Jumuiya ya Waswahili Kariakoo wampa onyo Makinda na wenzake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jumuiya ya Waswahili Kariakoo wampa onyo Makinda na wenzake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mashadoplantan, Jun 14, 2011.

 1. m

  mashadoplantan Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  [​IMG]

  Mshairi Muyaka Al Ghassany (1776-1840 ) toka Mombasa aliwahi kusema hivi:

  Vita vyako Fahamu
  Havimdhuru Karimu
  Ila wewe Bahaimu
  Jujue Utaumia


  Katika hali isiyo ya kawaida Jumuiya ya wa Swahili Tanzania imemjia juu Spika Anne Makinda juu ya kauli yake ya kuwakebehi watu wa Kariakoo ambako wengi wao wana asili ya Kiswahili.

  Tamko rasmi la Jumuiya ya waswahili limekuja baada ya kauli ya makinda iliyojaa dharau na kebehi kwa wabunge kuwa wasiwe kama watu wa Kariakoo. Klabu ya Saigon nayo imesema itatoa tamko lao rasmi kesho juu ya haya matamshi machafu na ya dharau ya spika Anna Makinda.

  Anne Makinda labda alitakiwa kurudi darasani na akapigwe brash kuhusu umuhimu wa Kariakoo na watu waliowahi kuishi kariakoo na Makinda should know better than most kuwa hicho chama kilichomweka kwenye hicho kiti alichokalia kilizaliwa Kariakoo na na kusema ukweli ni kuwa dharau aliyoitoa Anna Makinda kwa kariakoo itakuwa si kwa wafanya bishara ndogo ndogo walipo pale bali ni pamoja na waswahili wengine kama akina Mwinjuma Mwinyikambi, Kiyate Mshume, Jumbe Tambaza, Sheikh Hassan bin Amir and Sheikh Suleiman Takadir ambao walikuwa ni wakaazi wa Kariakoo.

  Labda Makinda angeongea na wenzie wakampeleka maeneo ya makuu 4 yaliyoifanya kariakoo :

  1.Kariakoo

  2.Gerezani

  3.Kisutu

  4.Mission Quarter.

  Spika Anna angejua watu wa Katiakoo wameshiri vipi kwenye kwenye uhuru wa nchi hii asingeweza kuwatukana wabunge kwa dharau kama alivyofanya leo.

  Najua Makinda hawezi kumwomba ZUNGU au wabunge wengine wa Dar lakini sitoshangaa kuwa huyu mama akawa hajui hata hiyo TAA ilikuwa na makao makuu wapi na sacrifice zipi mzee Bin Sudi aliziingia kutoa lile jengo mwaka 1930!

  Anna kama ulijuwa hujui basi ujue kuwa jengo hili ndio TANU ilizaliwa na mpaka leo lipo pale mtaa wa kariakoo na Mtaa Mpya ulipoungana


  Kama ulikuwa hujui basi upande wa Magharibi wa Kariakoondiko ilikokuwa Mission Quarter (NYUMA YA TBL) na eneo hili lilitengwa maalim kwa ajili ya kuwalinda wahamiaji na waswahili waliokuwa wengi kariakoo na ambao waliishhi kwa amani na utulivu kwa miaka zaidi ya 70 mpaka leo hii ambako Pspika wa Bunge unatoa kauli zenye nia ya kuvunja amani na utulivu baina ya watu wa kariakoo

  Kwa kuonyesha kuwa Waswahili wa Kariakoo walikuwa hawana kinyongo ndio maana majina ya mitaa imebaki vile vile kama vile mtaa wa Masasi, Likoma, Ndanda, Muhonda, Muheza , Magila na sasa hivi mmetuletea jina la mpuuzi wenu yule (MAKAMBA) na mkampa mtaa jina ili hali hana lolote la maana linalomsabahisha na Kariakoo (when time will come TUTALIONDOA)

  Lakini wana JAMII FORUM msimlaumu sana huyu Anna Makinda kwani naye anafuata nyayo za baba yake Mwalimu Nyerere ambaye alianza kupandikiza mbegu mbaya za kudharau not only waswahili lakini wana kariakoo kwa ujumla.

  Watu wengine maarudu ambao walikuwa ni wana Kariakoo walikuwa wakazi wa MISSION QUATER ni babu yangu bwana THOMAS PLANTAN ambaye alikuwa ni rais wa African Association na al Marhum mzee JOHN RUPIA ambaye alikuwa ni tajiri mkubwa sana enzi zile.

  Anna Makinda kama hujui basi kwa taarifa yako tuu ni kuwa nyumba ya Al Marhum John Rupia ilikuwa mtaa wa Likoma na Magila, nyumba hii mpaka leo ipo na ndiko African Association ilianzishwa mwaka 1929. Nyumba hii mpaka leo ipo japi si katika hali yake ya zamani.

  Lakini pia nataka nikujulishe kuwa Mission Quarter ndiko kulikokuwepo kiwanda cha kuchapisha cha mwafrica wa kwanza ambacho kilikuwa cha mzee wangu MASHADO PLANTAN ambaye alikuwa ni mtu wa kusini na alikuwa anachapisha JAMII FORUM ya enzi hizo ilikuwa ikiitwa ZUHURA ambayo Nyerere alikuwa analitumia sana kupiga debe dhidi ya wakoloni!

  Lakini yote hayo Makinda kwako unaona ni upuuzi tuu kwani kariakoo pia ina eneo linaitwa GEREZANI ambako ilikuwa ni nyumbani kwa Omari Londo, Ally Sykes, Zuberi Mtemvu, Mashado Plantan, Muhsin Mende and Dossa Aziz. Hawa walikuwa ni majabali na wazalendo waliokutana na Nyerere baadae. Kwa kuonyesha tuu kuwa sisi si wafuata bendera, ZUBERI MTEMVU, MUHSIN MENDE na MASHADO PLANTAN waliamua kujiondoa TANU na kuanzisha chama kingine cha upinzani kwa jina la TANGNYIKA AFRICAN CONGRESS na hapo ndiko zilianza tofauti kubwa na baba yako Nyerere.

  Anna makinda unaposema waBunge wasiwe kama watu wa kariakoo unamaana hutaki wawe INDEPENDENT THINKERS kama akina Mzee Mshume Kiyate, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Idd Faizi, Idd Tosiri, Bantu Kasella Bantu, Abdulwahid Sykes and Dossa Aziz?

  Kwa kuendelea kukuambia tuu umuhimu wa kariakoo ni kuwa ile open space inayotazamana na viwanja vya Mnazi Mmoja ilikuwa ni plot ya JOHN RUPIA ambayo aliitoa kama zawadi kwa TANU ili wajenge ile centre. Of course kwa sababu ya serikali yako ilivyokuwa haithamini historia na heritage ili nyumba ilivynjwa wamejenga gorofa pale bila kuzingatia au kuweka kumbukumbu yoyote ile, na huyo baba yenu Nyeree mnaye sema kuwa mnahifadhi ujumbe wake historia kaye nyingi iliyokuwa mle ndani iliishia kutupwa bila mazingatio yoyote yale ya kuhifadhi yaliyokuwa mle.

  Sehemu nyingine ambayo leo hii umeitukana ni Soko la kariakoo ambalo Nyerere alikuwa haishi kwenda pale....bila kusahau kuwa hata shirika la masoko kariakoo lilikuwa linatoa SCHOLARSHIP kuwasomesha watu mpaka University of Dar.

  Leo Hii spika wa Bunge umeamua kuwatukana :

  WASHOMVI ambao walikuwa wanafanya baishara ya samaki

  WAZARAMO ambao walikuwa wanafanya baishara ya nazi

  WANYAMWEZI (wanawake) ambao walikuwa wanafanya baishara ya tumbaku kavu huku wanaume wakifanya biashara ya viazi ziliskukuwa zinalimwa Kigamboni

  WALUGURU walikuwa wanafanya biashara za machungwa na mboga za majani

  WAARABU walikukuwa wanafanya biashara ya ngano, mabucha ya nyama, na viungo mbali mbali

  WAHINDI walikuwa wanashindana sana na WAARABU kwenye biashara mbali mbali


  Je Anna Makinda unajua kama Nyerere aliwahi kufanya kazi soko la kariakoo kama Market Master? Je unajua kama ofisi yake ilikuwa kwenye junction ya mtaa wa Tandamti ( siku hizi mnauita mtaa wa Mshume Kiyate) na mtaa wa Swahili?

  Matusi uliyowatukana wana Kariakoo leo ni matusi ambayo umewatukana wa Swahili wa Mwembe Togwa (siku hizi mnapaita Fire), Umewatukana wakari wa Ronald Cameroon Road ( sikuhizi United Nations Road) na wengineo wengi...lakini wansiasa wenye calibre za wewe Anna Makinda ndio hao hao mlioamua kuquestion maamuzi ya mzee Kitwana Kondo alipokuwa meya mwaka 1995 alipoa mua kubadili jina la mtaa wa Tandamti na kuita mtaa wa Mshume Kiyate ...tena mlipiga makelele mkisaidiwa na waandishi wa habari ambao hawaijui historia ya kariakoo kwa kuuliza huyu Mshume Kiyate ni nani? Nyie nyie ndio mlilalamika mitaa mingine ya kariakoo ilipobadilishwa na kupewa majina ya Tatu Binti Mzee, Max Mbwana, Omari Londo halafu leo hii unathubutu kututukana sisi wana Kariakoo!

  Onyo kwa Anna Makinda na wanasiasa wenye tabia za kudharau watu wa kariakoo kama Cyrill Chami na wengineo, Wana Kariakoo na Waswahili wa zama hizi hatutonyamaza kwani vyombo vya kulalama tunavyo na haki zetu tunazijua na mkiendelea na dharau zenu basi mjue kuwa pamoja kuwa waswahili hatutonyamaza na kama ikiwezekana tujibu mapigo basi tutaangalia namna bora zaidi za kuwajibu lakini hatutokaa kimya...maana leo mmeanza na waswahili na watu wa kariakoo kesho tunajua mtahamia kwa wa chagga na watu wa Moshi kesho kutwa mtahamia kwa nyakyusa na watu wa Mbeya na Iringa

  Tofauti ni kuwa sasa tumelimika na tunaouwezo wa kuona mnapoanza kutuletea dharau bila kujali wakazi na watu wa kariakoo nao ni wapiga kura kama watu wa kwenu


  Muyaka al Ghassany pia alisema hivi:
  Yu wapi Firauni
  Yuwapi wapi Karuni
  Na Shadadi Maluuni
  Wote wameangamia


  Anna Makinda leo umeamua kuwatukana wana Kariakoo, historia ya Kariakoo na wanaotafuta rizki zao Kariakoo na Waswahili wanaoishi pale lakini ukae ukijua kuwa kuna leo na kesho na sisi hili hatutosahau. Mshazowea kututukana lakini at some point someone has to stand up and say no hatukubali. Labda umesahau kuwa kwa waswahili wa Kariakoo kuna 2 extremes ambazo naona ushazowea ile moja tuu
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Dah.......asante mdau nimejifunza history hapa.........akutukanae akuchagulii TUSI
   
 3. regam

  regam JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mh!kaaaaz kwelikweli!
   
 4. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Kelele zooooteeeeee hizo za wanakariakoo lakini uchaguzi ukija magamba ya kijani yanapata 100% of the vote. kazi ipo
   
 5. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  wanakuwa kama hawaoni mbali,lakini wamsamehe yule mama kwani naona kama amelemewa na ile kazi
   
 6. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Huyo mama anahitaji aombe msamaha na afute kauli yake.
   
 7. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  [​IMG]


  Kama kwa picha iliyopostiwa ndio reflection ya jamii ya waswahili, basi ni heri Mama Makinda wala asithubutu kuomba radhi.
  Yaani mnataka Bunge liwe na marap rap ya kiswahili kama hayo?
   
 8. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mwaka huu mmeshikwa pabaya mtatafuta mchawi msimpate, naona mnaokoteza hoja za kulazimisha. Kila mtu hata anayekaa kariakoo anajua kuwa neno kariakoo limenasibishwa na soko na hata mitaani linavyotumika ni sawa na soko. Sasa hao wahuni wanaotaka kufananisha bunge na soko/ kariakoo wasitafute upenyo kuficha uozo wao kwa kupitia hoja hii isiyo na mashiko. Kwa kuwa ninyi ndio think tank yao waambieni dawa ni ku behave kama wawakilishi wa wananchi na wala sio wauza kahawa wa Saigoni ambao hawabanwi na sheria wala kananuni kuongea utumbo.
   
 9. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kariakoo wacha watukanwe ni wao ndo walijifanya ccm damu wakat wa uchaguzi sasa hii ndo shukran ya punda...
   
 10. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Bonge la historia ya kariakoo iliyoandaaliwa kwa weledi wa hali ya juu. Toa nakala kwenye gazeti kama inawezekana ili wengine kama Makinda ambao ni waoga wa kushindana kwa hoja na hawana ujanja wa kuja JF waone hiyo historia na kuipa Kariakoo heshima inayostahili.
   
 11. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu unichambulia hiyo kariakoo mpaka nimejiskia poa hongera mkubwa unaweza ukaendlea na nyingine muheshimiwa
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Watu wengine bana!!

  1) nini maana ya colours ulizotumia?
  2) nini essence ya kuuliza kama watu wanajua nyumba ya sijui nani na nanizilipokuwa?
  3) Mitaa ya kariakoo na ubadilishwaji wake una maana gani hapa?

  Unajua lugha ya picha wewe!!!! oooh!! sykes, sijui Shamte sijui Rupia..............ili iweje?

  Utamaduni wa kulalamika kuonewa hata kwenye mambo yasiyo na maana ni jambo baya sana!!

  Nakubali kuwa matumizi ya maneno kama haya sio mazuri, na natambua kwamba yanaweza kutafsiriwa vibaya, na the fact kwamba Makinda labda anahitaji kufundishwa Communication Skills.

  Pia usisahau Makamba alishawahi kusema same thing!!
   
 13. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,293
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kwa sababu wengi wao ni waislamu wao ni cuf na ccm tu. Waache watukanwe mpaka kwenye misuli.
   
 14. M

  MAURIN Senior Member

  #14
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mama hafai kuwa spika wa bunge la TANZANIA,yeye na serikali yake ya CCM wanadharau kwa wananchi wa TANZANIA,ILA MWISHO UMEFIKA
   
 15. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,612
  Trophy Points: 280
  duh...!!mkweli aombe msamaha.
   
 16. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Nenda kawaambie waliokutuma wajipange upya, tamko halifanani na makala za Lula mwana nzela, andika hapo jina na tarehe kisha utueleze hiyo jumuiya ya waswahili unawaowaita wa kariakoo ilisajiliwa na mamlaka gani hapa nchini.
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  Tena huyu mama katukosea vibaya sana. Anashangaza! Khaa, haoni haya wala hajui vibaya!

  Mengi kayasema Mashado, mimi sina zaidi ila namuandikia barua rasmi huko huko bungeni atuombe radhi.
   
 18. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Jamani eeh! sasa hivi ni zmu ya akina mama!!!
  Mwenyekiti wa chama alisema!
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Anna Makinda is a disgrace to all clear thinking Tanzanians.
   
 20. J

  Jombi Jombii Senior Member

  #20
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 186
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Bibi Makinda anachemka kila eneo lakini yote ni jazba yake kwa mambo ambayo angeweza kutoa maagizo bila kuropoka.Nadhani alimaanisha zile patashika za wafanyabiashara wa sokoni kariakoo wakati wa kuuza na kununua ambapo kila mtu anaongea bila mpangilio.MSAMEENI BURE WALIOMPONZA NI WALIOMSHAWISHI ACHUKUE NAFASI YA BOSI WAKE
   
Loading...