JWTZ Wakanusha taarifa za kuibiwa Kifaru

JWTZ Wakanusha taarifa za kuibiwa Kifaru

Inawezekana hakikuibwa ila kilisahaulika kwa bahati mbaya nje ya nyumba ya mwanakijii mmoja, wakati wakufanya stock wakagundua kimoja kina misi.
Kitakuwa kilienda kufanya nini huko kwa mwanakijiji huyo mmoja? (if that was the case, anyway)
 
Ukisoma ile story ina uhalisia Zaidi kuliko walichokanusha JW, yule mwandishi amemhoji Polisi na amemnukuu Hakimu na jina la Hakimu liko pale, inawezekanaje iwe story ya uongo???
Siku si nyingi atatolewa mtu kucha mimi yangu macho.Bora uandike habari za kumkashifu Lowassa utaheshimika ila hizo zingine.................
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Kama container zinapotea nini kifaru bana, mbona fresh tu acheni kujistukia.
 
JWTZ yakanusha taarifa za kuibwa kwa kifaru, lasema taarifa hizo hazina ukweli, lasisitiza ulinzi katika maeneo ya jeshi uko imara.

Hata hivyo Jeshi hilo limelitaka Gazeti la Dira kuomba radhi Mara moja wakishindwa kufanya hivyo hatua Kali na za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

ClY_I9oVAAEsSEt.jpg:large

Chanzo: ITV
***
haya Dira hoja hiyo mezani
 
Wa kuomba radhi ni mahakama inayoendesha kesi siyo gazeti. Make bila mahakama kusikiliza hiyo kesi gazette lisingepata habari.
 
JWTZ yakanusha taarifa za kuibwa kwa kifaru, lasema taarifa hizo hazina ukweli, lasisitiza ulinzi katika maeneo ya jeshi uko imara.

Hata hivyo Jeshi hilo limelitaka Gazeti la Dira kuomba radhi Mara moja wakishindwa kufanya hivyo hatua Kali na za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

ClY_I9oVAAEsSEt.jpg:large

Chanzo: ITV
Ni hatua za kisheria wala siyo kinidhamu. Nadhani waandishi wa DIRA siyo wanajeshi. Serikali (waziri) ndiyo wangetoa ilani ya kuwataka waombe radhi. Jeshi walipaswa waishie angalau kukanusha tu. Watajikuta wanaingia kwenye malumbano makubwa pale gazeti la DIRA litakapokaza uzi. Ngoja tuone.
 
Kesi iko mahakamani, Dira wamemnukuu mh Hakimu alafu wanatakiwa wakanaushe..? wanakanusha nini?
 
Duh! hii yako ni kali. yaani ITV ikachukulie habari zake TBC1? Radio One, Clouds FM. Kiss FM, Tanga Kunani FM zikapange foleni kuomba habari toka TBC FM? Kweli wewe ni jiniasi.
aahaha kuna watu sijui watumia akili za wapi kufikiria....angeangalia habari za TBC na UHURU gazet na magazeti mengine na vyombo vingine vya habari...habari zao zinautofauti though inaweza kuwa habari moja
 
Wakidhibitiwa hawa makanjanja utasikia oooh wanarudisha nyuma demokrasia,uhuru wa vyombo vya habari na majungu mengi sasa mukipewa uhuru ndio kuandika utumbo.
Ombi langu kwa serikali vyombo vyote vya habari vitoe taarifa zao kutoka katika vyanzo vya vyombo vya Serikali na sio kujitafutia habari zao za uzushi.
Una uhakika gani kama serikali itatoa data zote bila magumashi.?
wambie watoe uthibitisho wa taarifa yao
Watu wakiibua msiyotaka kusikia hamkosi kuwafungia haraka ili tusijue kinacho endelea
 
Sasa kosa la gazeti nini?, kama ni kosa basi wale waliowakamata wananchi ishirini na hakimu anayesikiliza hiyo kesi, hakuna sababu ya kuomba samahani
 
Wakidhibitiwa hawa makanjanja utasikia oooh wanarudisha nyuma demokrasia,uhuru wa vyombo vya habari na majungu mengi sasa mukipewa uhuru ndio kuandika utumbo.
Ombi langu kwa serikali vyombo vyote vya habari vitoe taarifa zao kutoka katika vyanzo vya vyombo vya Serikali na sio kujitafutia habari zao za uzushi.
Lazima unamatatizo ya viungo vya kufikiri
 
Ombi langu kwa serikali vyombo vyote vya habari vitoe taarifa zao kutoka katika vyanzo vya vyombo vya Serikali na sio kujitafutia habari zao za uzushi.

Aiseee.. Na Serikali hii ya sasa ya Magufuli..!
 
Back
Top Bottom