Kachanganyikiwa sababu ya utumbo wa mbuzi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kachanganyikiwa sababu ya utumbo wa mbuzi.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by St. Paka Mweusi, Dec 23, 2010.

 1. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,898
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Dunia haiishi vya kushangaza,mwenzenu jana nimepata mgeni mtoto wa kijerumani,na kwa kuwa tulipanga anitembelee nikamwambia nitakupikia chakula cha kiafrika.Na kweli mtoto wa kiume nikapitia kwa mchina nikachukua utumbo wa mbuzi na ndizi matoke.Nikaandaa utumbo kwa ufundi wangu wote, nikaweka vitunguu swaumu,tangawizi,limao,pilipili mbuzi kwa mbali,kitunguu maji,nyanya ya kopo,pilipili hoho na mazagazaga kibao ya kiafrika.Mgeni wangu alipofika nikamkaribisha na alifurahia akasema tangu azaliwe hajawahi kula chakula kitamu kama hicho na ameniomba akanitambulishe kwa wazazi wake kama mchumba mwenye sifa ya upishi.Sasa wandugu naombeni ushauri nikubali kutambulishwa au huo ndio utakuwa mwanzo wa kugeuzwa hausi boi.
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mimi sikushauri chochote ila kitendo cha yeye KUOMBA kimenifurahisha muno. Wewe nanihiii lete nyingine......

  Yani mimi nasubiri tu miaka yooote hii niombwe ila wapi?
   
 3. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Yaani huyo binti wa kizungu kadata na thupu ya utumbo tu au kuna mengineyo ulimpatia?
   
 4. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,898
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145


  Ni hiyohiyo supu hakuna kingine mkuu.
   
 5. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,898
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145  Mkuu naomba upate nyingine kwa bili yangu,umenifurahisha sana maana hilo la bahati nilikuwa sijaliangalia.
   
 6. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kala utumbo mchicha tangawizi kaomba akutambulishe kabla sija kushauri nikuulize vp MTAMU?
   
 7. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #7
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Wewe Pm bwana acha kutuzuga hapa mpaka mnakubaliana aje kukutembela mlikuwa mmetongozana au??? Hapa kuna walakini iweje aje kukutembelea tu thena ale utumbo azuke tu akakutambulishe home kwao??? Kuna kitu hakijakaa sawa hapa kuwa wazi
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  twende wote basi...
   
 9. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  kaka jiandae!
   
 10. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,898
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Sijamuonja bado,hivyo sijui kama ni mtamu au mchungu.
   
 11. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Onja kwanza kabla hujakubali kutambulishwa, Isije kuwa nama. wana ng'ang'ania hao!!
   
 12. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mkuu kubali mana upishi hobi yako
   
 13. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  D, Hili nalo neno
   
 14. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,898
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145  Mama, kwani nakuzuga vipi tena,wenzetu hawana kawaida ya kuficha yaliyo mioyoni mwao,akipenda kitu anakueleza hapohapo na ukweli ni kuwa sikuwa nimemtongoza ila nilikuwa na mpango huo.
   
 15. NILHAM RASHED

  NILHAM RASHED JF-Expert Member

  #15
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka we utakuwa house boy tu..wallah nakuapilia..
   
 16. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #16
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,898
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Twende wote wapi?Sihitaji mkalimani.
   
 17. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #17
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,898
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Uhausiboi hapana, ila amesema kama ninataka baba yake ataniajiri kwenye ng`ombe wao.
   
 18. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #18
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,898
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145

  Nitaufikiria ushauri huu.
   
 19. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Mhh Mega kwanza tunda, ndio mambo ya kutambulishana yafwate...Utauziwa mbuzi kwenye gunia shauri yako!!!
   
 20. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,898
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145  Mh,mapenzi gani hayo ya kupikiana?
   
Loading...