfarakano tu... wa watu wawili..

ukweli mwenyekiti wa ccm alikuwa hajajiandaa kuongoza chama... sasa ndani ya chama upo mgongano wa kimaslahi maana wapo wanao athirika na utendaji wa mkuu name wananguvu ndani ya chama... pia wapo wanaomkubali mwenyekiti...
Bila nguvu ya mwenyekiti wa sasa kipind kile kudondoka ilikuwa waz waz ndo mana zile kampen lilitumika sana jina la mwenyekiti kuliko chama sasa tumekijenga nadhan 2020 litatumika jina la chama kulko mwenyekiti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe huna lolote la msingi hapa. Unachojaribu ni kutafuta attention ya watu. Hizi zako ni riwaya mkuu chama kiko imara na hamna kinachofanywa kwa kukurupuka mambo yote yapo kwenye mpango kazi wa chama.

By the way hiki
chama sio cha mtu mmoja kama kilivyo Chadema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naomba tu asipate muhula mwingine maana hii first term amekurupuka kupitukia tena bado hivi ni mwanzoni mwa first term....tujiulize jee akishinda hiyo second term??....force rule ndo itazidi....Hakuna kiongozi yoyote ambae nitampenda kwa kosa hili kuwavunjia nyumba wananchi masikini bila ya kuwalipa fidia au kuwasaidia kwa njia nyingine yoyote ilimradi wasiteseke na wakufikiriwa zaidi ni watoto...TOO BAD

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili kosa baya sana. Tena hata kama watu walikua ndani ya hifadhi, lkn ki ubinadamu walipaswa kufikiriwa namna ya kustiriwa ki binadamu, na ikizingatiwa kwa kiasi kikubwa nchi yetu haijapimwa na wananchi wana uwelewa Mdogo sana masuala ya sheria. Tena kibaya zaidi wengi wao ni walala hoi ambao nyumba yenyewe aliipata ki bahati bahati tu.
 
Hili kosa baya sana. Tena hata kama watu walikua ndani ya hifadhi, lkn ki ubinadamu walipaswa kufikiriwa namna ya kustiriwa ki binadamu, na ikizingatiwa kwa kiasi kikubwa nchi yetu haijapimwa na wananchi wana uwelewa Mdogo sana masuala ya sheria. Tena kibaya zaidi wengi wao ni walala hoi ambao nyumba yenyewe aliipata ki bahati bahati tu.
Wanatumia madaraka vibaya lakini wajue kuwa matumizi mabaya ya madaraka yatawacost kwa baadae....nawahurumia sana wale watoto ambao wanalala nje na kuathiriwa kwenye masomo yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom