"Kachero" na Hatima ya CCM 2020

"Kachero" na Hatima ya CCM 2020

Na Dr. Musa Leonard Mdede

BENARD CAMILLIUS MEMBE : “Kachero“ anayemtesa JPM sirini

Akiwa na Uzoefu wa kufanya kazi ya “ukachero” katika Ikulu ya magogoni takribani miaka kumi (1978 - 1989 ) na mwanadiplomasia aliyehudumu katika ubalozi wa Tanzania jijini Ottawa,Canada kati mwaka (1992 - 2000) kabla ya kurejea nchini na kuhudumu kama mbunge wa mtama kwa miaka 15 (2000 - 2015 ) na na Naibu waziri wa Makazi,Nishati na Madini na baadaye Waziri wa Mambi ya Nje na Uhusiano wa kimataifa

Duru za kisiasa kutoka “corridor” za Lumumba yalipo makao makuu madogo ya CCM jijini Dar es Salaam zinadokeza kuwa hamkani mambo si shwari chamani.KACHERO Membe hayuko kimya kama wengi wanavyodhani bali yupo kazini kimkakati kuhakikisha 2020 “anakwaa” ugombea ndani ya chama hicho

Si yeye Membe binafsi bali Wazee ndani ya Chama ambao wengi wameamua kukaa kimya na hatuwasikii tena tangu awamu ya tano iingie madarakani na ahadi tele tele ambazo zimegeuka kuwa mithili kusubiri “Ferry” stendi ya Ubungo

Mwaka 2015 mara tu baada ya uchaguzi “Kachero” Membe alipata kuzungumza na wanahabari jijini DSM akikosoa namna mfumo wa “kukurupuka” unaotumika serikali ya awamu ya tano unavoharibu misingi iliyojengwa na watangulizi kama hivi sasa tunaposhuhudia Sakata la “Bombadier” na “ACACIA“

Press ya Membe ilidhihirisha kuwa haungi mkono “ukurupukaji” ambao mpaka sasa unaligharimu Taifa pakubwa.Kwa mara ya pili tena mwanzoni mwa mwaka 2016 Taarifa zilisambaa kupitia mitandao ya kijamii kama atazungumza na wanahabari katika kile kilichoonekana kutokukubaliana na hali ya mambo,ingawa hakuna ajuaye nini kilitokea kwani Press hiyo haikufanyika

Akiwa miongoni mwa tano bora kwa wagombea Urais ndani ya CCM mwaka 2015,Membe baada ya kushindwa kupata nafasi ya “Kupeperusha Bendera” ya CCM alitangaza kustaafu Siasa na kusaidia chama kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,Je,litekeleza ahadi yake hiyo kila mmoja anajua nini kilitokea kampeni za chama tawala 2015.Kwa sasa hali inaonekana kuwa tofauti kwani “wazee“ wamesikika wakisem “Bora tungempa Membe” ingawa wengi wanaongea kwa sauti ya chini kwa hofu ya kushughulikiwa

Upande wa pili,pangua pangua imeanza,kuwaondoa wale wote waliomuunga mkono na wanahofiwa watamuunga mkono wakati ukifika.Pangua pangua hii inaanzia ktk nafasi nyeti serikalini,Baraza la Mawaziri,Wakuu wa mikoa na wilaya na chamani pia ambapo tumeshuhudia baadhi ya mikoa kama Mwanza ambapo watu maalumu wameandaliwa kuwakabili wale wanaoonekana kuwa ni “watu” wa “Kachero Membe” haya ni maagizo yanayotekelezwa kutoka mamlaka ya juu zaidi

Wazee chamani “wanahaha” kukiokoa chama kwa kua wanajua chama kitaweza kupoteza uungwaji mkono katika chaguzi zijazo,ndomaana wengi hawasikiki tangu uchaguzi mkuu maaka 2015 kwani hawaridhishwi na hali ya mambo,kwani imeshuhudiwa baadhi ya nafasi ktk chaguzi ndani ya chama zikikosa wagombea kitu ambacho si cha kawaida kwa chama hicho kikongwe

Propaganda kadhaa za kujihami zimeandaliwa mahususi ili kudhibiti “vugu vugu” la kumkataa “JPM” chamani.JPM BAKI MPAKA 2030,PICHA YA BANGO UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA IKIONESHA JPM Rais(2015 - 2025),JPM ASIPINGWE 2020 CHAMANI & KATIBA YA CHAMA IBADILISHWE JPM AWE MGOMBEA “automatically“ 2020 BILA KURA ZA MAONI hizi ni propaganda zilizoandaliwa mahususi kuzima “vugu vugu“ la mbadala wa JPM

Wafanyabiashara,Wakuu wa mashirika ya umma na watumishi ktk nafasi nyeti wanaohisiwa ni “Watu wa Kachero” wanashughulikiwa kiaina ili kupunguza nguvu ya uungwaji mkono wa “Kachero” ndani ya Chama.

Mkulu anajua wazi kuwa atakuwa na wakati mgumu hapo mbeleni kwa kuwa hata moja ya familia ya Rais mmoja mstaafu “imejiapiza” kumfanya Rais wa muhula wa mmoja (one term president) kwa gharama yoyote na familia hii ina nguvu ndani ya chama na inatajwa kuwa na uhusiano na“Kachero”,hivyo mkulu baada ya kuona upepo unamwendea vibaya amefanya uteuzi wa mmoja wa familia hiyo ili kupunguza “munkari” wa kudhibitiwa,duru zinaonesha kuwa Baraza litapanguliwa ili mmoja wa wana familia kukalia moja ya wizara,ingawa bado hilo haliondoi “kiapo“ cha kuhakikisha kigingi kinawekwa kumzuia 2020

Wazee chamani wananena kwa sauti ya chini ili chama kipone lazima “Kachero” akalie “kiti cha enzi” kwa kuwa wanaona eti ana busara kuliko yule waliyempigania kwa jasho na damu na sasa wanadhihakiwa na watu wake waliokalia “viti vya enzi”naye,ingawa hawakumpigania yaani wanavuna wasichopanda,Katika kile Nape Nnauye alichokisema,“Wakati sisi tunaumia katika kutafuta KURA za CCM huko vijijini wengine walikua wanakunywa BIA Bar” hii inadhirisha kuwa kuna “Opportunist” wanaofaidi kuku kwa mrija na hali hawakupigania Chama.

Kisiasa hii ina afya kwa kua inamkosesha usingizi mkulu na angalau itamfanya aweze ku “behave” akijua fika hicho kiti ni cha moto kesho na kesho kutwa anaweza kalia mwingine

Hofu ya wafia chama ni kuwa juhudi zisipotumika chama kinaweza kikazama katika tope na kupata mkwamo wa kudumu jambo ambalo wafia chama hawataki kitokee kwa kua wanajua fika itawagharimu pakubwa kukirejesha katika mstari kwa kuwa kila kona ni malalamiko yanayoashiria uungwaji mkono haupo miongoni mwa walio wengi.

Wanaomfahamu Kachero Membe wanadai ni mtu aliyekaa magogoni kwa kipindi kirefu kama “Kachero” si wa kupuuzwa na ukimya una mshindo mkuu utakaohanikizwa na Hali ya kukosa dira ya awamu ya tano ambapo hata sasa kuna mkwamo mkubwa huku tukishuhudia sakata kadhaa zikitafuna serikali kuanzia “Uteuzi wa upendeleo wa ukabila na ukanda,Visasi kwa wafanyabiashara wakubwa,Ubadhirifu wenye sura ya kudhibiti vyombo vya habari kuripoti ukweki na uhalisia,“ACACIA na MAKINIKIA“ na sasa Sakata la fidia ya “BOMBADIER Q400 huko Canada

Je, Lumumba patakalika ama mambo yatakua tafarani zaidi ya 2015,tusubiri muda ni mwalimu mzuri...!!!@yale mabwabwa ya lumumba yata coment ujinga.

C&P from FB

My take;
J
ee hii yaweza kuwa ndio sababu ya kiwewe kingi cha mzee na kuwa na maamuzi ya kushangaza? imani imemuishia kwa wale walio mzunguka?
Na jee style hii ya hasira na chuki inamsaidia kuwakomoa wapinzani wake wa ndani ya chama na nje au ndio inazidi kumharibia?
CC kwa Balozi Mombo
CC kwa Balozi Nchimbi
 
Chakaza

Hizi ni fikra zangu juu ya JPM na CCM.

Hana uzoefu wa kuongoza chama cha siasa kama CCM, achilia mbali TADEA. Mambo makubwa matatu yanamsumbua kuhusu CCM.

Kwanza ni uwezo wa kuwa na ushawishi na kumudu nafasi ya uenyekiti bila kutumia nguvu. Hakujiandaa kuwa mwenyekiti. Unapokuwa mwanaCCM unayegombania nafasi ya uRais tayari unakua umeandaa katibu mkuu wako, makamu, uenezi, n.k. Tayari unajiandaa kuwa mwenyekiti wa chama.

JPM hakujiandaa kwenye hili. Uenyekiti umemkuta na sasa hajui yupi amuweke wapi na yupi amtupe. Huyo atakayemtupa, je atamfanyia fitna?

Mwisho wa siku anakosa ushawishi na kubakia na kina Bashite, Polepole, na kaliba hiyo ambayo haina ushawishi ndani ya chama zaidi ya kuonekana vituko.

JPM kwa sababu ana hofu na hana imani na wanaCCM kuhofia kumzunguka amebakiza silaha moja tu kuimarisha uenyekiti wake - Dola.

Kwa sasa CCM ipo chini ya dola si juu ya dola kama zamani ambapo katibu mkuu au mjumbe wa NEC ana nguvu kuliko Kamanda Siro. Meza imegeuka na wanaCCM wamekuwa wapole na hawana furaha ukiacha wale wanaokula sasa.

Pili muundo wa serikali ulioasisiwa na Nyerere umeifanya CCM kuwa kubwa kuliko nchi. Katika uteuzi wowote ule idara zote muhimu lazima zishikwe na chama na si mtu mwingine.

Enzi hizo CCM ndiyo Tanzania, sasa Tanzania ndiyo CCM-Mwenyekiti.

Tofauti ni kwamba CCM ndiyo walitoa viongozi wa idara zote muhimu. Sasa idara muhimu zinapewa watu wasiokuwa hata na uCCM lakini wanapaswa kuiabudu CCM-Mwenyekiti. WanaCCM wanaona wanabaguliwa kwa kulishwa makombo ya teuzi.

Tatu na mwisho ni hofu juu ya upinzani hususani CHADEMA. Iwapo CHADEMA hakitaishiwa nguvu mpaka 2020 kitampa shida JPM.

Shida ni Lowassa mwingine kujitoa kwenye chama. Kama Lowassa ametoka na sisi tuliobaki hatuoni faida ya kuwa CCM kwa nini tubaki?

Hivyo ni "hekima" na "busara" kwa Mwenyekiti kutumia nguvu kuua upinzani ili iwapo kuna mwanaCCM mwenye ushawishi atakapotaka kutoka akose pakwenda.

Kwa hiyo leo ikionekana Membe ni tishio ataandamwa na kufanywa mfano ili mwingine asiige. Tanzania iwe CCM-Mwenyekiti kwa kupenda au la!

Kuna kiza mbele.

cc JokaKuu Mchambuzi Mag3
 
Usicheze na nguvu ya Rais. Kile kiti mtu akishakaa pale ndio ameshakaa, anakula miaka 10 yake. Mtu ana state apparatus zote unamzuia vipi ndani ya Chama asipite 2020. Huyo Kachero anaweza kuwekwa house arrest mpaka uchaguzi ukapita 2020nna hakuna cha kufanya zaidi tutasikia tetesi kwenye Magazeti na kwa Mange kimambi basi. Labda wapinzani wa nje ila sio wa ndani ya Chama.
 
Kweli, ingawa nae ngosha kawaamisha wengi sana waliopo ikulu kawapeleka huko mikoani, nae anajua kwenye system kuna watu wa watu ndio maana ana tibua tibua
System ni system tu hawawezi kuona nchi yao inaharibika wakakubali iharibike haiwezekani. Muhimu na kubwa kuliko yote ni ustawi wa nchi yetu akionekana mmoja anaharibu misingi aliyeweka nyerere asemwe mpaka asimame kwenye msitari sahihi
 
mwanzoni mwa utawala wake Mkuu alikuwa na sapoti fln kutoka kwa wapinzani na umma kuliko hata ccm yenyewe, kwa u -turn aliyoipiga anabaki no man's land!
 
mwanzoni mwa utawala wake Mkuu alikuwa na sapoti fln kutoka kwa wapinzani na umma kuliko hata ccm yenyewe, kwa u -turn aliyoipiga anabaki no man's land!
 
Wale waliomo ndani ya viroba wametambuliwa jamani?..nauliza nimeamka usingizini tu.

Habeeb Marhan
 
Mtoa mada umejitahidi kuuchimba ukweli uliyokatika kisiwa kisichofikika. Kuna mengi yanayoendelea ktk harakati za kumtoa aliyepo kitini. Kachero anacheza kwa nafasi yake lakini pia wale wengine hawajazima mitambo Yao pia.
Kwa ufupi tu, mkulu amezungukwa na maadui kila kona. Hili analijua fika na ndo maana kuna wakati anajikuta akipiga kampeni kwenye ziara za uongozi.
Mwaka 2019, utakuwa mwaka wenye pilikapilika nyingi za kisiasa ndani ya chama kikongwe cha Tanzania, pilikapilika hizi zitaendana na kuchafuana. Aliyeshika mpini amejiandaa vyema kutumia nafasi yake kudhoofisha wote waliojitokeza kutoa ushindani msimu uliopita na kwa hakika hata hawa wachache waliobaki kwenye teuzi, watalia na kusaga meno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Membe mwizi tu na fisadi hana lolote wala hana mbinu km tunavyojiaminisha

MTU hatar ccm alikuwa ni mzee lowasa tu

Hata kikwete sio mzee wa mipango km lowasa

Membe hana mbinu yeyote hata km angehudumu usalama wa taifa miaka mia

Magu nae atakuwa wa hovyo km ataruhusu kuyumbishwa na membe

Japo magufuli na membe wote ni viongoz wabovu

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
kwa magufuli kila goti litapigwa wakuu. kama kuna mtu amekaa mkao anajidanganya kwamba atampinga 2020 ajue ataishia kama anavyoishia Mr. zero sasa hivi.
 
Huyu alieleta thread hii naona kama bado anajidanganya...mkuu mfarakano uliotokea 2015 hauji kutokea tena kamwe katika chama hichi subirin 2020 mchapwe tena

Sent using Jamii Forums mobile app


wewe unona ni mfarakano tu... wa watu wawili..

ukweli mwenyekiti wa ccm alikuwa hajajiandaa kuongoza chama... sasa ndani ya chama upo mgongano wa kimaslahi maana wapo wanao athirika na utendaji wa mkuu name wananguvu ndani ya chama... pia wapo wanaomkubali mwenyekiti...
 
Nimeona picha polepole ndio kampokea Naibu Balozi wa Marekani. Kiprotocal balozi ni mtu mkubwa sana nilitegemea akutane na Katibu mkuu kama hayupo basi makatibu wakuu wasaidizi/naibu mmojawapo angekutana nae.

Badala yake kakutana na mtu wa propaganda kwa lugha nyepesi Pole pole ndio Ag. KM.

Swali la kujiulize katibu mkuu yupo wapi? Naibu katibu mkuu bara au visiwani wko wapi?

I guess kuna shida ndio maana hawapo
 
Back
Top Bottom