Kabila la Waswahili (Wangozi)

Kabila la Waswahili (Wangozi)

Jumbe Kondo

Senior Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
109
Reaction score
68
Kumekuwa na tetesi kubwa kama kweli kuna kabila la watu waitwao Waswahili au kwa jina lao la jadi (Wangozi).
Wengi wamekuwa wakipinga. Lakini swali langu hili - Je kunaweza tokea lugha bila ya watu wazawa?
Je, Kiswahili ni mchanganyiko wa malugha ama ni lugha ya jadi ambayo imechukua maneno kutoka pengine?
Nakubaliana na kauli ya pili. Kiswahili na Waswahili walikwepo tangu jadi wakiishi maeneo ya Lamu, Tana ( zote Kenya) na Kismayu ( kusini mwa Somalia) pamoja na wenzao Wamijikenda.
Baadaye wakazagaa pwani yote na kuingia Kwale, Shimoni, Pemba, Unguja, Ngazija, Tanga, Bagamoyo, Kilwa, Mwani ( Msumbiji) n.k.
Ukitaka kujua juu ya watu fulani, waulize mbari zao...na hapo ndio utang'amua kama kweli au rongo.

Hizi ndio mbari za Waswahili kwa wale wanaosema hakuna kabila la Wangozi (Waswahili).
Je wayaona yale majina ya ghuba hapa? Akina Al ndizi bin paipai ibn embe?
Sasa aje fulani kutuambia eti Waswahili na Kiswahili kilianzia Masahariki ya Kati na Bara Asia wakati twajua ni WaMijikenda na makabila mengine ya KiBantu ya mwambao wa Pwani ya Afrika mashariki ndio waliowazaa ndu'zetu hawa.


1. MBARI ZA WAKILINDINI

Mbari ya Mwinyi Nguti wa Mwinyi Mwinzagu
" Mwinyi Humzi
" Mwinyi Kombo wa Dani
" Mwinyi Kae wa Pembe
" Mwinyi Hudumzi



2. MBARI ZA WATANGANA

Mbari ya Mwinyi Muli
" Mwinyi Mjaka
" Mwinyi Umbwi
" Mwinyi Ngwisa


3. MBARI ZA WACHANGAMWE

Mbari ya Mwinyi Kitue
" Mwinyi Mgosi
" Mwinyi Mfaki
" Mwinyi Koba
" Mwinyi Ngovo


4. MBARI ZA WAMVITA

Mbari ya Mwinyi Kutani
" Mwinyi Kae
" Mwinyi Hunziali


5. MBARI ZA WAMALINDI

Mbari ya Banu Shasha
" Banu Mbwana


6. MBARI ZA WAJOMVU (au WAJUNDA)

Mbari ya Mwinyi Faki
" Mwinyi Chande wa Shamaniya
" Mwinyi Usi Muhija
" Mwinyi Uledi wa Ndau
" Mwinyi Jaa wa Mwinyi Nguti


7. MBARI ZA WAMTWAPA

Mbari ya Mwinyi Nyali (au Mbari ya Ng'ombeni)
" Mwinyi Jimve
" Mwinyi Goziadi
" Mwinyi Rakwe
" Banu Muyaka
" Banu Shemapwe

8. MBARI ZA WAKILIFI

Mbari ya Mwinyi Shoka
" Mwinyi Kiwanda
" Mwinyi Mkomati
" Mwinyi Gome


9. MBARI ZA WAPATE

Mbari ya Wa-Pate
" Wa-Amu
" Wa-Kitau
" Wa-Twaka
" Wa-Tikuu
" Wa-Kipungani
" Wa-Barawa
" Wa-Shela

10. MBARI ZA WAGUNYA (au WABAJUNI)

Mbari ya Washaka
" Wa-Uziwa
" Wa-Ungama
" Wa-Ozi
" Wa-Sada
 
Sasa Wapemba, WaTanga, WaBagamoyo, WaKilwa, WaMafia na Wazanzibari pia watupe mbari zao.
 
Jahazi la Ziwa, kwanza shikamoo!

Ahsante kwa maelezo kuntu uliyotuwekea hapa. Mjadala wa Uafrika wa Kiswahili ni kwa ajili ya wasiotafiti na wanaopenda kushikilia kile walichokisikia mara ya kwanza. Jina lililochaguliwa na msamiati uliosanifishwa kutoka Unguja ndio ulioleta kadhia yote hii.

Mwalimu wangu Mussa Muhamed wa Chuo Kikuu Dar es Salaam aliwahi kuniambia kuwa mtazamo sahihi wa Kiswahili ni kupitia lahaja zake, ambazo miongoni mwazo zipo ambazo hazijawahi kabisa kupata athari ya lugha ziso za Kibantu, mfano Kimakunduchi.

Kingine ni kuwa lugha zilizoathiriana sana huwa zinaelekeana kwa kiwango kikubwa, na hupishana kwenye matamshi, msamiati usio wa msingi na vipengele vingine vidogo. Ndio maana wasemaji wa lugha hizi huelewana, kinyume na uhusiano kati ya Kiarabu/Kiingereza/Kireno na Kiswahili.

Nitarudi!
 
Last edited by a moderator:
Kiswahili ni lugha miongoni mwa lugha za Kibantu.

Tamko hili la Kiswahili linatokana nalugha ya Kiarabu nalo ni sahil maana yake Pwani au Mwambao Je, jina hili ambalo limetokanana lugha ya Kiarabu, wao wenyewe Wa-Bantu walikuwa hawana jina la kujiita katika lugha yao?

Jawabu laa! Lilikuwepo, nalo ni Wangozi na lugha yao Kingozi Wangozi ina maana yakabila, kama makabila mengine katika ulimwengu.

Waandishi wengi wameandika juu yaWaswahili na wanamapisi ya mapokezi walioeleza kwamba kabila kuitwa Wangozi ni kuwamatumizi makubwa yao walikitumia ngozi, viriba vya maji, viriba vya kuvugutia moto kwawahunzi au wafua chuma, kitapa cha kuchotea maji, viatu, kanda, nyuo za panga na visu hatakanda za kupimia ardhi na kadhalika Wangozi si kwamba walitumia ngozi kuwa walikuwa niwawindaji au ni wafugaji na ndipo wakaitwa Wangozi.

Kwa wanamapisi waandishi hawakubali wanamapisi mapokezi, na ni jambo la kusikitisha kuwa wana fikra hiyo, wakizingatia hila mapokezi uandishi walipata maelezo kwa wanamapisi mapokezi ndipo wakaweza kuandikamapisi na mambo mengineo, wanamapisi maan.dishi v;anataka ushabidi ili waamini kwamaandishi, kuwa asili ya Waswahili ni Wangozi, ushahidi uliopo ni kwamba lugha ya Kiswahili cha zamani kinajulikana kwa jina la Kingozi na washairi wengi walijua jina hili kuitwa tungo zazamani zimeandikwa kwa Kingozi.

Majina ya makabila au miji yabadilika kwa mabadiliko ya mazingira au mapisi si jambo jipyakwa kuandikwa majina kulingana na jambo fulani au kitu fulani, kwa mfano si Wangozi pekeyao, hata, makabila mengine, yana majina ya mito, miti na kadhalika Na pia tukizingatia kabilaau jina ni utambulisho wa kikundi au mtu kwa sababu hiyo ndio kila kikundi kikajulikana kwajina lake, na tafimti ya baina ya kabila na kabila ni lugha, ndio inapambanua kabila hii kwa ile MAPIS! YA KISWAHILI 105Katika ulimwengu kuna lugha nyingi Kwa hizo lugha ndio kupatikana makundi mbali mbali,makundi hayo ndio hizo kabilaIamko Mswahili au Kiswahili lina maana mawili, kwa mapokezi:

Ni kwamba Waarabubwalipokuja wakawakuta wenyeji wa pwani au mwambao, waliwaita 'watu wa mwambao' kwaKiarabu sahil na kubadilika mpaka kuwa Swahili Maana ya pili ni kwamba walipokujabWaarabu wakawakuta wenyeji, wakauliza nyinyi ni watu wa kutoka wapi? Wenyeji wakajibu, sisi ni watu 'wa siwa hili' Katika lugha tuna masiwa na siwa, tuna visiwa na kisiwa Hapa nikwa msomi mwenyewe kuyalinganisha maneno au matamko haya mawili ni lipi lililolekea.

Shehe Nabhani - Mapisi Ya Kiswahili
 
Kiswahili Wastani - Kingozi
asali - uki
ndege - nyuni
chumvi - munyu
kidole - chanda
 
Shukrani kwa elimu...uliyotoa. Ila nina swali, nini maana ya neno " Mwinyi..".? Katika kabila la waluguru kuna hii salamu inayohusu mwinyi. Mfano..A. Hali gani? B. Njema..A. Mwinyi....B. Mngwana...Shikamoo...A. Marhaba. Sasa maana yake mwinyi nini?
 
Halafu majina kama KOBA, Mjaka au Jaka, Chande...hutumika sana miongoni mwa jamii za waluguru/ wazaramo. Je nao ni waswahili?
 
Makabila ya Pwani asili zao pamoja na hata mbari hufanana wakati fulani..wacha hata majina. Hata Shona Wazimbabwe wana majina mengi sawia na Wamijikenda. WaBantu wengi walifanya kuwaacha wenzao nyuma wakihama kwingineko. Majina hayapotei
 
Makabila ya Pwani asili zao pamoja na hata mbari hufanana wakati fulani..wacha hata majina. Hata Shona Wazimbabwe wana majina mengi sawia na Wamijikenda. WaBantu wengi walifanya kuwaacha wenzao nyuma wakihama kwingineko. Majina hayapotei
Okay.. Nimekupata mkuu, ahsante sana kwa ufafanuzi. Ila swali langu hili neno mwinyi huwa nalisikia sana nyumbani na huwa sifahamu maanake. Mfano, Mwinyi- Mvua, Mwinyi- Goha....ss maana ya mwinyi ni nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom