Kabila amuangukia Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kabila amuangukia Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Na Jabir Idrissa - Imechapwa 26 October 2011

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]


  BALOZI wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) ameshindwa kuthibitisha iwapo nchi yake imeomba majeshi kutoka Tanzania.Katika mahojiano na MwanaHALISI, Balozi Alfany Mpango alisema juzi Jumatatu, jijini Dar es Salaam, "Habari hizo sijui mimi."

  Mpango ambaye anaongea Kiswahili katika lafudhi ya Kikongomani alimwambia mwandishi wa habari hizi, kwa sauti ya upole, kwamba yeye hajui lolote juu ya serikali yake kuomba msaada wa majeshi kutoka Tanzania.Gazeti la l'Oeil du Patriote (Jicho la Mzalendo) ambalo hutolewa mjini Paris, Ufaransa, limedai kwamba katika kukabiliana na tishio la kung'olewa madarakani, Rais Joseph Kabila ameomba majeshi kutoka Tanzania na Korea Kaskazini ili kumlinda.

  Kwa mujibu wa gazeti hilo la kila wiki, toleo la wiki ya pili ya mwezi huu, tayari askari wa Tanzania wameingia mjini Kinshasa kuimarisha ulinzi wa Rais Kabila na kwamba "wataingia uwanja wa mapambano pale mambo yatakapomwendea kombo."Lakini ofisa wa ngazi ya juu katika wizara ya mambo ya nje ameliambia gazeti hili jana kuwa hana taarifa kuhusu suala hilo.Alipong'ang'aniwa alisema,"Mh, taarifa hizi kwa kweli sizijui. Nitakuwa kikaoni si muda mrefu.

  Nitauliza wenzangu…Nitakujulisha." Hakupatikana hata alipoitwa tena na tena.
  Taarifa zilizoenea katika nchi za Maziwa Makuu kuhusu hali kuelekea uchaguzi nchini DRC, zinasema "Kabila maji ya shingo.

  "
  Mwezi ujao, Kongo-DRC inafanya uchaguzi mkuu wa pili tangu Rais Kabila amrithi baba yake, Laurent Kabila, aliyeuawa kwa kupigwa risasi na mmoja wa walioitwa "dogodogo" wa jeshi lake.

  Jeshi la Kabila lililouondoa utawala wa Mobutu, lilikuwa na askari wa umri mdogo walioitwa "dogodogo."Naye Kanali Kapambala Mgawe wa makao makuu ya jeshi ambaye gazeti liliambiwa ni msemaji wa jeshi, amesema suala hilo "litakuwa ngazi ya kitaifa."Mwandishi: Ngazi ya kitaifa ndio wapi?

  Au kwa Waziri wa Ulinzi?
  Kanali: Huko ni kwa rais.Mwandishi: Lakini inaweza kuwa maombi yameanzia kwenu au angalau mnajua jambo hili?

  Kanali: Vyovyote vile lakini kama nilivyokwambia, hilo litakuwa ngazi ya kitaifa. Hayawezi kuja kwetu. Ndio hivyo ndugu yangu. Asante.Gazeti lilishindwa kumpata waziri wa ulinzi, Dk. Hussein Mwinyi. Simu yake imekuwa ikisema hapatikani.Mwandishi wa rais, Salva Rweyemamu hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hili.

  Simu yake iliita bila kupokelewa. Hata ujumbe ambao ulipelekwa kwa njia ya simu ya mkononi (sms) haukujibiwa.
  Taarifa kutoka Kinshasa zimeeleza kuwa Kabila ameanza kubadilisha marafiki baada ya maswahiba wake wa miaka mingi, Marekani na baadhi ya nchi za Jumuiya ya Ulaya, kumshinikiza kuhakikisha uchaguzi mkuu nchini mwake unakuwa huru na wa haki.

  Marekani na Ulaya wanasema, hawako tayari kushiriki kwenye kuhujumu demokrasia ya Kongo; bali wako tayari kuunga mkono uamuzi wa raia wa nchi hiyo.
  Haijafahamika mara moja kilichosababisha nchi hizo rafiki wa karibu wa Rais Kabila kubadilisha msimamo.Wachambuzi wa mambo wanasema, Marekani na Jumuiya ya Ulaya wamesukumwa na upepo wa mageuzi katika nchi za Mashariki ya Kati.

  Hata hivyo, duru za kisiasa nchini DRC zinasema tofauti na uchaguzi wa mwaka 2006, wapinzani wa Rais Kabila, ni makini sana uchaguzi huu.
  Duru zinataja chama cha Union Democatie Populaire et Sociale (UDPS) na washirika wake, kuwa tayari wamejipanga kuhakikisha Kabila harejei madarakani katika uchaguzi huo.Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja katika kipindi ambacho baadhi ya wananchi wa Kongo-DRC wanahoji uraia wa Rais Kabila.

  Kiongozi huyo aliyeingia madarakani mwaka 1998 baada ya kifo cha Laurent Kabila, si Mkongomani bali ni raia wa Rwanda wa kabila la Kitusi – kwa baba na mama.Baba mzazi wa Joseph Kabila anaitwa Adrien Christofer Kanambe.

  Mama yake halisi anaitwa Macelina.
  Adrien Christofer Kanambe alikuwa na mke aitwaye Macelina Kanambe, mama yake mzazi Joseph "Kabila."Uchunguzi unaonyesha kuwa Laurent Kabila na mkewe Sifa Mahanya ni wazazi wa "kuokoteza" wa Rais Joseph Kabila.

  Gazeti la Jicho la Mzalendo limesema pia kuwa tayari askari wa Korea Kaskazini wametua mjini Kinshasa ili kutoa mafunzo maalum ya kutumia silaha, zikiwamo zile zilizoko nje na mikataba ya kimataifa.

  Gazeti linadai serikali ya Rais Kabila imeagiza shehena ya silaha kutoka Korea Kaskazini. Baadhi yake, limesema zimehifadhiwa kwenye kambi mpya ya kijeshi ya Kingakati.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Haya sasa...
  Mambo haya ndiyo yatakuja kutuletea Al-Shabaab haya!
  Kisa cha Kabila na waasi wake tunakijua?...au tunaingiza tu majeshi kwa ushoga wa watu binafsi?
  Jamani tulishagharimika sana enzi za "Nchitano Zilizo Msitari Wa Mbele Katika Ukombozi Kusini Mwa Africa"...tunataka kurudi huko tena?
  Hakyanani nchi hii maendeleo tutayasikia kwa jirani!
   
 3. bhageshi

  bhageshi JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2011
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 264
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Haya ndio mambo ya kujadili pia katika mchakato wa katiba sio mtu mmoja na uswahiba wake anaamua tu kupeleka vijana wetu msituni eti kumsaidi swahiba wake. hapa mhimili uwepo wa kujadili hali za hatari kama hizi kabla ya kutoa kibali cha kupeleka jeshi letu machafukoni. Wachafuane wao, wafe wapiganaji wetu watuachie yatima na wajane ndani mwetu. Nasema siipendi hali hii ya mtu kuwa na mamlaka rukuki ya kimaamuzi peke yake.
   
 4. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Haya mambo ndio yanaturudisha nyuma kimaendeleo,
  Tuachane kusaidia hao watu sasa, tunatakiwa tusaidie uchumi wetu kukua,
  Wapiganaji hao wanahitajika hapa kwetu, sio Zaire kulinda maslahi ya kijinga
  Kama wananchi wa Kongo DRC wanampenda watampa kura za kutosha kushinda uchaguzi,
  Na kama LA si akubali matokeo aanze upya, kwanza Jose bado chalii sana tu, kwa nini ang'ang'anie madaraka kizamani hivyo?
   
 5. V

  Vonix JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Katiba mpya ndio mpango mzima,kupunguza madaraka ya raisi kama si kuondoa kabisa ili maamuzi mazito yote sharti yapite bungeni.
   
 6. p

  prudence Member

  #6
  Nov 1, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona mna jump to conclusion?kwani raisi wetu amekubali hilo ombi la kabila?
   
 7. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jamani, kama mtu anauwezo kumsaidia mwenzake sijui asipinduliwe kwanini asitumie uwezo huo huo kujisaidia yeye uchumi usimpindue, kwa sababu kupinduliwa yeye kwa kushindwa kuudhibiti uchumi ni aibu zaidi ya Kabila atakavyo pinduliwa...
   
 8. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Tulijitia umbea wa kutaka kumrudisha Obote madarakani na tukajitia kwenye vita ya kujitakia. Idd Amin alikuwa na haki ya kutuchukia na kutuvamia. Sasa tusipoangalia banyamulenge watatuletea balaa
   
 9. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Congo ni sehemu ya Tanzania, na kabila baba alikuwa analindwa na watanzania mpaka alipoondoka mkutanoni Sheraton, Dar. Tuichukue nchi hiyo!... haina mwenyewe.
   
 10. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aliyekuwapo kawekwa na nani? Museveni lazima amalize deni la vita vya kagera, then he can go.
   
 11. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Nchi yetu wenyewe inatushinda, sasa tukishaichukua hiyo iweje?
   
 12. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kwa kuwa ni suala na ubakaji wa demokrasia, JK lazima akubali tu. Maana hizo za ubakaji wa demokrasia hapa tz ndiyo zake na ccm yake.
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  We need to be free and help our own people.... after all Tukipeleka wanajeshi nje posho inaenda kwa wakuu wa jeshi na kuhujumu wapiganaji
   
 14. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kuna watu wengine hawajui kua hata kabila Tanzania ndio imemfunda, kumsomesha China na kuhakikisha anakua madarakani. Tukimpa vijana we2 kwa ajili ya kusimamia kuchakachua kura ni kawaida.
   
 15. t

  toby ziegler Senior Member

  #15
  Nov 1, 2011
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Majibu yenu yapo kwenye US diplomatic cables toka Kinshasa kwenda Washington
   
 16. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #16
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Congo+uganda,ni foreign territories za tanzania.
   
 17. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #17
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ulaya na Marekani lazima wamgeuke as amewakaribisha wawekezaji wengi wa toka China
  Cha msingi awaangukie wachina watampiga tafu.
  Ila kama uchaguzi utakuwa wa haki why atumie nguvu kurejea madarakani au anadhani yeye ni mfalme
   
 18. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Mkuu China wanachojali ni kukwapua rasili mali zozote ulizo nazo na wakishakomba kila kitu kikiisha wanatimua kama upepo. Hata leo hii vita itokee Congo itakuwa yale yale ya Libya, China watakaa kando na kuwa mabubu na kuangalia upepo unaenda wapi. Hakuna mnafiki mkubwa kama China
   
 19. T

  Testimony Senior Member

  #19
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kabila alitoa $1M au zaidi, kumsapoti JK kwenye uchaguzi uliopita. si ajabu basi JK nae akatuma tumajeshi ketu kule kwenda kulipa fadhila. si unajua sisi ni waafrika, so kulipa fadhila ndo norms zetu?

  Hususan kwa vile Kabila hana haja na tusenti ambao hata hivyo sisi wenyewe hatuna. Lakini vijana wawili watatu wa kuongeza nguvu, hususan na wale wasioonekana ambao wanauwezo mkubwa wa kucheza na mahesabu ya kura na uchakachuzi tunao wa kutosha na bila shaka hao ndo muhimu zaidi kwa Jo kwa sasa!
   
 20. m

  mharakati JF-Expert Member

  #20
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  sijui kabisa interests za nchii zimelenga wapi haswa katika hili, ila hii inaonyesha wamarekani na ulaya hawapati chao kama zamani kwa kabila, kabila amekua mgumu kidogo kuwapa mikataba ya 95% sasa wanataka aje mwingine.

  Lakini pamoja na haya hatuwezi peleka vijana wetu kama nchi yenye demokrasia na nchi kiongozi katika maziwa makubwa kumlinda mtu asiyetakiwa na wananchi wake eti kwa sababu ni mshikaji binafsi wa rais wetu, hii itatucost baadae Kabila akiondoka na wakaja wengine waliokua wanampinga na itahatarisha maisha ya vijana wetu waliopo Congo wanaopiga piga kazi za hapa na pale kulisha familia zao huku nyumbani.

  Kingine kikubwa nani atalipia vijana ni sisi au Kabila? kama ni yeye basi Tanzania ipeleke majasusi na siyo JWTZ, kama ni sisi tunalipa je tutapata nini kama nchi kabila akishinda/akiendelea kukaa madarakani. huu urafiki hamna siku hizi Afrika hii, ni maslahi mbele
   
Loading...