"Kachero" na Hatima ya CCM 2020

Another rubish. Ccm ilikuwa na Hali mbaya kipindi ya Lowasa, haitatokeaga awamu hii

Mkuu inawezekana kabisa hali ikawa mbaya 2020.
Membe amehamia Ukawa na anamuunga mkono Lowassa, Jk naye anatangaza kumuunga mkono EL chini ya ukawa, CCM itakuwa na hali mbaya kuliko 2015.

Ukumbuke CCM wanategemea sana fitina na itifaki ambazo hawa wa sasa hawaziwezi na waliopo wanaoziweza wamenuna na baadala yake watakuwa upande wa fitina za kubomoa na si kujenga..
 
Na Dr. Musa Leonard Mdede

BENARD CAMILLIUS MEMBE : “Kachero“ anayemtesa JPM sirini

Akiwa na Uzoefu wa kufanya kazi ya “ukachero” katika Ikulu ya magogoni takribani miaka kumi (1978 - 1989 ) na mwanadiplomasia aliyehudumu katika ubalozi wa Tanzania jijini Ottawa,Canada kati mwaka (1992 - 2000) kabla ya kurejea nchini na kuhudumu kama mbunge wa mtama kwa miaka 15 (2000 - 2015 ) na na Naibu waziri wa Makazi,Nishati na Madini na baadaye Waziri wa Mambi ya Nje na Uhusiano wa kimataifa

Duru za kisiasa kutoka “corridor” za Lumumba yalipo makao makuu madogo ya CCM jijini Dar es Salaam zinadokeza kuwa hamkani mambo si shwari chamani.KACHERO Membe hayuko kimya kama wengi wanavyodhani bali yupo kazini kimkakati kuhakikisha 2020 “anakwaa” ugombea ndani ya chama hicho

Si yeye Membe binafsi bali Wazee ndani ya Chama ambao wengi wameamua kukaa kimya na hatuwasikii tena tangu awamu ya tano iingie madarakani na ahadi tele tele ambazo zimegeuka kuwa mithili kusubiri “Ferry” stendi ya Ubungo

Mwaka 2015 mara tu baada ya uchaguzi “Kachero” Membe alipata kuzungumza na wanahabari jijini DSM akikosoa namna mfumo wa “kukurupuka” unaotumika serikali ya awamu ya tano unavoharibu misingi iliyojengwa na watangulizi kama hivi sasa tunaposhuhudia Sakata la “Bombadier” na “ACACIA“

Press ya Membe ilidhihirisha kuwa haungi mkono “ukurupukaji” ambao mpaka sasa unaligharimu Taifa pakubwa.Kwa mara ya pili tena mwanzoni mwa mwaka 2016 Taarifa zilisambaa kupitia mitandao ya kijamii kama atazungumza na wanahabari katika kile kilichoonekana kutokukubaliana na hali ya mambo,ingawa hakuna ajuaye nini kilitokea kwani Press hiyo haikufanyika

Akiwa miongoni mwa tano bora kwa wagombea Urais ndani ya CCM mwaka 2015,Membe baada ya kushindwa kupata nafasi ya “Kupeperusha Bendera” ya CCM alitangaza kustaafu Siasa na kusaidia chama kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,Je,litekeleza ahadi yake hiyo kila mmoja anajua nini kilitokea kampeni za chama tawala 2015.Kwa sasa hali inaonekana kuwa tofauti kwani “wazee“ wamesikika wakisem “Bora tungempa Membe” ingawa wengi wanaongea kwa sauti ya chini kwa hofu ya kushughulikiwa

Upande wa pili,pangua pangua imeanza,kuwaondoa wale wote waliomuunga mkono na wanahofiwa watamuunga mkono wakati ukifika.Pangua pangua hii inaanzia ktk nafasi nyeti serikalini,Baraza la Mawaziri,Wakuu wa mikoa na wilaya na chamani pia ambapo tumeshuhudia baadhi ya mikoa kama Mwanza ambapo watu maalumu wameandaliwa kuwakabili wale wanaoonekana kuwa ni “watu” wa “Kachero Membe” haya ni maagizo yanayotekelezwa kutoka mamlaka ya juu zaidi

Wazee chamani “wanahaha” kukiokoa chama kwa kua wanajua chama kitaweza kupoteza uungwaji mkono katika chaguzi zijazo,ndomaana wengi hawasikiki tangu uchaguzi mkuu maaka 2015 kwani hawaridhishwi na hali ya mambo,kwani imeshuhudiwa baadhi ya nafasi ktk chaguzi ndani ya chama zikikosa wagombea kitu ambacho si cha kawaida kwa chama hicho kikongwe

Propaganda kadhaa za kujihami zimeandaliwa mahususi ili kudhibiti “vugu vugu” la kumkataa “JPM” chamani.JPM BAKI MPAKA 2030,PICHA YA BANGO UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA IKIONESHA JPM Rais(2015 - 2025),JPM ASIPINGWE 2020 CHAMANI & KATIBA YA CHAMA IBADILISHWE JPM AWE MGOMBEA “automatically“ 2020 BILA KURA ZA MAONI hizi ni propaganda zilizoandaliwa mahususi kuzima “vugu vugu“ la mbadala wa JPM

Wafanyabiashara,Wakuu wa mashirika ya umma na watumishi ktk nafasi nyeti wanaohisiwa ni “Watu wa Kachero” wanashughulikiwa kiaina ili kupunguza nguvu ya uungwaji mkono wa “Kachero” ndani ya Chama.

Mkulu anajua wazi kuwa atakuwa na wakati mgumu hapo mbeleni kwa kuwa hata moja ya familia ya Rais mmoja mstaafu “imejiapiza” kumfanya Rais wa muhula wa mmoja (one term president) kwa gharama yoyote na familia hii ina nguvu ndani ya chama na inatajwa kuwa na uhusiano na“Kachero”,hivyo mkulu baada ya kuona upepo unamwendea vibaya amefanya uteuzi wa mmoja wa familia hiyo ili kupunguza “munkari” wa kudhibitiwa,duru zinaonesha kuwa Baraza litapanguliwa ili mmoja wa wana familia kukalia moja ya wizara,ingawa bado hilo haliondoi “kiapo“ cha kuhakikisha kigingi kinawekwa kumzuia 2020

Wazee chamani wananena kwa sauti ya chini ili chama kipone lazima “Kachero” akalie “kiti cha enzi” kwa kuwa wanaona eti ana busara kuliko yule waliyempigania kwa jasho na damu na sasa wanadhihakiwa na watu wake waliokalia “viti vya enzi”naye,ingawa hawakumpigania yaani wanavuna wasichopanda,Katika kile Nape Nnauye alichokisema,“Wakati sisi tunaumia katika kutafuta KURA za CCM huko vijijini wengine walikua wanakunywa BIA Bar” hii inadhirisha kuwa kuna “Opportunist” wanaofaidi kuku kwa mrija na hali hawakupigania Chama.

Kisiasa hii ina afya kwa kua inamkosesha usingizi mkulu na angalau itamfanya aweze ku “behave” akijua fika hicho kiti ni cha moto kesho na kesho kutwa anaweza kalia mwingine

Hofu ya wafia chama ni kuwa juhudi zisipotumika chama kinaweza kikazama katika tope na kupata mkwamo wa kudumu jambo ambalo wafia chama hawataki kitokee kwa kua wanajua fika itawagharimu pakubwa kukirejesha katika mstari kwa kuwa kila kona ni malalamiko yanayoashiria uungwaji mkono haupo miongoni mwa walio wengi.

Wanaomfahamu Kachero Membe wanadai ni mtu aliyekaa magogoni kwa kipindi kirefu kama “Kachero” si wa kupuuzwa na ukimya una mshindo mkuu utakaohanikizwa na Hali ya kukosa dira ya awamu ya tano ambapo hata sasa kuna mkwamo mkubwa huku tukishuhudia sakata kadhaa zikitafuna serikali kuanzia “Uteuzi wa upendeleo wa ukabila na ukanda,Visasi kwa wafanyabiashara wakubwa,Ubadhirifu wenye sura ya kudhibiti vyombo vya habari kuripoti ukweki na uhalisia,“ACACIA na MAKINIKIA“ na sasa Sakata la fidia ya “BOMBADIER Q400 huko Canada

Je, Lumumba patakalika ama mambo yatakua tafarani zaidi ya 2015,tusubiri muda ni mwalimu mzuri...!!!@yale mabwabwa ya lumumba yata coment ujinga.

C&P from FB

My take;
J
ee hii yaweza kuwa ndio sababu ya kiwewe kingi cha mzee na kuwa na maamuzi ya kushangaza? imani imemuishia kwa wale walio mzunguka?
Na jee style hii ya hasira na chuki inamsaidia kuwakomoa wapinzani wake wa ndani ya chama na nje au ndio inazidi kumharibia?

Kumbuka kukaa magogoni sio sifa ya kuwa rais

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna kitu kama hiyo mzee, only in your dreams, dreams that will never occur, forget about it.
 
Siasa bongo ni kwikwi,harakati zimezidi,mlituaminisha jk chama kinamfia asipochaguliwa mamvi lakini wameendelea kutamba, hata huyo Mzee huko ni kama mamluki tu,ila kwa kuwa watanzania mazwazwa na manyumbu wacha watupeleke hakuna namna!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duru za kisiasa kutoka “corridor” za Lumumba yalipo makao makuu madogo ya CCM jijini Dar es Salaam zinadokeza kuwa hamkani mambo si shwari chamani.KACHERO Membe hayuko kimya kama wengi wanavyodhani bali yupo kazini kimkakati kuhakikisha 2020 “anakwaa” ugombea ndani ya chama hicho
Katiba ya CCM ilishabadilishwa jamaa anapita bila kupingwa...au hukumbuki
 
Kumbuka kukaa magogoni sio sifa ya kuwa rais

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tulichoshuhudia hapa ni kuwa watu hawasomi na kuelewa mantiki ya hoja bali wanahemka kulingana na hisia za mapenzi waliyo nayo. Mwandishi hajasema kuwa Membe anafaa kuwa Rais, wala hajasema atashinda.
Mada inazungumzia kuwa ni Kachero anayemtesa magu kuelekea 2020 basi. Anamtesaje? hilo ndio lilikuwa hoja ya kujadili, na kama hata washabiki wake wanateseka hivi basi pengine hata yeye haya ya ajabu afanyayo ni mateso ya hisia zake pia
 
Weraweraaaaaaaaaaaaa! menyewe kwa menyeweeeeeeee! acha wafu wazike wafu wao! sie 2020 njia ya magogoni ileeeeeeeeeeeeee! wera weraaaaaaaaaaaaaa!
 
This is so sweet...

Na Dr. Musa Leonard Mdede

BENARD CAMILLIUS MEMBE : “Kachero“ anayemtesa JPM sirini

Akiwa na Uzoefu wa kufanya kazi ya “ukachero” katika Ikulu ya magogoni takribani miaka kumi (1978 - 1989 ) na mwanadiplomasia aliyehudumu katika ubalozi wa Tanzania jijini Ottawa,Canada kati mwaka (1992 - 2000) kabla ya kurejea nchini na kuhudumu kama mbunge wa mtama kwa miaka 15 (2000 - 2015 ) na na Naibu waziri wa Makazi,Nishati na Madini na baadaye Waziri wa Mambi ya Nje na Uhusiano wa kimataifa

Duru za kisiasa kutoka “corridor” za Lumumba yalipo makao makuu madogo ya CCM jijini Dar es Salaam zinadokeza kuwa hamkani mambo si shwari chamani.KACHERO Membe hayuko kimya kama wengi wanavyodhani bali yupo kazini kimkakati kuhakikisha 2020 “anakwaa” ugombea ndani ya chama hicho

Si yeye Membe binafsi bali Wazee ndani ya Chama ambao wengi wameamua kukaa kimya na hatuwasikii tena tangu awamu ya tano iingie madarakani na ahadi tele tele ambazo zimegeuka kuwa mithili kusubiri “Ferry” stendi ya Ubungo

Mwaka 2015 mara tu baada ya uchaguzi “Kachero” Membe alipata kuzungumza na wanahabari jijini DSM akikosoa namna mfumo wa “kukurupuka” unaotumika serikali ya awamu ya tano unavoharibu misingi iliyojengwa na watangulizi kama hivi sasa tunaposhuhudia Sakata la “Bombadier” na “ACACIA“

Press ya Membe ilidhihirisha kuwa haungi mkono “ukurupukaji” ambao mpaka sasa unaligharimu Taifa pakubwa.Kwa mara ya pili tena mwanzoni mwa mwaka 2016 Taarifa zilisambaa kupitia mitandao ya kijamii kama atazungumza na wanahabari katika kile kilichoonekana kutokukubaliana na hali ya mambo,ingawa hakuna ajuaye nini kilitokea kwani Press hiyo haikufanyika

Akiwa miongoni mwa tano bora kwa wagombea Urais ndani ya CCM mwaka 2015,Membe baada ya kushindwa kupata nafasi ya “Kupeperusha Bendera” ya CCM alitangaza kustaafu Siasa na kusaidia chama kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,Je,litekeleza ahadi yake hiyo kila mmoja anajua nini kilitokea kampeni za chama tawala 2015.Kwa sasa hali inaonekana kuwa tofauti kwani “wazee“ wamesikika wakisem “Bora tungempa Membe” ingawa wengi wanaongea kwa sauti ya chini kwa hofu ya kushughulikiwa

Upande wa pili,pangua pangua imeanza,kuwaondoa wale wote waliomuunga mkono na wanahofiwa watamuunga mkono wakati ukifika.Pangua pangua hii inaanzia ktk nafasi nyeti serikalini,Baraza la Mawaziri,Wakuu wa mikoa na wilaya na chamani pia ambapo tumeshuhudia baadhi ya mikoa kama Mwanza ambapo watu maalumu wameandaliwa kuwakabili wale wanaoonekana kuwa ni “watu” wa “Kachero Membe” haya ni maagizo yanayotekelezwa kutoka mamlaka ya juu zaidi

Wazee chamani “wanahaha” kukiokoa chama kwa kua wanajua chama kitaweza kupoteza uungwaji mkono katika chaguzi zijazo,ndomaana wengi hawasikiki tangu uchaguzi mkuu maaka 2015 kwani hawaridhishwi na hali ya mambo,kwani imeshuhudiwa baadhi ya nafasi ktk chaguzi ndani ya chama zikikosa wagombea kitu ambacho si cha kawaida kwa chama hicho kikongwe

Propaganda kadhaa za kujihami zimeandaliwa mahususi ili kudhibiti “vugu vugu” la kumkataa “JPM” chamani.JPM BAKI MPAKA 2030,PICHA YA BANGO UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA IKIONESHA JPM Rais(2015 - 2025),JPM ASIPINGWE 2020 CHAMANI & KATIBA YA CHAMA IBADILISHWE JPM AWE MGOMBEA “automatically“ 2020 BILA KURA ZA MAONI hizi ni propaganda zilizoandaliwa mahususi kuzima “vugu vugu“ la mbadala wa JPM

Wafanyabiashara,Wakuu wa mashirika ya umma na watumishi ktk nafasi nyeti wanaohisiwa ni “Watu wa Kachero” wanashughulikiwa kiaina ili kupunguza nguvu ya uungwaji mkono wa “Kachero” ndani ya Chama.

Mkulu anajua wazi kuwa atakuwa na wakati mgumu hapo mbeleni kwa kuwa hata moja ya familia ya Rais mmoja mstaafu “imejiapiza” kumfanya Rais wa muhula wa mmoja (one term president) kwa gharama yoyote na familia hii ina nguvu ndani ya chama na inatajwa kuwa na uhusiano na“Kachero”,hivyo mkulu baada ya kuona upepo unamwendea vibaya amefanya uteuzi wa mmoja wa familia hiyo ili kupunguza “munkari” wa kudhibitiwa,duru zinaonesha kuwa Baraza litapanguliwa ili mmoja wa wana familia kukalia moja ya wizara,ingawa bado hilo haliondoi “kiapo“ cha kuhakikisha kigingi kinawekwa kumzuia 2020

Wazee chamani wananena kwa sauti ya chini ili chama kipone lazima “Kachero” akalie “kiti cha enzi” kwa kuwa wanaona eti ana busara kuliko yule waliyempigania kwa jasho na damu na sasa wanadhihakiwa na watu wake waliokalia “viti vya enzi”naye,ingawa hawakumpigania yaani wanavuna wasichopanda,Katika kile Nape Nnauye alichokisema,“Wakati sisi tunaumia katika kutafuta KURA za CCM huko vijijini wengine walikua wanakunywa BIA Bar” hii inadhirisha kuwa kuna “Opportunist” wanaofaidi kuku kwa mrija na hali hawakupigania Chama.

Kisiasa hii ina afya kwa kua inamkosesha usingizi mkulu na angalau itamfanya aweze ku “behave” akijua fika hicho kiti ni cha moto kesho na kesho kutwa anaweza kalia mwingine

Hofu ya wafia chama ni kuwa juhudi zisipotumika chama kinaweza kikazama katika tope na kupata mkwamo wa kudumu jambo ambalo wafia chama hawataki kitokee kwa kua wanajua fika itawagharimu pakubwa kukirejesha katika mstari kwa kuwa kila kona ni malalamiko yanayoashiria uungwaji mkono haupo miongoni mwa walio wengi.

Wanaomfahamu Kachero Membe wanadai ni mtu aliyekaa magogoni kwa kipindi kirefu kama “Kachero” si wa kupuuzwa na ukimya una mshindo mkuu utakaohanikizwa na Hali ya kukosa dira ya awamu ya tano ambapo hata sasa kuna mkwamo mkubwa huku tukishuhudia sakata kadhaa zikitafuna serikali kuanzia “Uteuzi wa upendeleo wa ukabila na ukanda,Visasi kwa wafanyabiashara wakubwa,Ubadhirifu wenye sura ya kudhibiti vyombo vya habari kuripoti ukweki na uhalisia,“ACACIA na MAKINIKIA“ na sasa Sakata la fidia ya “BOMBADIER Q400 huko Canada

Je, Lumumba patakalika ama mambo yatakua tafarani zaidi ya 2015,tusubiri muda ni mwalimu mzuri...!!!@yale mabwabwa ya lumumba yata coment ujinga.

C&P from FB

My take;
J
ee hii yaweza kuwa ndio sababu ya kiwewe kingi cha mzee na kuwa na maamuzi ya kushangaza? imani imemuishia kwa wale walio mzunguka?
Na jee style hii ya hasira na chuki inamsaidia kuwakomoa wapinzani wake wa ndani ya chama na nje au ndio inazidi kumharibia?
 
hakuna,asiyejua kwamba huyo kachero hakupenda pale jina lake lilipo katwa, alishindwa tu kuchukua maamuzi aliyoyachukua mzee.
 
Nimeona picha polepole ndio kampokea Naibu Balozi wa Marekani. Kiprotocal balozi ni mtu mkubwa sana nilitegemea akutane na Katibu mkuu kama hayupo basi makatibu wakuu wasaidizi/naibu mmojawapo angekutana nae.

Badala yake kakutana na mtu wa propaganda kwa lugha nyepesi Pole pole ndio Ag. KM.

Swali la kujiulize katibu mkuu yupo wapi? Naibu katibu mkuu bara au visiwani wko wapi?

I guess kuna shida ndio maana hawapo
 
Hata walie wagalegle, wavimbe wapasuke, ila JPM hadi 2025. Hakuna kama JPM.

Huyo kachero, 2013 alishindwa kutaja mafisadi bungeni alipoulizwa sasa atakuwa na huo ubavu wa kuwa rais. By the way, asidhanie kuwa wasomi na watu tulio makini tumesahau alichokifanya.
 
Back
Top Bottom