Jumuiya ya Waswahili Kariakoo wampa onyo Makinda na wenzake

Kuitwa mswahili wa Kariakoo sio tusi,kama mtoa hoja alivyoelelzea,waanzilishi wa Taifa hili waliishi na kufanya harakati zao katika maeneo ya Kariakoo.Vyama vya TAA,TANU,Congress vilizaliwa Kariakoo.Kwa sasa Kariakoo ni business district,biashara za kila aina zinafanyika pale na watu mbali mbali.

ni kweli sio tusi, lakini inapolinganishwa na mambo mabaya ndio tusi
 
wamsamehe tu jaman.
ni bnadamu yule


:A S 12:na pia akuisema kwa nia mbya...sema tu aliitoa wakat mbaya....
 
itakuwa vizuri itawasaidia watu kupunguza kuropoka ingawa nahisi ni maneno tu hakuna utekelezaji
 
Nimepita mda si mrefu pale kariakoo nikakuta baadhi ya watu wanaangalia kama kuna uwezekenao wa kumburuza mahakamani Spika Makinda kwa madai ya kuwatukana, na wengine wanataka kuandamana kupinga kauli yake aliyoitoa bungeni kwa wabunge akiwaasa waache kujidharau kwa kufanya mambo hovyohovyo mithili ya watu walioko Kariakoo Dar es Salaam. "Huyu mwanamke amevuka mipaka ameacha kushughulika na bunge ameamua kupolomosha matusi dhidi yetu tumemkosea nini?" Analalamika mfanya biashara mmoja

Anaweza akathibitisha maana pale kariakoo kuna watu wanafanya mambo hovyohovyo bila utaratibu maalum
 
Hii inanikumbusha sakata la Pius Msekwa wakati akiwa spika. Huyu aliwahi kusema “Watu waache wivu wa kike.” Msekwa alikuwa akijitetea kwa kupewa nafasi ya uenyekiti wa bodi ya wakurugenzi katika kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom wakati akiwa bado Spika. Lakini baadae 'aliomba radhi' kwa kusema hiyo ni nahau ya kiswahili! Makinda anaweza kuwa muungwana nae 'akaomba radhi' kwa kuteleza ulimi.
 
Duh! Ivi kumbe ukiisema Kariakoo unakuwa umewasema Waswahili. Kwa hiyo ukisema neno 'waswahili bwana wana matatizo' unakuwa umekisema kikundi cha watu flani.

Hata ukisema
1. Uswahilini kuna vituko!
2. Acha uswahili bwana!
3. Mbona unakuwa mswahili?
4. Mi sipendi mambo ya uswahili?
5. Fanya masaa ya kizungu sio ya kiswahili!
6. Jamaa ni mswahili mswahili?
7. Kuishi na waswahili taabu kweli!

Hapa ujiandae kupokea tamko la Waswahili.

Hili tamko naona lilikuwa standby, likisubiri siku limwangukie mtu tena wa imani flani kwa sababu sikuliona wakati ule alipolitamka mmoja wetu (McGamba) kipindi cha kampeni za uchaguzi.

Halafu mbona tamko lenyewe limekaa kama tamko la mswahili mmoja aliyeamua kuipa uhai kuonekana ni msimamo wa wengi? Sioni msemaji wa hao Waswahili, Mwenyekiti wa Waswahili, tamko limetolewa katika mkutano uliofanyika wapi na saa ngapi.

Tumeshajifunza, hii nchi haitachukuliwa na watu waliotumia muda mwingi kusoma madrasa. Mnaenda kujifunza chuki, visasi na matusi.

Makinda amesema "watu wa k.koo''
 
Tuanze kuheshimu jamii za watu tofauti hata kama hawana kitu lkn heshima iwepo, sio kwa vile kapewa huo uspika bure basi asiheshimu jamii za watu wengine, kila mtu ana haki sawa ingawa mbele ya CCM mafisadi ni nambari one, lkn sisi kwetu kila raia ni nambari one
 
siyoni kosa la mama hapa,kila mtu anatumia huo msemo,tuwe wakweli watu wa kariakoo kweli wanaongea bila mpango anayebisha aende leo,msimuonee mama!
 
Makubwa! Historia ya Kariakoo na povu juu, jamaa kaandika mpaka basi. Ila kwa ninavyomfahamu Makinda, hataomba radhi abadan! Anajua waliompa u-Spika si watu wa Kariakoo!
 
mdini mdini wewe!

Na huu udini tuliutumia vizuri kumng'oa mswahili Abuu Juma kwenye umeya wa manispaa yetu ya Ilala na kumsimika kijana wa kizazi kipya ambaye ni Graduate Jerry Silaa.
Maana ilifikia wakati huyu mswahili Abuu Juma alidhani jina la umeya ni sehemu ya jina la ukoo wake.
 
Hivi hii mada inahusu kauli ya Mh Spika Makinda pekee au kuna jambo limefichwa hapa? Mambo ya Nyerere, Chami, John Rupia, Sykes yanaingiaje hapa? Kama malalamiko yenu mnaojiita Waswahili ni kuhusu kubadilisha majina ya mitaa badala ya hata kuiboresha mitaa yenyewe likiwemo Soko la Kariakoo mimi namuunga mkono Spika Makinda kwa kauli yake juu yenu maana mnalalamikia mambo yasiyo na msingi!
Soma historia, upate somo, usepe, huna mchango wewe hapa!
 
Ahahahaha!huwa nakumbuka nikienda likizo mwaka mpya Kibosho tunakula Mbege na nguruwe tamu

Siyo lazima uende moshi kama shida yako ni kitimoto hata pale ikulu ya magogoni inaliwa kwa sana na mheshimiwa, kama uamini ili jiulize kwa nini hajawahi kwenda kuhiji macca?
 
Makinda amesema "watu wa k.koo''

Makinda amesema watu wa k.koo, Jumuiya ya Waswahili inasema yenyewe ndiyo iliyosemwa na kudharauliwa;

Logical conclusion ni kwamba Watu wa K.Koo ni Waswahili (you can use K.Koo and Waswahili interchangeably kwa mujibu wa mtoa hoja).
 
Makubwa! Historia ya Kariakoo na povu juu, jamaa kaandika mpaka basi. Ila kwa ninavyomfahamu Makinda, hataomba radhi abadan! Anajua waliompa u-Spika si watu wa Kariakoo!

mkuu alishaomba radhi na kufafanua pale bungeni
 
Ni vizuri na kama ni mtu timanu na mwenye haya na soni na aliyefundwa na kufundika na wazazi wake BASI ATABIDI Kwa hali zote zile AWAOMBE RADHI wakaazi wa Kariakoo.
 
Aisee mkuu nashukuru sana nimefaidi sana historia ya hapo Kariakoo. ipo siku nitatafuta zilipo hizo ofisi za TAA na nyingizezo ambapo vuguvugu la uhuru liliamzia. Nilivyomwelewa makinda hakutuna wakazi wa Kariakoo balia aliongelea vurugu za kule ndani ya soko hususani kule shimoni ambako hakuna utawala na kila mtu anaongea cha kwake bila kusikilizana. Naona wewe pamoja na historia nzuri ulikuwa tu unatafuta sehemu ya kutapikia nyongo yako pole sana.
 
Dhamira potofu hujidhihirisha kupitia mdomo. Dhamira ya huyu spika itajulikana kadri tunavyosonga mbele.
 
Back
Top Bottom