"Justice For Jahenda" - Hasira Yahamia Buruburu Baada ya Video Ya UnyanyasajI

"Justice For Jahenda" - Hasira Yahamia Buruburu Baada ya Video Ya UnyanyasajI

Wakaguongo

Member
Joined
Sep 23, 2026
Posts
62
Reaction score
33
Kilichoanza kama video iliyosambaa mitandaoni sasa kimehamia mitaani. Vijana wamejitokeza leo huko Buruburu, Nairobi, wakielekea katika Kanisa la Redeemed Gospel Church, wakitaka hatua zichukuliwe kufuatia video inayomuonyesha msichana anayetambuliwa kama Jahenda akidhalilishwa na kundi la wasichana ndani ya 'washrooms' zinazoaminika ni za eneo la burudani ambalo bado haijabainika wazi ni wapi hasa.

Kwa nini GenZ wameandamana kanisani humo?

Ni kwa sababu kuna madai mitandaoni kwamba mmoja wa wasichana walionakiliwa kwenye video wakimdhalilisha Jahenda ni binti ya Mchungaji Mkuu wa kanisa hilo. Hatahivyo, Mchungaji Felix Kavoi sasa amekanusha madai hayo, akisema yeye si baba wa msichana yeyote kati ya wanaohusishwa na video hiyo.

Video hiyo imezua hasira kubwa nchini tangu iliposambaa wiki hii. Ndani yake, Jahenda anaonekana akiwa amezungukwa na wasichana wengine huku baadhi yao wakirekodi tukio hilo. Mmoja wao anaonekana kumshika shingoni, huku Jahenda akijaribu kuomba msamaha.

Ni tukio lililopelekea hata Chuo Kuu Cha Riara kutoa tamko baada ya baadhi ya walioonekana kwenye video hiyo kuripotiwa kuwa wanafunzi wake. Chuo hicho kilikemea tukio hilo na kusema kimeanzisha uchunguzi wa ndani n pia kiko tayari kushirikiana na mamlaka zinazochunguza suala hilo.
987.jpg


Na leo, hasira hiyo imeonekana kuhamia nje ya mitandao, huku vijana wakifika Buruburu kudai uwajibikaji.


Hivyo basi, mjadala sasa si kuhusu video pekee. Ni kuhusu Jahenda kupata haki, uchunguzi kufanyika bila upendeleo, na kuhakikisha kuwa umaarufu, uhusiano wa kifamilia, taasisi au hadhi ya mtu haviwezi kuwa kinga dhidi ya uwajibikaji.

Je, hasira ya umma iliyohamia mitaani itasaidia kusukuma uchunguzi wa haki au itaishia kuwa tukio lingine la siku chache kwenye mitandao?
 
Back
Top Bottom