Wachina walitumia kondom za utumbo Kondom ya Utumbo wa Nguruwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachina walitumia kondom za utumbo Kondom ya Utumbo wa Nguruwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by HUNIJUI, Oct 20, 2012.

 1. HUNIJUI

  HUNIJUI JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 1,441
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nani asiyejua Kondom? Nani asiyejua kazi ya Kondom? Lakini unajua kifaa hicho ambacho siku hizo husambazwa bure kilianza lini na wapi? Tarehe yenyewe haifahamiki lakini katika karne ya 15 yaani miaka mia 6 iliyopita kondom zilikuwepo na zilikuwqa zinatumika katika bara la Asia. Miaka mia sita iliyopita Kondom nchini china zilikuwa nizatengenezwa kutumia utumbo au mbuzi au kondoo. Matajiri walikuwa wakitumia Kondom zilizotengenezwa kwa karatasi ya hariri iliyopakwa mafuta. Nako nchini Japan Kondom zilikuwa zikitengenezwa kwa magamba ya kobe au pembe za wanyama . Naama pembe ilikuwa ikivaliwa kama kondom..ni huko Japan, miaka mia 6 iliyopita. Ni katiuka karne iliyopita , mwaka 1900 kondom zilizotengenezwa kwa utumbo wa mbuzi na kondoo hata utumbo wa ngombe zilianza kuenea duniani. Enzi hizo ilikuwa inatumiwa kukinga magonjwa ya zinaa na kuzuia mimbia isiyotakikana. ......... Ni kawaida kwa wanawake wengi wakati wa ujazito kuanza kutapika , kuwa ni kichefu chefu ,kuhisi kisunzi au kizunguzungu , kujisikia mnyonge, hasa wakati wa asubuhi. Wazungu wanasema ni Morning sickness. Wataalam wanasema haina sababu moja. Lakini wanakubali kuwa husababishwa na ongezeko la homoni hasa ya Estrogen katika mwili wa mwanamkea ambayo inaweza kumuongezea , uwezo wa kusikia harufu hasa mbaya. Kuongezeka kwa maji aina ya gastroline. Na unafahamu kuwa mwanamume.Baba mwenye nyumba pia anaweza kuwa na dalili hizo hizo za ujauzito yaani ?, kizunguzungu,kutapika , kichef chefu , tumbo kufura na kuwa na hasira kama mkewe? Kwa wakati huu Mike Dowdall , bwana mwenye umri wa miaka 25 kutoka Manchester Uingereza amefura tumbo, anatapika tapika , asubuhi, husikia kisunzi au kizunguzungu na anapenda kula vitu vichachu kama maembe mabichi yalitiwa chumvi au pilipili. Kwa wakati huu mpenzi wake Amanda Bennett ni mjamzito. Dahili za Mike zilipoanza bi Amanada alichukulia kwamba mpenzi wake ambaye wameishia naye miaka mitatu anamfanyia mzaha au stihizai Eti anamuiga vile anavyo tapika, na kupenda kula kula. Lakini madaktari kutoka Manchster wanasema Bwana Mike ana ugonjwa wa mimba bandia. Wao wanaita Couvade syndrome huu sio uchawi , bali ni ugonjwa unaoweza kuwapata wanaume. Tumbo kufura, kutapika tapika asubuhi, kuhisi kizunguzungu na kupenda kula maembe ya liotiwa chumvi au pilipili. Mike amekuwa na uja uzito bandia kwa wiki 33 na kama vile tu akina mama walio na mimba , Mike ameongeza uzani au zaidi ya kila 3 na sasa anajihisi mchovu kila mara, kuumwa na mgongo na kwnda haja ndogo kila mara. Madaktari hao wanasema ugonjwa huu unaweza kusababishwa na ile hali kuwa wasiwasi unaposubiri mkeo kujifungua, au pia kuwa karibu sana na mkeo. Bi Amanda ambaye ana mimba ya wiki zaidi ya 34 sasa analazimika kumsugua mumewe mgongoni na kiunoni kila siku na kumkanda tumbo lake. Habari hizo zimeshamiri katika gazeti la The Sun la uingereza. ...... Si hadithi bali ni kweli kwamba , mtu na mkewe wakiishi kwa zaidi ya miaka 25 huishia kufanana! Asante msikilizaji wa BBC kutoka Tanzania kutukumbusha hao? ukitaka kuthibitisha hilo hebu mwaangalie bibi na babu, ukiwa wewe ni mtum mzima hebu waangalie wazazi wako wote wawili? Mwalimu Nyerere Hebu tazama picha ya Hayati baba wa Taifa wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere na Mama Maria? Unaonaje? Mama Maria Nyerere Lakini kitu gani kinasababisha hali hii ya mtu na mkewe kufanana baada ya kukaa pamoja kwa miaka 25 au zaidi? Waalam wanasema , ikiwa kuna upendo kati yenu, hii itachangia? kwa vile kwa miaka 25 mume na mke hucheka pamoja , kulia pamoja,wakati wa hupata msiba uhuzunika pamoja , wakati wa matatizo na mihangaiko wanakabiliana nayo pamoja michoro hivi vinasaidia kugeuza shepu na sura au uso wa mtu hivyo mume na mkewe huishia kufanana. vyakula pia inasaidia kuwafanya wafanane. kwa vile wamkaa pamoja kwa miaka , mume na mkewe hula vyakula aina moja na kukaa mazingia aina moja hii pia inasaidi kuwafanya wafanane. Ni utafiti uliofanywa na Dr. Zajonc(ZI-onz) akishirikiana na Pamela Adelmann, Sheila Murphy na Paula Niedenthal na kucahpiswha katika jarida la kisayansi la , Motivation and Emotion. .......... Jee unataka kujua utakapozeeka utafanana vipi?. Kazi rahisi sana. Wataalam wakiongozwa na Dr. Zajonc(ZI-onz) wanasema kama wewe nimwanamume hebu muangalie baba mkwe wako, na kama wewe ni mwanamke , muangalie kwa umakini mama mkwe. Urefu unaweza kuwa tofauti lakini sura, utakapozeeka utafanana kama wakwe zako. ......... nani anataka dola milioni 64 bila kutoa jasho jingi? nadhani kazi hii itakuwa nyepesi mno kwa jamaa wa Bongo Tanzania, au Mombasa, au Uganda mtuweza?. Tajiri mmoja nchini Hong Kong ametoa zawadi ya dola milioni 64 za kimarekani kwa mtu yeyote atakaye faulu kumtongoza binti yake bi Gigi Chao na akubali kuolewa nae. tatizo ni hili bi Chao ni msango, au lesbian mwanamkea nayependelea kufanya mapenzi ya jinsia moja. tatizo jengine ni kuwa bi Chao mwenye umri wa miaka 33 tayari amefunga ndoa kisiri na mwanamke mwenzake hivi majuzi tu. sasa basi, ukitaka dola hizo milioni 64 za kimarekani mtongoze, Bi chao , ufaulu kumuondoa katika ndoa hiyo na mwanamke mwenzake na uafaulu kumuoa. kama unaweza basi niandike katika facebook, BBC swahili.com nikuunganisha na tajiri huyo wa Hong Kong

  Source: HB MTETEZI ENTERTAINMENTS: Wachina walitumia kondom za utumbo
   
 2. HUNIJUI

  HUNIJUI JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 1,441
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hao ndo wachina
   
 3. HUNIJUI

  HUNIJUI JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 1,441
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sipati picha kama wanakutana na watu wenye Dini yenye imani tofauti na hawa Wadudu
   
 4. sabasita

  sabasita JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  habari iko mixed mpaka basi
   
 5. Mogambi

  Mogambi Member

  #5
  Oct 21, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Sishangai, maasai vijijini hutumia mifuko laini ya rambo!
   
 6. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Mara kondomu, mara mimba sijapata lengo lako halisi.
   
 7. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,084
  Likes Received: 601
  Trophy Points: 280
  hujasomeka, udaku zaidi umejiri hapo
   
 8. f

  filonos JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  haya pia siku shangaa MAKABILA fulani huzifua na kaazimana CONDOM hayopia ni maendeleo..ya uchumi..
   
 9. n

  nummy JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 589
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwani kondomu ni nini na inatumika kufanyia kazi gani?
   
Loading...