JWTZ, CUF wavutana

JWTZ, CUF wavutana

Jangakuu

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
513
Reaction score
221

[TD="bgcolor: #ffffff"]CHAMA cha Wananchi (CUF) na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wameingia katika mvutano mkali kuhusu mateso yanayodaiwa kufanywa na askari wa jeshi hilo dhidi ya viongozi wa chama hicho na raia mkoani Mtwara.
Wakati CUF wakizitaka asasi za kiraia zinazoshughulikia haki za binadamu na haki za wanawake kumsaidia kisaikolojia mwanamke anayedaiwa kubakwa na askari wa JWTZ mkoani humo, jeshi hilo limeonya kuwa tukio hilo ni la kupandikizwa.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, JWTZ imewataka wananchi wapuuze taarifa hizo zinazofanywa na watu wenye malengo ya kulichafua jeshi.
Wakati JWTZ ikitoa taarifa hiyo, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema askari wa jeshi hilo waliopo Mtwara wamekuwa wakifanya vitendo vya kihalifu ikiwemo kutesa, kubaka na kuwapiga watu.
Lipumba alisema kutekwa kwa Naibu Mkurugenzi wa CUF Taifa, Shaweji Mketo na viongozi wengine wa chama hicho Mkoa wa Mtwara, ni kinyume cha sheria na kitendo hicho kinapaswa kulaaniwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam jana, Lipumba alisema wanafanya mchakato wa kushughulikia uonevu huo wa JWTZ.
Profesa Lipumba alisema mbali ya Mketo, viongozi wengine waliotekwa na kuteswa ni Salum Hamis Mohamed (Mwenyekiti CUF Mtwara Mjini), Ismail Hamis Jamal (Mwenyekiti CUF Mtwara Vijijini), Ismail Bakari Njalu (Mwenyekiti wa Vijana -JUVICUF Mtwara Mjini), Said Issa Kulaga (Katibu CUF Mtwara Mjini) na Kashindye Kalungwana (Dereva wa CUF Ofisi Kuu)
Alisema katika hatua hizo, watahakikisha waliohusika na unyama dhidi ya mwanamke huyo wanafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Alieleza kuwa, viongozi hao baada ya kutekwa na askari wa JWTZ, walivuliwa nguo zote na kulazwa kifudifudi, kumwagiwa maji ya baridi na kupakwa chumvi kisha kuanza kupigwa usiku kucha kwa kutumia mikanda ya jeshi, ngumi, mateke, fimbo maalumu za ngozi za wanyama na miti maalumu.
Akielezea tukio hilo, Profesa Lipumba alisema viongozi hao wakiwa njiani kurejea Mtwara mjini wakitokea Msimbati, ghafla waliona magari mawili ya kijeshi ambayo baada ya kuona gari la CUF lenye namba T 886 BGW, waliziba barabara na askari wa JWTZ waliwashusha na kuanza kuwapiga na kisha kuwarusha kwenye karandinga la jeshi.
Alisema baadaye viongozi hao walipelekwa katika kambi ya jeshi ya Naliendele kabla ya kuachiwa majira ya saa 5:00 usiku kwa kukabidhiwa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara ambaye hadi anakabidhiwa viongozi hao, alikataa kutoa ushirikiano kwa CUF.
Alisema Mketo alipozinduka Juni 28 alijikuta ana dripu na hakuelewa ni ya nini na baadaye wanajeshi waliitoa.
Profesa Lipumba alisema tukio la utesaji raia ndani ya kambi ya jeshi ukiliunganisha na matukio mengine kama ya uteasaji wa Dk. Stephen Ulimboka, kutekwa nyara kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, kulipuliwa bomu katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kunadhihirisha hatua za awali za kusambaratika kwa dola.
Licha ya malalamiko hayo, taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya Jeshi la Wananchi, ilieleza endapo taarifa hizo zitatangazwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari wananchi wazipuuze, kwani hazina ukweli wowote zaidi ya kuwa ni za upotoshaji.
Kauli ya jeshi ilisema: “Msichana huyo amepandikizwa ili kuharibu taswira nzuri ya JWTZ. Ifahamike kwamba maofisa na askari wa JWTZ waliopo Mtwara wanafanya kazi kwa uangalizi wa karibu, na vitendo hivyo vya aibu hawawezi kuvifanya. Jeshi letu linafanya kazi kwa nidhamu na si kama baadhi ya watu wenye maslahi binafsi wanavyolipaka matope.”


[TD="bgcolor: #ffffff"]
na Mwandishi wetu

[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #ffffff"][/TD]
[/TD]
Source: Tzdaima
 
siku hiz hadi jeshini ni Siasa Tupu. Tabu kwelikweli
 
Prof Lipumba na wenzako, subirini Obama aondoke. Sasa hivi hata masikio ya wanaharakati yako kwenye ziara ya huyo Mkuu wa sayari iitwao dunia!
 
Mungu saidia Tanzania kama na jeshi limefikia huko nchi hii itasambaratika.vipande vipande
 
Poleni sana CUF inaonyesha Mume kamchoka mke wake. Ama kweli NDOA NDOANO. NENDENI KWA MSHENGA MKA MWELEZE HAYO MATATIZO.
 
Ndio maana naogopa kumili bistola ungese kama huu wa jwtz siwezi vumilia lazima ndingeondoka hata na wa2 hv...na kama una guruneti unawalipua wote kwenye karandinga lao kuingiza jeshi kwenye siasa ni hatare sana.
 
Poleni wana CUF Ile kauli ya Waziri Mkuu Pinda ndo inavyotekeleza sasa nyinyi na.CCM si mna ndoa mbona Policcem na Jeshccem wanawakandamija wajameni wakati mu sehemu ya serikali tawala ya Yule rais Professor wenu akimuita ni Bwana Mkubwa na Kusema ilibidi aokoe Jahazi la Bwana Mkubwa huyo uchaguzi wa 2010. Yashangaza haya yaleyale ya Asifuye Mvua,.......
 
Watu hapa jamvini wanadai tuna jeshi, mimi nauliza jeshi lipi JWTZ.
Jeshi letu limejaa wahalifu na watu wenye hamu ya kutumika kisiasa
kwa manufaa yao binafsi na ya CCM.

Huyo kamanda (CEO) wa Kikosi cha JWTZ Naliendele ni la zima ataukwaa ukuu wa wilaya hivi karibuni.
Wale mano jua jina lake hebu tuleteeni hapa ili tumpe vipande vyake.
CCM wanageuza vikosi vya jeshi kuwa mahabusu za kisiasa??
Wanajeshi nao wanakubali kutumika kama gagulo chafu kwenye dangulo??
Jeshi gani hili jeshi la kuteka na kutesa wananchi wake??
Jeshi jeshi gani linalipua maghala ya silaha baada ya kuuza silaha na nyingine kuzificha ili zitumike na vibaraka wa CCM kulipua mikutano ya kisiasa ya Wapinzani??
Jeshili JWTZ jeshi gani jeshi la wahuni wabakaji na walawiti??
Jershi JWTZ jeshi gani jeshi njaa la wezi na wanyang'anyinyi???

Jeshi JWTZ jeshi gani la kupiga raia wake magumi, mateke na kuwaning'iniza viwiko vya mikono kwa stairi ya makaburu wa Afrika ya kusini??
Jeshi JWTZ jeshi gani linaloyumbishwa na wanasiasa wenye njaa, uchu wa madaraka na damu ya raia wa Tanzania wasio na hatia????

Jeshi JWTZ jeshi gani linatumika kama walinzi wa kolokoloni kwenye nyumba za Vibosile wa CCM.

Jeshi JWTZ jeshi gani lenye maafande wenye mawazo mafupi kama anduje na mgando kama gundi ya PATEX???

Lete majina ya wahusika wa UHUNI unao fanywa na jeshi letu JWTZ ili tuwachambue mmoj mmoja
Siku zote Hatuangalii, mvi kichwani cheo wala mabegani ana nini, mtu yeyote tutampa vipande mpaka ashibe na kuweweseka.

JF itakuwa kama kutembe uchi mbele ya mkwe
 
CUF musisubiri watu wa kuwatetea nyinyi wenyewe munaweza.
 
Wakati wenzao wa CHADEMA wakiwa Arusha kupambana hali kama hiyo wenyewe wakawa wanafanya mapinduzi bungeni, ambayo hata hivyo yalishindwa.
 
Mbona Mwigulu Nchemba a.k.a mzee wa kuropoka na kumwaga pumba hajitokezi kusema CUF wamejiteka ili kutafuta umaarufu?
 
Ina maana polisi wameshindwa kabisa kulinda raia na mali zao mpaka wanajeshi watumike kwa kazi za polisi? Nchi hii inaelekea kubaya.
 
Kwa kweli kama hali ndo hiyo,duu hapo mambo magumu,lakin kigoma washaanza kuingia wanaume wa KAGAME,maana wale ndo wanaume hawa wakwetu ni wakiume kwa wale ni wachumba tu,na kagame anasubiri jk aseme fyooo!
 
Poleni sana CUF inaonyesha Mume kamchoka mke wake. Ama kweli NDOA NDOANO. NENDENI KWA MSHENGA MKA MWELEZE HAYO MATATIZO.

Sasa ni nani anaelekea kuchumbiwa ili tuandae sare za kitchen party na send off?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ndio maana naogopa kumili bistola ungese kama huu wa jwtz siwezi vumilia lazima ndingeondoka hata na wa2 hv...na kama una guruneti unawalipua wote kwenye karandinga lao kuingiza jeshi kwenye siasa ni hatare sana.

ndiyo akili yako inavyokutuma?
 
CUF wanapaswa kuelewa kuwa ccm imedhamiria kuua watanzania ili mradi kutimiza malengo yao
hivyo waache ushabiki wa kinafiki pale CDM wanapoumizwa na maccm na mapolisi wao'
 
Back
Top Bottom