JWTZ: Mashujaa waliojitolea kutulinda

navy boi

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
1,517
480
UTENZI BORA WA LEO

Kuna shairi limeandikwa na Mwanajeshi mmoja nchini Nigeria limenivutia sana. Nimelitafsiri kwa Kiswahili na ninali-dedicate kwa Jeshi letu la Wananchi wa Tanzania (JWTZ);
_____________________________

Tunalala kwenye vumbi na matope ili wewe ulale kitandani,
Tunala na bunduki ili wewe ulale na mwenzi wako,
Tunalala porini ili wewe ulale kwenye nyumba,

Unavaa kofia maridadi ya kupendeza, sisi tunavaa kofia ngumu na nzito za chuma,
Unavaa "vest" nzuri ya pamba, sisi tunavaa "vest" za shaba,
Unavaa mkanda wa ngozi kiunoni, sisi tunavaa mikanda ya risasi,

Asubuhi unaamshwa na "alarm" nzuri ya simu yako, sisi tunaamshwa na milio ya mabomu na risasi,
Unatembelea gari zuri la thamani, sisi tunatembelea vifaru na malori,
Unakula chakula kizuri ukipendacho, tunakula wadudu na matunda porini,

Tunakesha ili wewe upate usingizi,
Tunaua ili wewe uishi,
Tunaumia ili wewe upone,

Tunaitoa sadaka "leo yetu" kwa manufaa ya "kesho yako",
Tunatoa sadaka maisha yetu ili kutetea maisha yako,
Tunakupigania usiku na mchana kwa sababu tunakupenda,
Tunaipenda nchi yetu,

Sisi ni wanajeshi,
Sisi ni wazalendo,
Sisi ni mashujaa,

Ombea wote waliofia vitani,
Wamekufa wakitetea nchi yetu,
Wamekufa wakitetea uhai wako,
Ni mashujaa wetu,

Nchi yetu,
Amani yetu,
Jeshi letu.
MUNGU LIBARIKI Jeshi La Wananchi wa Tanzania (JWTZ).!
 
samahani ndugu unaweza kuleta shairi hili kwa ki ingreza pia. Sio kwamba sijaelewa ila naamin kuna utaalam na artistic devices nyingi zimepotea baada ya kutafsiri japo maana itabaki kuwa ileile.

Duc in Altum
 
navy boi,

..shairi limeandikwa na mwanajeshi kwenda kwa raia.

..ilitakiwa liandikwe na raia wakiwaenzi wanajeshi.

..shujaa hata siku moja hajikwezi, bali huwa ni mnyenyekevu.

..shairi lina lugha ya kujisifia na kujikweza, kwa mfano maneno "sisi ni mashujaa" au "sisi ni wazalendo"

..pamoja na hayo naheshimu sana moyo wa kujitolea wa askari wetu. nauenzi mchago wa askari wote waliotumikia na wanaondelea kutumikia jeshi letu.
 
Nafikiri hata kada zingine za utumishi wa umma zinakutana na changamoto kwa namna yake.
Hata walimu, madaktari na manesi wameisha wahi kugoma kutokana na mazingira mabovu ya kazi.
 
navy boi,

..shairi limeandikwa na mwanajeshi kwenda kwa raia.

..ilitakiwa liandikwe na raia wakiwaenzi wanajeshi.

..shujaa hata siku moja hajikwezi, bali huwa ni mnyenyekevu.

..shairi lina lugha ya kujisifia na kujikweza, kwa mfano maneno "sisi ni mashujaa" au "sisi ni wazalendo"

..pamoja na hayo naheshimu sana moyo wa kujitolea wa askari wetu. nauenzi mchago wa askari wote waliotumikia na wanaondelea kutumikia jeshi letu.
Pamoja sana
Joka kuu.
Hawa watu wanamchango mkubwa sana.
Nikiwaza tu kwamba mtu anakula bata club
Lakin kuna sehem kuna kamanda yuko porini ana smg analinda mipaka ya nchi

Heshima kwao.
 
..tuko salama dhidi ya mashambulizi au uvamizi wa kijeshi.

..lakini nchi haiko salama ukiangalia jinsi mipaka yetu ilivyokuwa uchochoro wa kutorosha maliasili zetu.

..tunaingia hasara kubwa sana ktk eneo hilo, na ni vizuri serikali ya awamu hii ikaimarisha zaidi ulinzi mipakani ili kudhibiti magendo na hujuma za kiuchumi ktk mipaka yetu.
 
Ukiona hata hajaweka source...ya moja kwa moja yawezekana kaongeza 'chumvi' nyingi kwenye tafsiri. Bado nampa faida ya mashaka!
 
Mkuu aliyelitoa huko na kulitafsiri nahisii ni ndugu G.J.Malisa

Mbona kama hujamtaja apate credit zake?!
 
Hapana, wanalipwa kutulinda ... (ni ajira)
Hakuna mtu anaeweza kulipa gharama ya uhai anaoutoa mtu kuilinda nchi.. Kua mzalendo asee. Jaribu hata kuangalia vita vya kagera alafu uje na hii argument yako kuwa wanalupwa kutulinda.
 
UTENZI BORA WA LEO

Kuna shairi limeandikwa na Mwanajeshi mmoja nchini Nigeria limenivutia sana. Nimelitafsiri kwa Kiswahili na ninali-dedicate kwa Jeshi letu la Wananchi wa Tanzania (JWTZ);
_____________________________

Tunalala kwenye vumbi na matope ili wewe ulale kitandani,
Tunala na bunduki ili wewe ulale na mwenzi wako,
Tunalala porini ili wewe ulale kwenye nyumba,

Unavaa kofia maridadi ya kupendeza, sisi tunavaa kofia ngumu na nzito za chuma,
Unavaa "vest" nzuri ya pamba, sisi tunavaa "vest" za shaba,
Unavaa mkanda wa ngozi kiunoni, sisi tunavaa mikanda ya risasi,

Asubuhi unaamshwa na "alarm" nzuri ya simu yako, sisi tunaamshwa na milio ya mabomu na risasi,
Unatembelea gari zuri la thamani, sisi tunatembelea vifaru na malori,
Unakula chakula kizuri ukipendacho, tunakula wadudu na matunda porini,

Tunakesha ili wewe upate usingizi,
Tunaua ili wewe uishi,
Tunaumia ili wewe upone,

Tunaitoa sadaka "leo yetu" kwa manufaa ya "kesho yako",
Tunatoa sadaka maisha yetu ili kutetea maisha yako,
Tunakupigania usiku na mchana kwa sababu tunakupenda,
Tunaipenda nchi yetu,

Sisi ni wanajeshi,
Sisi ni wazalendo,
Sisi ni mashujaa,

Ombea wote waliofia vitani,
Wamekufa wakitetea nchi yetu,
Wamekufa wakitetea uhai wako,
Ni mashujaa wetu,

Nchi yetu,
Amani yetu,
Jeshi letu.
MUNGU LIBARIKI Jeshi La Wananchi wa Tanzania (JWTZ).!
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.

Tanzania ni nchi ya amani na wanajeshi wetu ni kula, kulala, kunywa bia zisizolipiwa kodi na gwaride. Wamefanya kazi ni kuvamia uraiani na kupiga raia. Kwenye disaster kama ile ya Kilombero raia ndio waliobeba maiti iliyoopolewa.

Ili jeshi liko under utilized kabisa.

So I respectfully disagree. Hiyo poem inawafaa hao hao wa Nigeria.
 
Naomba KUULIZA Kwani Wao KUFANYA Hiyo KAZI Walilazimishwa? Kuna Mambo Mengine Tunayotaka KUYAKUZA au KUYASIFU Yanathibitisha UPUNGUFU Wetu Wa KIFIKRA. Hilo SHAIRI Halina Tofauti Na Kumkuta Mtu AKIMSIFIA Golikipa Wa Timu Fulani Kuwa Amedaka Vizuri Na Kuokoa MICHOMO Hatari Wakati KIUHALISIA Ni Wajibu Wa Huyo Golikipa Kulinda Goli Kwani Ndiyo AMESAJILIWA Kwa Jukumu Hilo. Wanajeshi KUTULINDA au KUTUPIGANIA Ndiyo WAJIBU Wao Wa KIUTENDAJI Na Tuache Kuwa Na HURUMA Zisizo Na Msingi Dhidi Yao. Si Mmetaka AJIRA Fanyeni Sasa!
 
Pole sana.
 
Baba yako kagame anaijua JWTZ vyema
So huwez kuisifia kamwe
Tunaijua hilo.
 
Ahh this is too much.. Hii ni mara ya 10 nakutana na shairi hili hili na kila mtu anajikweza amelifasiri yeye!!! Malisa kada wa chadema kule Facebook ana sema amelifasiri yeye.. Maundu kada wa ACT amefasiri yeye..
 
Back
Top Bottom