Kabla hata ya uchaguzi mkuu ufanyika tumeanza kuona madhaifu ya wapinzani?

SOPINTO

Member
Oct 19, 2020
7
45
Zikiwa zimebaki siku chache tu za kupiga kura za uchaguzi wa Urais , Ubunge na Udiwani , tayari tumeisha anza kusikia mgongano wa vyama vya upinzani.

Ni kama vile watoto yatima , Maalim Seif anamshangaa Mgombea Urais wa chama chake upande wa JMt kuwa kwanini anapiga kampeni za kugombea Urais wakati walishakubaliana kuwa wanamuunga mkono mgombea urais wa chama cha CHADEMA

Wakati huo huo mgombea kupitia ACT Wazalendo anasema kumuunga mkono mgombea Urais mwezako kisheria haikubaliki. Wananchi wanafanywa mazwazwa

Sasa sijui hizi siasa au mipasho?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom