geophysics
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 904
- 166
Watu 10 wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar baada ya kupigwa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa kambi ya Bavuai Migombani kufuatia mke wa askari mmoja kuibiwa pochi na watu wasiojulikana.
Mwanamke huyo aliibiwa pochi hiyo huko Jangombe katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Habari kutoka eneo la tukio zimeeleza askari hao walianza kupiga watu kwa zamu katika mitaa ya Jangombe, Urusi na Mpendae majira ya saa 1:00 jioni juzi na kusababisha watu kukimbia ovyo na maduka kufungwa.
Source: www.ippmedia.com 11/03/2011