Kaa Mkao wa Kula,kiongozi wa Nchi Kutekwa akiwa angani: Utabiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaa Mkao wa Kula,kiongozi wa Nchi Kutekwa akiwa angani: Utabiri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Jul 25, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Musa Mkama

  MNAJIMU Mkuu Afrika Mashariki Sheikh Yahya Hussein, ametabiri kuwa kutokea kwa madhara mengi ikiwamo kiongozi mmoja wa nchi za Mashariki ya Afrika kutekwa nyara.

  Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Magomeni jijini Dar es Salaam Sheikh Yahya bila kutaja wala kufafanua alisema kuwa kiongozi huyo atatekwa na kupinduliwa akiwa katika ndege.

  "Natabiri kuwa kutatokea madhara mengi kama vile mitetemeko ya ardhi, mafuriko, hali mbaya ya hewa, migomo , mapinduzi na utovu wa nidhamu wa raia kwa viongozi wao... natabiri kuna kiongozi mmoja wa nchi za mashariki ya kiafrika kutekwa nyara au kuinduliwa akiwa katika ndege,"alisema.

  Alitabiri matukio makubwa yatakayotokea na kuwakumba viongozi kuwa wabunge kufungwa au kufikwa na vifo vya ghafla pamoja na kupata kashfa mbaya na kufukuzwa kazi wakiwa nje.

  Alisema kuwa kutatokea matatizo katika mambo ya Ulinzi na usalama hasa kwa viongozi wakuu wa nchi mabalimbali, waliolala wataamka na kutatokea mabadiliko makubwa katika mambo mbalimbali ya kisiasa kijamii.

  "Nawatahadharisha viongozi wa kisisasa kwamba kila fikra na mawazo lazima yazingatiwe kwa uangalifu au inaweza kuleta mfarakano," alisema na kuongeza kuwa'

  "Upinzani katika vyama vya siasa vinavyoatwala na visivyo tawala kupata nguvu na kutokea mabadiliko makubwa katika vyama hivyo".

  Alitabiri pia kuwa waliolala wataamka bila kuwataja ni kina nani na kwamba kutokana na kuamka huko kutatokea mabadiliko makubwa katika mambo mbalimbali ya kisiasa na kijamii, watu kukumbatia tabia ya kizamani na kukuza mazingira mapya.


  SOURCE: MWANANCHI.
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Wale wenye kumpinga sheikh Yahya katika utabiri wake kwa kudai kwamba he is too general, sasa ndiyo wakati mwafaka wa kumhoji atuambie siku, tarehe na saa ya huyo mkuu wa nchi atakapotekwa nyara akiwa angani kwenye ndege. Pengine aseme Mkuu huyo ni nani na atakuwa kwenye ndege ya shirika gani?!
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huyo jamaa ni shuhsu mkubwa ile mbaya na huwa tayari ameshapenyezewa au kugundua hila hizo kutokana na ushushu wake ,kuna watu wamemsitukia.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  I think he has been watching too many American movies.
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Jul 26, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Specially taggart and police academy...! lol
   
 6. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hopeless prophesy.
   
 7. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mchezo wa Simba na Yanga kachemsha tutamwamini vipi?
   
 8. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Aliwahi kutabiri kwamba Tanzania mwaka 2005 tungepata raisi mwanamke. Baadae alipoulizwa mbona haikuwa hivyo yeye akaibuka na kusema eti hakukosea kwa kuwa Kikwete ana sura ya kike! Kuna kipindi pia alisema kuna kiongozi mzito wa Kongo angepoteza maisha mwaka fulani (sikumbuki). Baadae haikutokea hivyo; alipoulizwa akasema Babu Seya ni kama kiongozi tena muhimu na ametokea Kongo na hivyo basi kufungwa kwake maisha ni sawa na kufariki dunia.

  Huyu ni mzugaji tu, njaa inamsumbua, tumsamehe kwa sababu na yeye anatafuta ugali wake!
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Jul 26, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hivi huyu ni Sheikh kweli au namna gani?
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Lakini si anatabiri tu hakusema ndiyo lazima iwe kweli ati!?
  Mbona TMA wakitabiri mvua kesho yake na kama haikunyesha haisemwi kuwa wamedanganya? Utabiri ni kama 'Bayes Theory' ambao probability ya kutokea kwake lazima iwe karibu na moja. Kwa hiyo utabiri ni chini ya uhakika na kidogo ya ukweli.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mh..Kazee kale Mushrik mkubwa na nashangaa hata wewe ustaadh mzima unakashadadia!

  Sasa what happened to "makafiri wanataka kuizima nuru ya allah" au haka kababu sio kakafiri?
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Just giving a benefit of a doubt kwa shekhe yahaya... Hii labda itatokea ngazija huko au visiwa vya mauritius, madagascar and the likes.... si hizi nchi zetu tano zinazounda huo umoja
   
 13. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Nani mushrik hilo Mw'mungu mwenyewe anajuwa. Kidogo ya ufahamu wangu kuhusu shirk ni kunyan'ganya mamlaka na uweza ya Mw'Mungu muumba na kuyapa kiumbe(kiumbwa). Sasa sheikh Yahya Hussein anachofanya ni kutabiri matukio kama vile idara ya hali ya hewa inavyotabiri kutokea kwa mvua,upepo, mawimbi, vimbunga n.k na siku nyengine wala havitokei. Siwezi kusema na wao, kama Yahya Husein, wanashirk,kwa kuwa ni watabiri tu, uhakika wa kutokea hayo wanayoyatabri anaujuwa Muweza Mw'mungu s.w. Ila hao watabiri kama Yahya Hussein na wenzake, wakijidai wanaweza kujuwa nini kitatokea baadae na kwa uhakika,hapo watakuwa wamekiuka mipaka. Ujuwe elimu ya nyota si kharamu kama itatumika kwa manufaa ya kubinaadamu na maslahi ya dini. Tariq bin Zayd kaupeleka Uislamu Spain(Andalusia) kwa elimu za namna kama hiyo.
  Mw'mungu na mtume wanajuwa zaidi.
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jamani mnategemea nini na mtaalamu wa majini Shekh Yahaya?
   
 15. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Inawezekana usemayo Mkuu na ww hapo ushatabiri kama Yahya Hussein,tofauti ww hukuita "press conference" tu.
  Nilichosema baadae ni kuwa utabiri kama 'Bayes Theorum' ni chini ya uhakika na kidogo ya ukweli.
   
 16. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,219
  Trophy Points: 280
  hakuna utabiri hapo mambo aliyoyasema ni lazima ni kutokea ktk jamii ni muda tu muafaka unapofika ktk hilo jambo kutokea!hakuna jipya hapo!
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,803
  Likes Received: 83,176
  Trophy Points: 280
  Huyu naye! anatafuta soko la utabiri wake kwa nguvu zote! Hajui kusoma alama za nyakati kwamba wengi wameshamshtukia.
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kama ni hivyo basi tuite kazi yake guess work badala ya prophecy. Au unaonaje mkuu? By the way mkuu kuna tofauti kati ya prophesies na forecasts. TMA forecast the whether.
   
 19. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu,utaona kuwa nimewaweka Yahya Hussein na TMA katika kundi moja base on theory of Probability(sinahakika kama Hussein anajiona hivyo), hii ya prophecy it sounds like divinity or a sort of revealition of which God has unintervened-hand in its doings, undoings or redoings.
   
 20. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Anachofanya huyu kibabu ni kinyume na mapenzi ya Mungu. Ni chukizo na dhambi kufanya utabiri au kupiga ramli au kusoma viganja. Na yeyote therefore anayefanya mambo hayo yanawezekana kwa kushirikiana na yule mwovu shetani. Hivyo yeye bondage na lucifer. Nchi yetu haiendelei kwa sababu ya watu kama hawa pamoja na mafisadi hawampendezi Mungu.
   
Loading...