Serikali Kuruhusu safari za Usiku ni msaada kwa Wafanyabiashara na wenye ratiba ngumu

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Dhana za ajari tuweke pembeni, Ajari nyingi hapa kwetu ni Uzembe wa Madereva, ndiomaana neno lililozoeleka panapotokea ajari ni Mwendo mkali, Overtake, Kukwepa Boda boda n.k jambo ambalo haliamuliwi na muda bali uzembe, tena usiku mwanga wa taa unaweza ukawa unasaidi kujua kua kuna gari mbele yako.

Labda Wapo ambao wao vyovyote vile haibadilishi kitu kwao, japo Siku inaweza ikatokea dharura ndio ukatamani na kukumbuka, ila kuna makundi ambayo moja kwa moja yatasaidika na haya maamuzi

Kundi la kwanza...

MFANYAKAZI AMBAYE NI MFANYABIASHARA..
Kuna watu Mchana anatakiwa kazini J3-Ijumaa, J mosi & J2 ndio gap lake la Kuingia sokoni, Siku mbili tuu hizo ukisema uzigawanye kuzitumia tena kusafiri unabaki na madakika, hivyo Usiku wa ijumaa ndio mda wake wa kusafiri, weekend Biashara inafanyika, Jumapili usiku unageuza na Mzigo wako au Pesa ya mauzo.

Hii nazungumzia kwa Experience kabisaa
Binafsi nalazimika sana ijumaa usiku kutega Malori au SPECIAL HIRE nisafiri nifike sokoni asubuhi,
Nifanye mishe Jumamosi na Jumapili mpka jioni nitafute tena Gari ya kugeuza,
Hii itasaidia sana kupata usafiri wa uhakikaa kuliko kulenga Malori au Upande Special Hire iliyojaa ukalie jeneza(hii ni kawaida kwangu)

Kundi la Pili....
Kuna watu ni wafanyakazi, amepata dharura Jioni anatakiwa aende mkoani, Akisubiri tuu asubuhi ashachelewa tukio aendako,

Huyo huyo akitaka kurudi akisema tuu asubiri asubuhi ni kwamba tayari atarudi nje ya muda, anakutana na Notisi.

Kundi la tatu...
Kuna Watu kitendo cha kutumia Mda wa mchana kukaa kwenye seat masaa 8,9,10 n.k ni kupoteza muda hasa Wafanyabiashara ambapo moja kwa moja ni msimamizi wa biashara yake..

Lakini pia...
Mda wa kutosha kufanya Kilichokupeleka...
Chukulia una time limit ya Siku 2 tuu nzima, Mfano j1 & j2, Unapoondoka Jumamosi tayari hapo ushaikata siku au ushaivunja kabisa, yaani ufike usiku au Mchana/jioni,

Hapo kumbuka kesho asubuhi ni safari, utapata wapi mda wa kushughulikia jambo lako? Ila kwa njia hii unaondoka ijumaa usiku, Asubuhi upo Site, jumapili unashinda, usiku safari ya kurudi, unakua na siku 2 zilizoshiba hata za kusalimia kijijini/wazee/ndugu n.k

KUPUNGUZA FOLENI....
Foreni za msululu wa mabasi asubuhi(ushawahi ona hapo mbezi saa 12 asubuhi idadi ya basi zinazotoka at once?) kukimbizana kutoka stand na njiani zile ligi pita nikupite niwahi kufika zitapungua, hii itapunguza foreni zisizo na ulazima na ajari piaaa.

WAZEE WA BAJETI....
Hii pia naandika kwa experience l,
Kwanza Safari za usiku binafsi hua nachajiwa pesa pungufu, mfano moshi Dar Asaivi ndio imepanda nawapa 15k-18k nakati ukisubiri tuu asubuhi hapo unazungumzia 25k huko kuendelea,
Hapo hapo Wale ambao ukifika hutaki kwenda kuzongana kwa ndugu na jamaa utahitaji guest, Mimi naondoka zangu Moshi/arusha saa 2 usiku nalala kwenye gari nafika ubungo Mataa saa 12, hapo ushaokoa Ya guest, Jioni umekula nyumbani,
Hua unasave si chini ya 50k ambayo unaiingiza mzigoni..

Yote kwa yote Ajari zipo pia, mara nyingi tuu tushachomoa watu wakiwa hawafai,
Lakini Pia Madereva kulala, kuna siku tuliingia chaka, dereva kushtuliwa anafoka, mimi mzoefuu naona kila kitu huku anapangusa macho...
 
Vithibiti mwendo navyo vitolewe, watu tunataka kwenda na muda kuukomboa wakati, time is money. Dar-mwanza, dar-arusha, dar-mbeya hakuna kupoteza muda mwingi njiani kufika huko kama kuna uwezokano wa kukimbia haraka mabasi yakimbie tu. Kuwaza ajali ni mawazo yanayounda matukio hayo, ukiwaza chanya au hasi utapata matokeo yake. Mabasi yamekuwa mengi barabarani ukichanganya na magari mengine ni foleni kubwa isiyosogea kwa haraka kuingia jijini dar. Safari za usiku zitapunguza foleni kubwa barabarani kwa kuwa mabasi mengi yatasafiri sa 24
 
Vyombo vya usalama pia viwe macho 24/7 kudhibiti majanga ya wale majambazi wa kutega magogo na kuteka magari barabarani kama miaka ile ya 90.
 
Back
Top Bottom