K tano!

K tano!

Mwali

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2011
Posts
7,012
Reaction score
5,613
Kujielewa,
Kujipenda,
Kujithamini,
Kujiamini na
Kujikubali.


Ukiwa na hizo 5K ni moja ya hatua kubwa ya mafanikio
katika kujenga a Strong Personality na utu nafsi wenye ‘Utashi’.
Huna haja ya kutambuliwa iwe kwa kutajwa ama kusifiwa
bila kujali kama ni sifa mbaya ama nzuri ili kujiona kuwa nawe u mtu kati ya watu.

Huna haja ya kila likuhusulo liwe kwa misingi ya kusifiwa, sadikiwa,
chelekewa, chekwa na mengine mengi – ili tu kutambua ufanyalo ni msingi na la haja.
Huna haja ya kumuegemea mwanadamu mwenzio kwa lolote
like lililo kwa misingi ya kukubalika bali tu kwa kujikubali.


Muhimu kuliko yoote, huna haja ya kutafuta Furaha na Amani
toka kwa wengine bali utapata hayo ndani yako mweneywe daima!

Maneno haya yameletwa kwenu toka blog ya AshaDii: 5K's |Kujielewa, Kujipenda, Kujithamini, Kujiamini na Kujikubali… | Food For Thought
Kama ulikua hujaitembelea ndio uende sasa ukapate food for thoughts. 🙂
 
Last edited by a moderator:
hapa bhana, nilistuka kusikia K tano, loh!
 
Haya maneno yanawahusu watu ambao wanaishi maisha ya mtandaoni zaidi.
Akinywa kahawa asha-post instagram kwamba anakunywa kahawa sasa.
Akiambiwa kamethali asha kaweka twitter (with source) watu wajue kua tayari ameambiwa
mara anataka aniite Mwali kwa jina langu la nyumbani, aonekane anajuana na Mwali (celeb flani)
Hawa, hata hapa kwetu wamo! akianzisha thread haichangiwi ananuna au anajichangia mwenyewe!
Sio hivo bana! Enjoy kahawa yako, meditate on your methali, mwache mwali awe Anonymous!
Be you, be happy with who you are, hata kama watu hawajui kua upo. Wewe si unajua mwenyewe?
 
safi sana haswa hapo kwenye kujiamini...
confidence is ur success
 
Mmmhh k 5,kwann usingeweka tittle sifa 5
 
Haya maneno yanawahusu watu ambao wanaishi maisha ya mtandaoni zaidi.
Akinywa kahawa asha-post instagram kwamba anakunywa kahawa sasa.
Akiambiwa kamethali asha kaweka twitter (with source) watu wajue kua tayari ameambiwa
mara anataka aniite Mwali kwa jina langu la nyumbani, aonekane anajuana na Mwali (celeb flani)
Hawa, hata hapa kwetu wamo! akianzisha thread haichangiwi ananuna au anajichangia mwenyewe!
Sio hivo bana! Enjoy kahawa yako, meditate on your methali, mwache mwali awe Anonymous!
Be you, be happy with who you are, hata kama watu hawajui kua upo. Wewe si unajua mwenyewe?

message delivered kwa atakayelalama nimepigwa na jiwe basi ndo huyohuyo limemlenga. Nice message me like it.
 
Anaendelea Da Asha kwa kusema:
Kitendo cha kuchagua marafiki na kutaka kujibadilisha kuwa kama wao uliowachagua kwa makusudio ya kupandikiza ile feeling ya ‘Belonging' na kujiona sawa na marafiki ulio wachagua kwa sababu zozote zile ulizo nazo humaliza kabisa mtu kifikra ya kutambua wewe ni nani… Ukiwa na bahati unaweza kushtuka ukarudi nyuma na kujiachia jinsi ulivyo bila kujifanya… Ili ukipata marafiki upate wale ambao watakuchagua kwa jinsi ulivyo na si jinsi unavyojifanya ulivyo…
Source: Kujifanya usivyo ili tu ukubalike… | Food For Thought
 
Mimi nikajua ni Kikwete, Kabila, Kenyatta, Kaguta na Kagame labda wameunda kaumoja kao.
 
Why not,mi siangalii title tu,naangalia vitu vingi....author pia huwa naangalia
Next time have a lito confidence Mwali

Little confidence kwa sababu gani?
Kwa hiyo hapa hatuongelie five K ama?
 
Mimi nikajua ni Kikwete, Kabila, Kenyatta, Kaguta na Kagame labda wameunda kaumoja kao.

Ukiondoa Kikwete (labda na Kaguta) wengine wote majangili. Peleka ICC
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom