Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,508
- 911,249
Tuesday, 11 January 2011
* Ahoji uhalali wa kampuni ya kitapeli kulipwa fidia
* Wanaharakati kwenda mahakamani kuipinga
Na Bakari Mnkondo na Furaha Omary
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza suala la kampuni ya kufua umeme ya Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, ameibuka na kuhoji uhalali wa kampuni ya Dowans, ambayo ni ya kitapeli kulipwa fidia kwa utapeli wake.
"Nikiwa mwanasheria ninasubiri kwa hamu maazimio ya Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC) yasajiliwe Mahakama Kuu ili kuona maamuzi ya kuilipa Dowans yalifikiwaje nataka kujua msingi wa tapeli kulipwa fidia kwa utapeli wake?" amesema.
Alitoa maoni yake jana kuhusu sakata la Dowans baada ya kutafutwa na gazeti hili kwa muda mrefu. Hivi karibuni ICC ilifikia uamuzi wa kulitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuilipa kampuni ya Dowans sh. bilioni 97 kutokana na kuvunja mkataba kinyemela. Baada ya uamuzi huo, suala hilo lilifikishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ambaye alitoa ushauri kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, wa kukubali serikali kuilipa Dowans endapo uamuzi wa ICC utasajiliwa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kwa kauli hiyo, Dk. Mwakyembe, ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, anaungana na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, sasa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupinga kampuni ya Dowans kulipwa kiasi hicho cha fedha.
Akifafanua kuhusu msimamo wake wa kitaalamu, ambao alisisitiza ni tofauti na wa kisiasa, Dk. Mwakyembe alisema ana shauku ya kujua ni kwa namna gani serikali imepoteza kirahisi kesi hiyo, ambayo alisema hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa digrii ya sheria angeweza kuisimamia na kushinda.
"Upande wa kisiasa sina tatizo wapo wa kulizungumzia, lakini kitaalamu nitalizungumzia kwa kina kwa kuwa nipo kwenye taaluma ya sheria kwa miaka 20 nikiwa mwalimu. Ningependa kujua msingi wa ICC kufanya lililo batili jana kuwa halali leo," alisema.
Alisema kamati teule ya Bunge ilimaliza kazi kwa kutoa maazimio kadhaa, ambayo hadi sasa hakuna lililofutwa, na moja ya maazimio hayo ni kuiona Richmond ni kampuni hewa, hivyo kupendekeza ifutwe kwenye orodha ya kampuni za Tanzania na Oktoba, 2008 ilifutwa rasmi.
Dk. Mwakyembe alisema anasubiri kuona ICC ilimuonaje mmiliki wa Dowans Holdings SA, iliyosajiliwa nchini Costa Rica, ambako serikali ya nchi hiyo ilisema haimtambui kwa kuwa hana anuani wala ofisi.
"Kwenye kamati tulifanya utafiti wa kina na serikali ya Costa Rica ilitueleza mmiliki wa kampuni hiyo hajulikani kwa jina, ofisi, anuani ya posta wala namba za simu," alisema.
Dk. Mwakyembe aliyewahi kuwa mwalimu wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema walichoambulia Costa Rica ni kutajwa jina la Bernal Zamora Arse, anayemiliki kampuni takriban 100 zenye kuishia na SA, lakini hazielezi zipo jengo gani, nyumba ama kumiliki gari au pikipiki.
Alisema kutokana na ukweli huo, anashangazwa kuona uamuzi wa ICC ulivyofikiwa, na kuhoji fedha hizo zitalipwa kwa nani?. Dk. Mwakyembe alisema anasubiri uamuzi huo usajiliwe ili apate fursa ya kuupitia kwa kina na kuoana hatua za kuchukua kama mwanasheria.
Wakati huo huo, wanaharakati kupitia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wanakwenda Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kupinga amri ya TANESCO kuilipa Dowans fedha hizo, wakisema haina uhalali wa kulipwa, kwa kuwa ilishafahamika kuwa Richmond iliyoirithi ni kampuni hewa.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, wakili Francis Kimwaga, alitangaza hayo jana mjini Dar es Salaam, alipotoa tamko la wanaharakati kuhusu mtazamo na muitikio wa serikali kuhusu shauri hilo la Dowans. Alisema katika kesi waliyotarajia kuifungua jana, wanapinga kusajiliwa kwa uamuzi wa ICC.
Alisema kituo hicho na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu, usawa wa jinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct), wameshitushwa na kusikitishwa na mtazamo na muitikio wa serikali kuhusu shauri la Dowans.
"LHRC itafungua shauri leo (jana) Mahakama Kuu kupinga uhalali wa tuzo iliyotolewa kwa Dowans na ICC na isisajiliwe kwa kuwa mikataba ya awali ilipatikana kwa rushwa na kukiuka maslahi ya umma," alisema.
Kwa mujibu wa Kiwanga, mwenendo wa Wizara ya Nishati na Madini kuhusu suala hilo pia unatia shaka, hususan malipo kwa Dowans.
Alisema katika suala hilo kuna mambo ya kujiuliza, yakiwemo ya kuendeshwa kwa usiri kwa shauri hilo katika Mahakama ya ICC bila wananchi kuelezwa kilichokuwa kikiendelea tofauti na kesi ya Bi-Water dhidi ya serikali, ambapo walialikwa kama marafiki wa mahakama.
ìIkiwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kwa taarifa ya kamati teule ya Bunge iliyoundwa Novemba 13, 2007 kikao cha 11, mkutano wa tisa), ilithibitisha Richmond ni kampuni hewa, inawezekanaje kuwa na mkataba wa kurithisha mali zake kwa Dowans?.
"Uhalali wa kisheria wa miliki ya Dowans kwa mali za Richmond haupo, kwa nini serikali haikutaifisha mali za Richmond tangu awali?" alihoji Kiwanga.
Aliyataja mambo mengine ya kujiuliza ni ikiwa Dowans haikurithi kwa uhalali mali ya Richmond, inawezekanaje kuwa mdai halali dhidi ya serikali kuhusu mali iliyopatikana kutokana na uhalifu, na serikali kuharakisha kuilipa Dowans kuhusu mali iliyopatikana kwa uhalifu.
Kiwanga alihoji sababu za TANESCO kulazimishwa kuilipa Dowans wakati tangu awali ilishakataa kuhuishwa mkataba haramu wa Richmond kwa Dowans.
Wanaharakati hao wameitaka serikali na maofisa wa umma wanaohusika na suala hilo kuzingatia maelekezo ya Katiba na waheshimu uamuzi wa Bunge kuwa, Richmond ni kampuni hewa, hivyo kuendelea kulazimisha Dowans ni kukiuka utawala wa sheria.
Wameitaka Wizara ya Nishati na Madini kuacha kuwabebesha Watanzania mzigo wa kulipa gharama hizo kutokana na kodi wanazolipa, kwa kuwa malipo hayo yanatokana na uzembe, ubadhirifu na ufisadi.
Kwa upande wake, Dk. Sengondo Mvungi, alisema wanakwenda mahakamani ili kupata majibu ya mambo mbalimbali, huku akisema mahakama haipaswi kusajili matapeli, ila isimame iungane na wanaharakati hao na kuwataka Watanzania kujitokeza kupinga hukumu hiyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya, alisema inapaswa picha za wamiliki wa Dowans ziwekwe hadharani ili Watanzania wawajue wanaolipwa fedha hizo, badala ya kutajwa majina.
Chanzo: Uhuru