Hizi Coaster za Dar-Moshi USIKU/Moshi-Dar USIKU, Zina utaratibu Gani?

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,226
Naomba kujua Je Ni ratiba maalum yenye kibali cha serikali? Kwa Moshi/Arusha nazipata wapi? Dar najua Ni kimara kibo jioni..

Zinaingia Dar Kwenye saa kumi hivi usiku, wengi hua tunashukia Ubungo mataa..

Mimi hua napandia njiani hivyo nashindwa kuelewa jee watu waliomo ndani wanafahamiana wameikodisha? Au ina sanya kama gari nyingine?

Nimekua nikisafiri nazo sana na zimekua na msaada sana kwangu, ningependa kujua mbili tatu....
 
Special Hire, zikiwemo,
Hii ni maalumu kwa Wafanyabiashara ambao hawataki kupoteza siku wakiwa safarini, usiku wa kwanza anaenda lets say Dar, siku inayofuatia anaingia k.koo kununua mzigo, Jioni safairi.

Lakini pia wafanyakazi ambao wanatakiwa makazini/hawana ruhusa..

Ole wako sasa ifika kabla ya Saa 6 hujapita Mkata.
 
Labda kama dereva mgeni. Kuna chocho moja wazoefu wanapiga denge wale majamaa wa Mkata wanabaki wamelala tu hawajui chombo kimeshapita
 
Zamani ilikua pale ubungo maji,kwenye ile mitambo ya gesi pembeni ya barabarani huwa wanapaki pale..sijui kwa sasa.
ubungo sheli wanakuwepo pia siku hizi,ukiwahi sn asbh zipo na jioni kuanzia saa 10 alasiri..ilahawakai muda mrefu sn...
 
Labda kama dereva mgeni. Kuna chocho moja wazoefu wanapiga denge wale majamaa wa Mkata wanabaki wamelala tu hawajui chombo kimeshapita
Kuna chocho flan kweli sijui panaitwaje pale, ila nahisi ni njia ya Handeni ile, pana kama ka muninuko ukiwa unaingia mana ilikua usiku, kuna siku tulishapita, nakumbuka ilileta mzozo sana kwa abiria, dereva aliomba abiria waongeze buku buku sababu ni ya Mbali.
 
Hivi kwa sasa kuna sehemu nyingne Tz hii ikifika Saa 6 hupiti zaidi ya Mkata?
Nyingi zimekufa mfano Moro kulikua na hii inshu ila naona imeshakufa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom