Juzi kati nimepanda Coaster za magazeti usiku Dar-Arusha, tulipepea njiani

marktindo04

Member
Dec 16, 2019
23
74
Mamb vipi wana JF,

Aisee siku ya Jtatu nilitakiwa niwai kuja Arusha kwa ajili ya majukumu muhimu sana, kwa bahati mbaya nilikosa train ya saa nane ya kuja Arusha so ikanibidi nitafte namna ya kuondoka jioni hyo hyo.

So kuna jamaa ang alikua anafaham hzo coaster za kuja arusha zinachukua abiria pale ubungo oilcom, so nliwai na kukata seat yang mida ya saa kumi jioni na gari ilifika pale mida ya saa mbili usiku ndio tukaanza safari yetu.

Nilikua na uoga mwanzoni kutokana na watu kusema kuwa hizi gari huwa zinakimbia sana , hivo safar ilianza mdgo mdgo hadi tulipo iacha bunju dreva akaanza moto wake.

Aisee gear alizokuwa anapiga so za kitoto na overtaking ilikua kawaida sana ,kuna mda dreva aliendesha speed ambayo sijawai ishuhudia maishani katika safari zangu. Moyo ulipiga mapigo 100 kwa sekunde hadi ukaacha wenyewe ilikua ni hatari sana, kiufupi siku sinzia mpaka nafika Arusha na tulitumia almost masaa 7 kufika Arusha.

USHAURI
Kupanda hizo gari ni risk kama ku trade forex na ada ya chuo ,hivyo tuwe makini ndgu zangu
 
Tatizo mnazidi kukariri wadogo zetu kila gari linatombea usiku na linalokimbia sana ni gari ya gazeti.

Yaani gari ya gazeti itoke Dar saa mbili usiku inapeleka Return au?

Gazeti kuanzia saa sita usiku ndo inatoka dar,halafu kampuni ipi ya gazeti wa coaster njia hiyo ya AR?
Eti wanakatisha na tiketi?

Halafu kuna kitu mnaweza tu msikijue mkawa mnaishi kwa masimulizi zaidi,unahisi na kuamini gari hizo za gazeti watu hawaziachi njiani?kwamba hazipitwi na magari mengine?

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Kwanini msafii roho juu juu wakati kuna huu hata upepo husikii wala kuona chochote zaidi ya kufika kwa sekunde kadhaa kule uendako?
images - 2022-06-09T110531.335.jpeg
images - 2022-06-09T110528.536.jpeg

Japo na wenyewe una chamgamoto zake traffic police wanaweza kukusimamisha kama hivi na wakati huna leseni👇
images - 2022-06-09T110559.131.jpeg
 
Ulipanda coaster za kawaida kijana, nazo zinakimbia ila si sawa na hizo za magazeti
 
Tatizo mnazidi kukariri wadogo zetu kila gari linatombea usiku na linalokimbia sana ni gari ya gazeti.

Yaani gari ya gazeti itoke Dar saa mbili usiku inapeleka Return au?

Gazeti kuanzia saa sita usiku ndo inatoka dar,halafu kampuni ipi ya gazeti wa coaster njia hiyo ya AR?
Eti wanakatisha na tiketi?

Halafu kuna kitu mnaweza tu msikijue mkawa mnaishi kwa masimulizi zaidi,unahisi na kuamini gari hizo za gazeti watu hawaziachi njiani?kwamba hazipitwi na magari mengine?

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
Gari za gazeti huwa hawakatishi tiketi ila Kuna coaster zinajibrand kuwa ni za magazeti kumbe sio kweli
 
Back
Top Bottom