JWTZ, CUF wavutana

JWTZ, CUF wavutana

Watu hapa jamvini wanadai tuna jeshi, mimi nauliza jeshi lipi JWTZ.
Jeshi letu limejaa wahalifu na watu wenye hamu ya kutumika kisiasa
kwa manufaa yao binafsi na ya CCM.

Huyo kamanda (CEO) wa Kikosi cha JWTZ Naliendele ni la zima ataukwaa ukuu wa wilaya hivi karibuni.
Wale mano jua jina lake hebu tuleteeni hapa ili tumpe vipande vyake.
CCM wanageuza vikosi vya jeshi kuwa mahabusu za kisiasa??
Wanajeshi nao wanakubali kutumika kama gagulo chafu kwenye dangulo??
Jeshi gani hili jeshi la kuteka na kutesa wananchi wake??
Jeshi jeshi gani linalipua maghala ya silaha baada ya kuuza silaha na nyingine kuzificha ili zitumike na vibaraka wa CCM kulipua mikutano ya kisiasa ya Wapinzani??
Jeshili JWTZ jeshi gani jeshi la wahuni wabakaji na walawiti??
Jershi JWTZ jeshi gani jeshi njaa la wezi na wanyang'anyinyi???

Jeshi JWTZ jeshi gani la kupiga raia wake magumi, mateke na kuwaning'iniza viwiko vya mikono kwa stairi ya makaburu wa Afrika ya kusini??
Jeshi JWTZ jeshi gani linaloyumbishwa na wanasiasa wenye njaa, uchu wa madaraka na damu ya raia wa Tanzania wasio na hatia????

Jeshi JWTZ jeshi gani linatumika kama walinzi wa kolokoloni kwenye nyumba za Vibosile wa CCM.

Jeshi JWTZ jeshi gani lenye maafande wenye mawazo mafupi kama anduje na mgando kama gundi ya PATEX???

Lete majina ya wahusika wa UHUNI unao fanywa na jeshi letu JWTZ ili tuwachambue mmoj mmoja
Siku zote Hatuangalii, mvi kichwani cheo wala mabegani ana nini, mtu yeyote tutampa vipande mpaka ashibe na kuweweseka.

JF itakuwa kama kutembe uchi mbele ya mkwe
haya unayoongea unayajua au unaongozwa na hisia za chama chako cha cuf
 
Raia mwema yeyote ni lazima aguswe na haya , tuache kuwananga CUF pamoja na makosa yao hawastahili kufanyiwa hayo na wananchi wa Mtwara hawastahili kunyanyaswa/ kuteswa.
 

[TD="bgcolor: #ffffff"]CHAMA cha Wananchi (CUF) na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wameingia katika mvutano mkali kuhusu mateso yanayodaiwa kufanywa na askari wa jeshi hilo dhidi ya viongozi wa chama hicho na raia mkoani Mtwara.
Wakati CUF wakizitaka asasi za kiraia zinazoshughulikia haki za binadamu na haki za wanawake kumsaidia kisaikolojia mwanamke anayedaiwa kubakwa na askari wa JWTZ mkoani humo, jeshi hilo limeonya kuwa tukio hilo ni la kupandikizwa.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, JWTZ imewataka wananchi wapuuze taarifa hizo zinazofanywa na watu wenye malengo ya kulichafua jeshi.
Wakati JWTZ ikitoa taarifa hiyo, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema askari wa jeshi hilo waliopo Mtwara wamekuwa wakifanya vitendo vya kihalifu ikiwemo kutesa, kubaka na kuwapiga watu.
Lipumba alisema kutekwa kwa Naibu Mkurugenzi wa CUF Taifa, Shaweji Mketo na viongozi wengine wa chama hicho Mkoa wa Mtwara, ni kinyume cha sheria na kitendo hicho kinapaswa kulaaniwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam jana, Lipumba alisema wanafanya mchakato wa kushughulikia uonevu huo wa JWTZ.
Profesa Lipumba alisema mbali ya Mketo, viongozi wengine waliotekwa na kuteswa ni Salum Hamis Mohamed (Mwenyekiti CUF Mtwara Mjini), Ismail Hamis Jamal (Mwenyekiti CUF Mtwara Vijijini), Ismail Bakari Njalu (Mwenyekiti wa Vijana -JUVICUF Mtwara Mjini), Said Issa Kulaga (Katibu CUF Mtwara Mjini) na Kashindye Kalungwana (Dereva wa CUF Ofisi Kuu)
Alisema katika hatua hizo, watahakikisha waliohusika na unyama dhidi ya mwanamke huyo wanafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Alieleza kuwa, viongozi hao baada ya kutekwa na askari wa JWTZ, walivuliwa nguo zote na kulazwa kifudifudi, kumwagiwa maji ya baridi na kupakwa chumvi kisha kuanza kupigwa usiku kucha kwa kutumia mikanda ya jeshi, ngumi, mateke, fimbo maalumu za ngozi za wanyama na miti maalumu.
Akielezea tukio hilo, Profesa Lipumba alisema viongozi hao wakiwa njiani kurejea Mtwara mjini wakitokea Msimbati, ghafla waliona magari mawili ya kijeshi ambayo baada ya kuona gari la CUF lenye namba T 886 BGW, waliziba barabara na askari wa JWTZ waliwashusha na kuanza kuwapiga na kisha kuwarusha kwenye karandinga la jeshi.
Alisema baadaye viongozi hao walipelekwa katika kambi ya jeshi ya Naliendele kabla ya kuachiwa majira ya saa 5:00 usiku kwa kukabidhiwa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara ambaye hadi anakabidhiwa viongozi hao, alikataa kutoa ushirikiano kwa CUF.
Alisema Mketo alipozinduka Juni 28 alijikuta ana dripu na hakuelewa ni ya nini na baadaye wanajeshi waliitoa.
Profesa Lipumba alisema tukio la utesaji raia ndani ya kambi ya jeshi ukiliunganisha na matukio mengine kama ya uteasaji wa Dk. Stephen Ulimboka, kutekwa nyara kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, kulipuliwa bomu katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kunadhihirisha hatua za awali za kusambaratika kwa dola.
Licha ya malalamiko hayo, taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya Jeshi la Wananchi, ilieleza endapo taarifa hizo zitatangazwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari wananchi wazipuuze, kwani hazina ukweli wowote zaidi ya kuwa ni za upotoshaji.
Kauli ya jeshi ilisema: “Msichana huyo amepandikizwa ili kuharibu taswira nzuri ya JWTZ. Ifahamike kwamba maofisa na askari wa JWTZ waliopo Mtwara wanafanya kazi kwa uangalizi wa karibu, na vitendo hivyo vya aibu hawawezi kuvifanya. Jeshi letu linafanya kazi kwa nidhamu na si kama baadhi ya watu wenye maslahi binafsi wanavyolipaka matope.”


[TD="bgcolor: #ffffff"]
na Mwandishi wetu

[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #ffffff"][/TD]
[/TD]
Source: Tzdaima

Jwtz kwa hili kataeni tu lkn kutesa watu na kufanya matendo yalio kinyume na maadili ndio kawaida yenu, mkiishavaa magwanda munajiona kama askari wa motoni!
Ningewaona majasiri na kua mko makini kama mungekataa kuekwa under control ya american army ktk ujio wa Obama, hamuoni kua jinsi walivyokuja kua wamekuja na dola kamili na kua hata wakiamua kuishika nchi hamtakua na la kufanya kutokana na walivyokuzungukeni kila kona?

Sifa za utesaji na ubakaji kwa wanajeshi ni vitu vya kawaida, takriban majeshi wa mataifa yote hata wanajeshi wa kulinda amani baadhi yao hufanya vitendo kama hivyo.

JWTZ wala musizozane na wanasiasa jambo la msingi wawajibisheni askari wenu waliohusika na mambo hayo, hilo linawezekana timizeni wajibu wenu.
 
CUF member or CCM membe, is immaterial here, what is going on in Mtwara will make Sir Richard Turnbull and his colonial government look like angels sent from heaven.
I see fakeni JWTZ soldiers torturing and killing their fellow citizen under special and specific arrangement of CCM, because they happen to have different opinion politically

When people are politically drunk, the way CCM are like now, they tend to completely forget that their political opponents are human being and should not be treated differently.
CCM is dying and its grip to power is becoming loose by hours. In few month CCM will be an opposition party, how does it want to be treated?
We have tens of examples of Old gator political parties in Africa that lost power to their opponents to find themselves in none existence state ,as political parties, few minutes after their demise.



haya unayoongea unayajua au unaongozwa na hisia za chama chako cha cuf
 
Sio rahisi msichana kuja from no where na kuipakazia jwtz,kwa ujasiri upi alionao?. Jwtz stop being used we trust you,our hope and faith are vested on you guys,kwa hili mmechemka and i strongly conderm this foolish act.
 
CUF wanalalamika huku ndoa yao na CCM inaendelea kushamiri tu!!!
 
Back
Top Bottom