Jumuiya ya Waswahili Kariakoo wampa onyo Makinda na wenzake

ukitazama picha..hiyo ndiyo kariakoo anayoidhania spika Makinda lakini kwa mtazamo wa Mashado(nami namuunga mkono), kariakoo ni zaidi ya huo mtazamo finyu wa spika Makinda, na alichokieleza Mashado ndiyo maana pana ya kariakoo.

Asante sana Mashado....bahati mbaya sana kwa nchi yetu, historia ni kitu cha kupuuzwa(si unaona hata ile sikukuu ya mashujaa walishaifuta!)

Kwa spika Makinda ni aibu kwake kuongea bila kufikiri au kwa lugha ya sasa kuropoka(ukipenda kukurupuka)...ulitegemea asiwe ni mtu wa hivyo lakini ndiyo chaguo letu, tutafanyaje, vinginevyo tungempinga na sasa asingekuwa pale.

Mi nadhani wakubwa wajifunze kufikiri kabla ya kuongea, zile zama za UMC(msema chochote) zimepita, kila kauli itaangaliwa na kupimwa katika 3D, wengi wataangushwa kwa kauli tu na wakati utathibitisha.

Nawakilisha!

Naam Mkuu ukiwa Kiongozi ni lazima uwe makini sana kila unapotoa kauli na siyo kutoa kauli za kukurupuka ili kuhakikisha kwamba hutoi kauli ambazo zina athari ya kudhalilisha kwa namna moja au nyingine wale unaowaongoza. Huyu mama inabidi aombe samahani haraka sana au akichelewa sana hata hiyo samahani yake itakuwa haina maana
 
Mimi Kwa Mtazamo wangu na ushauri wangu ni kwa Viongozi Wetu, Wajue wao ni Vioo Vya Jamii, Neno lolote watakalozungumza LAZIMA walipime na kutafakari kabla ya kuzungumza, Viongozi wetu wengi wao ni Waropokaji halafu Mwisho wa siku wanakuja kujilaumu kwa Kauli zao, tukumbuke hata MAKAMBA na Viongozi wengine walitamka, wanatamka Kauli kama hizi zenye Utata, Makinda angekuwa MTU, RAIA wa kawaida bila Cheo Kikubwa watu wasingekasirishwa na Kauli yake, Mwisho wa siku amekosea na Shurti afute Kauli yake na ufafanuzi JUU, na iwe Fundisho kwa Watawala wengine kuchunga Midomo yako na Jeuri ya Vyeo Vyao.
Nawakilisha
 
Naam Mkuu ukiwa Kiongozi ni lazima uwe makini sana kila unapotoa kauli na siyo kutoa kauli za kukurupuka ili kuhakikisha kwamba hutoi kauli ambazo zina athari ya kudhalilisha kwa namna moja au nyingine wale unaowaongoza. Huyu mama inabidi aombe samahani haraka sana au akichelewa sana hata hiyo samahani yake itakuwa haina maana
hata asipoomba samahani unadhani kutakuwa na effecs zozote? As long as ni wa kijani na magamba wana Kariakoo sio big deal kwao. Lakini kauli hii ingetoka kwenye magwanda ya khaki saa hizi ungesikia matusi kila kona
 
Kuna jambo linaendelea ndani ya jamii yetu ambalo silielewi. Kwanza watu wamekuwa too sensitive, pili wamekuwa refractory and volatile. Tatu kumekuwa na utamaduni wa kunasaibisha mambo hata kama hayafanani, na hapa JF watu kuwa sensational.
Wiki moja iliyopita nilitoa tahadhari kwa wanJF( out of proportional and blown up) kwa suala la Jk na maaskofu, sijui hili ni jambo jipya au ni mwendelezo.

Mkenya anasema kuja hapa, mkurya anasema nataka(sio naomba), makinda kasema watu wa kariakoo.
Ni kweli viongozi wapime kauli zao kabla ya kuzitoa, pengine angesema bunge lisiwe kama sokoni au bunge lisiwe kama soko la kariakoo, lakini kusema watu wa kariakoo ina maana tata.
Hapa ni kumwambia awe mwangalifu na kauli zake tukijua yapo mapungufu ya kibinadamu kama ya marehemu Ditopile aliyewahi kusema watu wa bara hawajui kula chapati.
mashadoplantan;2100487.................... waswahili wengine kama akina Mwinjuma Mwinyikambi, Kiyate Mshume, Jumbe Tambaza, Sheikh Hassan bin Amir and Sheikh Suleiman Takadir ambao walikuwa ni wakaazi wa Kariako
Nadhani ametumia present tense na hili linawahusu wakazi wote wa kariakoo kwa leo hii, kama alitumia past tense maelezo yako yanabaki kuwa sahihi.
eneo hili lilitengwa maalim kwa ajili ya kuwalinda wahamiaji na waswahili.Kwa kuonyesha kuwa Waswahili wa Kariakoo walikuwa hawana kinyongo ndio maana majina ya mitaa imebaki vile vile kama vile mtaa wa Masasi, Likoma, Ndanda, Muhonda, Muheza , Magila na sasa hivi mmetuletea jina la mpuuzi wenu yule (MAKAMBA) na mkampa mtaa jina ili hali hana lolote la maana linalomsabahisha na Kariakoo (when time will come TUTALIONDOA
)Kwa ufahamu wangu watu wanaoongea kiswahili tunawaita waswahili, ndio maana watu kutoka bara enzi hizo walikuwa hawajui kiswahili ima fasaha au kabisa, walipokutana na wanaoongea kiswahili wakawa wanawaita waswahili. Ndugu Mashado pengine ni kwa ufahamu wangu mdogo, hebu tufafanulie waswahili waliopo kariakoo ambao wamechukizwa na kauli ya spika ni watu gani (ni kabila, ukoo) na tuwatambueje.
Kuhusu kubadili majina historia inaonyesha mameya wote wa Dar kuanzia uhuru hadi 2005 ni wakazi wa kariakoo au walichaguliwa kwa ushawishi wa kariakoo. Madwani wengi wa jiji wamo wa karikoo, na majina yanatolewa na madiwani wa jiji. Hayo majina ya Makamba au Mkapa yametokea wakati Meya akiwa Kleist Syskes mwenye unasaba na Abdulwahid Syskes. Sijui kwanini madiwani na meya wao waliamua kutoa majina hayo wakiijua fika historia ya kariakoo na kwanini walaumiwe watu wengine kwa kile kilichofanywa na wakariakoo!
Of course kwa sababu ya serikali yako ilivyokuwa haithamini........... na huyo baba yenu Nyerere
Baba yao nani? Nyerere alikuwa kiongozi wa taifa hili kwa miaka 23, sasa tufafanuliye alikuwa baba yao akina nani tofauti na Watanzania.
Leo Hii spika wa Bunge umeamua
kuwatukanaWASHOMVI,WAZARAMO,WANYAMWEZI,WALUGURU,WAARABU,HINDI walikuwa wanashindana sana na WAARABU
Hawa ndio waswahili uliomaanisha hapo awali au kundi hili kwa ujumla liitweje
Matusi uliyowatukana wana Kariakoo leo ni matusi ambayo umewatukana wa Swahili wa Mwembe Togwa (siku hizi mnapaita Fire), Umewatukana wakari wa Ronald Cameroon Road ( sikuhizi United Nations Road) na ...........mzee Kitwana Kondo alipokuwa meya mwaka 1995 alipoa mua kubadili jina la mtaa wa Tandamti na kuita mtaa wa Mshume Kiyate ...tena mlipiga makelele mkisaidiwa na waandishi wa habari ambao hawaijui historia ya kariakoo kwa kuuliza huyu Mshume Kiyate ni nani? Nyie nyie ndio mlilalamika mitaa mingine ya kariakoo ilipobadilishwa na kupewa majina ya Tatu Binti Mzee, Max Mbwana, Omari Londo
mnapaita.,'Nyie nyie', Je mnapaita ni akina nani, na nyie nyie ni wapi hao?kwani Mashado mgogoro huu ni akina nani dhidi ya wanani
?.........pamoja kuwa waswahili.atutokaa kimya...maana leo mmeanza na waswahili na watu wa kariakoo kesho tunajua mtahamia kwa wa chagga na watu wa Moshi kesho kutwa mtahamia kwa nyakyusa na watu wa Mbeya na Iringa
Kwani mchagga au mnyakyusa aliyeishi kariakoo tangu mwaka 1948 hawezi kuwa mswahili!!
Lakini wana JAMII FORUM msimlaumu sana huyu Anna Makinda kwani naye anafuata nyayo za baba yake Mwalimu Nyerere ambaye alianza kupandikiza mbegu mbaya za kudharau not only waswahili lakini wana kariakoo kwa ujumla
Kuna thread ambayo baadhi ya wachangiaji wamemtuhumu Nyerere kwa ukabila na udini. Katika jitihada za kuweka kumbukumbu sawa na kuelemishana baadhi yetu tumeomba ufafanunuzi au ushahidi wa madai hayo, nadhani watoa tuhuma bado wanatafakari, sasa na hili sijui unaweza kulitolea ushahidi wa jinsi mwl alivyodharau waswahili na alivyopandikiza chuki. Nitashukuru tafadhali.
 
mimi sioni kosa la anna makinda, kwa sababu ushaidi upo, vibaka wote wapo kariakoo, watu wa porojo wasio na kazi za kufanya wapo kariakoo, nyumba mbovu na duni zipo kariakoo, mashoga wapo kariakoo.
Sasa aombe radhi ya nini? Au kwa sababu ni mkristo? Mbona ikulu kule kuna wavuta bange wa kumwaga tu kwenye eneo la feri ambapo ni opposite na makao ya rais?
Nasisitiza spika ni mtu mkubwa hawezi kushinikizwa na kikundi cha wanywa kahawa kama huyu alieleta mada hii.

mdini mdini wewe!
 
Hata kama wenyeji wa kariakoo wengi wenu mmeuza nyumba zenu kwa matajiri waliovunja na kuvurumisha magorofa lakini bado hakupaswa kuwatukana kama kweli alimaniisha wenyeji na sio wapiga debe wa kariakoo na wauzaji sokoni
 
Hapo ndipo tofauti ya lugha iwepo baina ya kiongozi na mtu wa kawaida.

Hata Kama watu wote wanafahamu Kariakoo inamaanisha sokoni, kiongozi hapaswi kutumia assumption hiyo kwa vile kuna watu wana asili na Kariakoo na inaweza kuleta maana mbaya kwao.

Juzi Mkandara aliuliza kwanini wanachadema wanadharau Waislam kwa kutumia neno 'madrasa'...wakati kimsingi 'madrasa' ni neno zuri tu na pia ni character ambayo waislam wanatakuwa kuwa nayo (elimu ya madras)

Kabla ya hapo tuliwahi kujadiliana kuwa ni dharau kuwaita Wahindi 'wadosi' japokuwa dosti linamaana njema.

Kwa hiyo tunatarajia kiongozi asitumie maneno Kama "biashara ya umachinga" na mengineyo kama "anapenda pesa kama Mchagga/Mpemba" na kadhalika

Ongezea na hii: Mmarekani mwenye asili ya Afrika namwita mwenzake Nigger na haileti shida, ila mzungu akilitumia hili jina kumwita mweusi ni utata mtupu.
 
Mimi sioni kosa la Anna Makinda, kwa sababu ushaidi upo, vibaka wote wapo kariakoo, watu wa porojo wasio na kazi za kufanya wapo kariakoo, nyumba mbovu na duni zipo kariakoo, mashoga wapo kariakoo. Sasa aombe radhi ya nini? au kwa sababu ni mkristo? mbona ikulu kule kuna wavuta bange wa kumwaga tu kwenye eneo la feri ambapo ni opposite na makao ya Rais? Nasisitiza Spika ni mtu mkubwa hawezi kushinikizwa na kikundi cha wanywa kahawa kama huyu alieleta mada hii.
Ha ha ha ha ha ha ha,"Eti kikundi cha wanywa kahawa" mbavu zangu mie!!
 
Tena huyu mama katukosea vibaya sana. Anashangaza! Khaa, haoni haya wala hajui vibaya!

Mengi kayasema Mashado, mimi sina zaidi ila namuandikia barua rasmi huko huko bungeni atuombe radhi.
Makinda kakosea wapi?wewe huoni kuna tatizo kwa Kariakoo?
Makinda kwa hili nampa hongera
 
dar-es-salaam-tanzania-inside-the-kariakoo-market.jpg
Katika hali isiyo ya kawaida Jumuiya ya wa Swahili Tanzania imemjia juu Spika Anne Makinda juu ya kauli yake ya kuwakebehi watu wa Kariakoo ambako wengi wao wana asili ya Kiswahili.Tamko rasmi la Jumuiya ya waswahili limekuja baada ya kauli ya makinda iliyojaa dharau na kebehi kwa wabunge kuwa wasiwe kama watu wa Kariakoo. Klabu ya Saigon nayo imesema itatoa tamko lao rasmi kesho juu ya haya matamshi machafu na ya dharau ya spika Anna Makinda.Anne Makinda labda alitakiwa kurudi darasani na akapigwe brash kuhusu umuhimu wa Kariakoo na watu waliowahi kuishi kariakoo na Makinda should know better than most kuwa hicho chama kilichomweka kwenye hicho kiti alichokalia kilizaliwa Kariakoo na na kusema ukweli ni kuwa dharau aliyoitoa Anna Makinda kwa kariakoo itakuwa si kwa wafanya bishara ndogo ndogo walipo pale bali ni pamoja na waswahili wengine kama akina Mwinjuma Mwinyikambi, Kiyate Mshume, Jumbe Tambaza, Sheikh Hassan bin Amir and Sheikh Suleiman Takadir ambao walikuwa ni wakaazi wa Kariakoo.Labda Makinda angeongea na wenzie wakampeleka maeneo ya makuu 4 yaliyoifanya kariakoo : 1.Kariakoo 2.Gerezani 3.Kisutu 4.Mission Quarter. Spika Anna angejua watu wa Katiakoo wameshiri vipi kwenye kwenye uhuru wa nchi hii asingeweza kuwatukana wabunge kwa dharau kama alivyofanya leo. Najua Makinda hawezi kumwomba ZUNGU au wabunge wengine wa Dar lakini sitoshangaa kuwa huyu mama akawa hajui hata hiyo TAA ilikuwa na makao makuu wapi na sacrifice zipi mzee Bin Sudi aliziingia kutoa lile jengo mwaka 1930!Anna kama ulijuwa hujui basi ujue kuwa jengo hili ndio TANU ilizaliwa na mpaka leo lipo pale mtaa wa kariakoo na Mtaa Mpya ulipoungana Kama ulikuwa hujui basi upande wa Magharibi wa Kariakoondiko ilikokuwa Mission Quarter (NYUMA YA TBL) na eneo hili lilitengwa maalim kwa ajili ya kuwalinda wahamiaji na waswahili waliokuwa wengi kariakoo na ambao waliishhi kwa amani na utulivu kwa miaka zaidi ya 70 mpaka leo hii ambako Pspika wa Bunge unatoa kauli zenye nia ya kuvunja amani na utulivu baina ya watu wa kariakoo Kwa kuonyesha kuwa Waswahili wa Kariakoo walikuwa hawana kinyongo ndio maana majina ya mitaa imebaki vile vile kama vile mtaa wa Masasi, Likoma, Ndanda, Muhonda, Muheza , Magila na sasa hivi mmetuletea jina la mpuuzi wenu yule (MAKAMBA) na mkampa mtaa jina ili hali hana lolote la maana linalomsabahisha na Kariakoo (when time will come TUTALIONDOA)Lakini wana JAMII FORUM msimlaumu sana huyu Anna Makinda kwani naye anafuata nyayo za baba yake Mwalimu Nyerere ambaye alianza kupandikiza mbegu mbaya za kudharau not only waswahili lakini wana kariakoo kwa ujumla.Watu wengine maarudu ambao walikuwa ni wana Kariakoo walikuwa wakazi wa MISSION QUATER ni babu yangu bwana THOMAS PLANTAN ambaye alikuwa ni rais wa African Association na al Marhum mzee JOHN RUPIA ambaye alikuwa ni tajiri mkubwa sana enzi zile.Anna Makinda kama hujui basi kwa taarifa yako tuu ni kuwa nyumba ya Al Marhum John Rupia ilikuwa mtaa wa Likoma na Magila, nyumba hii mpaka leo ipo na ndiko African Association ilianzishwa mwaka 1929. Nyumba hii mpaka leo ipo japi si katika hali yake ya zamani.Lakini pia nataka nikujulishe kuwa Mission Quarter ndiko kulikokuwepo kiwanda cha kuchapisha cha mwafrica wa kwanza ambacho kilikuwa cha mzee wangu MASHADO PLANTAN ambaye alikuwa ni mtu wa kusini na alikuwa anachapisha JAMII FORUM ya enzi hizo ilikuwa ikiitwa ZUHURA ambayo Nyerere alikuwa analitumia sana kupiga debe dhidi ya wakoloni!Lakini yote hayo Makinda kwako unaona ni upuuzi tuu kwani kariakoo pia ina eneo linaitwa GEREZANI ambako ilikuwa ni nyumbani kwa Omari Londo, Ally Sykes, Zuberi Mtemvu, Mashado Plantan, Muhsin Mende and Dossa Aziz. Hawa walikuwa ni majabali na wazalendo waliokutana na Nyerere baadae. Kwa kuonyesha tuu kuwa sisi si wafuata bendera, ZUBERI MTEMVU, MUHSIN MENDE na MASHADO PLANTAN waliamua kujiondoa TANU na kuanzisha chama kingine cha upinzani kwa jina la TANGNYIKA AFRICAN CONGRESS na hapo ndiko zilianza tofauti kubwa na baba yako Nyerere.Anna makinda unaposema waBunge wasiwe kama watu wa kariakoo unamaana hutaki wawe INDEPENDENT THINKERS kama akina Mzee Mshume Kiyate, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Idd Faizi, Idd Tosiri, Bantu Kasella Bantu, Abdulwahid Sykes and Dossa Aziz?Kwa kuendelea kukuambia tuu umuhimu wa kariakoo ni kuwa ile open space inayotazamana na viwanja vya Mnazi Mmoja ilikuwa ni plot ya JOHN RUPIA ambayo aliitoa kama zawadi kwa TANU ili wajenge ile centre. Of course kwa sababu ya serikali yako ilivyokuwa haithamini historia na heritage ili nyumba ilivynjwa wamejenga gorofa pale bila kuzingatia au kuweka kumbukumbu yoyote ile, na huyo baba yenu Nyeree mnaye sema kuwa mnahifadhi ujumbe wake historia kaye nyingi iliyokuwa mle ndani iliishia kutupwa bila mazingatio yoyote yale ya kuhifadhi yaliyokuwa mle.Sehemu nyingine ambayo leo hii umeitukana ni Soko la kariakoo ambalo Nyerere alikuwa haishi kwenda pale....bila kusahau kuwa hata shirika la masoko kariakoo lilikuwa linatoa SCHOLARSHIP kuwasomesha watu mpaka University of Dar.Leo Hii spika wa Bunge umeamua kuwatukana :WASHOMVI ambao walikuwa wanafanya baishara ya samakiWAZARAMO ambao walikuwa wanafanya baishara ya naziWANYAMWEZI (wanawake) ambao walikuwa wanafanya baishara ya tumbaku kavu huku wanaume wakifanya biashara ya viazi ziliskukuwa zinalimwa KigamboniWALUGURU walikuwa wanafanya biashara za machungwa na mboga za majani WAARABU walikukuwa wanafanya biashara ya ngano, mabucha ya nyama, na viungo mbali mbaliWAHINDI walikuwa wanashindana sana na WAARABU kwenye biashara mbali mbaliJe Anna Makinda unajua kama Nyerere aliwahi kufanya kazi soko la kariakoo kama Market Master? Je unajua kama ofisi yake ilikuwa kwenye junction ya mtaa wa Tandamti ( siku hizi mnauita mtaa wa Mshume Kiyate) na mtaa wa Swahili?Matusi uliyowatukana wana Kariakoo leo ni matusi ambayo umewatukana wa Swahili wa Mwembe Togwa (siku hizi mnapaita Fire), Umewatukana wakari wa Ronald Cameroon Road ( sikuhizi United Nations Road) na wengineo wengi...lakini wansiasa wenye calibre za wewe Anna Makinda ndio hao hao mlioamua kuquestion maamuzi ya mzee Kitwana Kondo alipokuwa meya mwaka 1995 alipoa mua kubadili jina la mtaa wa Tandamti na kuita mtaa wa Mshume Kiyate ...tena mlipiga makelele mkisaidiwa na waandishi wa habari ambao hawaijui historia ya kariakoo kwa kuuliza huyu Mshume Kiyate ni nani? Nyie nyie ndio mlilalamika mitaa mingine ya kariakoo ilipobadilishwa na kupewa majina ya Tatu Binti Mzee, Max Mbwana, Omari Londo halafu leo hii unathubutu kututukana sisi wana Kariakoo!Onyo kwa Anna Makinda na wanasiasa wenye tabia za kudharau watu wa kariakoo kama Cyrill Chami
Hivi hii mada inahusu kauli ya Mh Spika Makinda pekee au kuna jambo limefichwa hapa? Mambo ya Nyerere, Chami, John Rupia, Sykes yanaingiaje hapa? Kama malalamiko yenu mnaojiita Waswahili ni kuhusu kubadilisha majina ya mitaa badala ya hata kuiboresha mitaa yenyewe likiwemo Soko la Kariakoo mimi namuunga mkono Spika Makinda kwa kauli yake juu yenu maana mnalalamikia mambo yasiyo na msingi!
 
Duh! Ivi kumbe ukiisema Kariakoo unakuwa umewasema Waswahili. Kwa hiyo ukisema neno 'waswahili bwana wana matatizo' unakuwa umekisema kikundi cha watu flani.

Hata ukisema
1. Uswahilini kuna vituko!
2. Acha uswahili bwana!
3. Mbona unakuwa mswahili?
4. Mi sipendi mambo ya uswahili?
5. Fanya masaa ya kizungu sio ya kiswahili!
6. Jamaa ni mswahili mswahili?
7. Kuishi na waswahili taabu kweli!

Hapa ujiandae kupokea tamko la Waswahili.

Hili tamko naona lilikuwa standby, likisubiri siku limwangukie mtu tena wa imani flani kwa sababu sikuliona wakati ule alipolitamka mmoja wetu (McGamba) kipindi cha kampeni za uchaguzi.

Halafu mbona tamko lenyewe limekaa kama tamko la mswahili mmoja aliyeamua kuipa uhai kuonekana ni msimamo wa wengi? Sioni msemaji wa hao Waswahili, Mwenyekiti wa Waswahili, tamko limetolewa katika mkutano uliofanyika wapi na saa ngapi.

Tumeshajifunza, hii nchi haitachukuliwa na watu waliotumia muda mwingi kusoma madrasa. Mnaenda kujifunza chuki, visasi na matusi.
 
hawa jamaa ni JUMUIYA YA WASWAHILI
hivi mtu akikuita msahili unajisikiaje
mimi sitaki hapa JF tuleteane mambo ya kiswahili

Hawa ndio wanaohongwa ghahawa wanauza kura
MAKINDA HONGERA
 
Tena huyu mama katukosea vibaya sana. Anashangaza! Khaa, haoni haya wala hajui vibaya! Mengi kayasema Mashado, mimi sina zaidi ila namuandikia barua rasmi huko huko bungeni atuombe radhi.
Hongera Faidha sasa nimetambua kwamba kumbe wakati mwingine unapinga hoja makusudi, nashangaa leo umekubali kwamba kweli tumetukanwa, nakuhitaji na kwenye hoja zenye mashiko kwa taifa usinganganie umagamba tusimame pamoja kama wapenda haki
 
Duh!
Niliposikia Speaker akisema wabunge waache kuwa kama watu wa Kariakoo, niliwaambia wenzangu " haya maneno aliyoyasema spika....tusubiri kasheshe maana watu hawakawii kujibu"and I was right!

1. Zama hizi za watu kuwa sensitive kuliko kawaida, kiongozi lazima apime kina neno alitoalo mdomoni maana laweza kuleta mlipuko kuliko wa mabomu ya Mbagala.

2. JF nayo sasa imegeuka platform ya kukuza au kuchochoea milipuko na chuki za kidini na hata ukabila.Kuna watu wakiona kitu hata kama ni kidogo namna gani watakikuza kwa kukileta hapa kijadiliwe. Wanaojadili nao HAWAPIMI nini cha kusema maana usiri wa identity unawapa ngao kusema chochote.

Swali - JE SIYO WAKATI MUAFAKA KUJITAFAKARI NA KUONA KUWA TANZANIA TUNA MATATIZO MAKUBWA YA KUPAMBANA NAO - UMASIKINI ULIOIGUBIKA NCHI NA SIYO NANI ANAAMINI NINI?

KIPAUMBELE KATIKA MAPAMBANO YETU NI NINI? HATA VITA INAKUWA NA MKAKATI.HUWEZI KUPAMBANA BILA KUMJUA ADUI YAKO HASA NI NANI! WATANZANIA BWANA! ( NISIJE KUSEMA WASWAHILI BWANA NIKAAMBULIA KIPIGO CHA MBWA MWIZI! LOL)

Wakati tunapoteza nguvu kupigana kidini na kikabila, wajanja wako busy kupora utajiri wa nchi, fursa na rasilimali.INASHANGZA SANA!
 
dar-es-salaam-tanzania-inside-the-kariakoo-market.jpg



Kama kwa picha iliyopostiwa ndio reflection ya jamii ya waswahili, basi ni heri Mama Makinda wala asithubutu kuomba radhi.
Yaani mnataka Bunge liwe na marap rap ya kiswahili kama hayo?

hawa ndio wanowalipa "Posho" waliopo huko mjengoni!
 
Kuitwa mswahili wa Kariakoo sio tusi,kama mtoa hoja alivyoelelzea,waanzilishi wa Taifa hili waliishi na kufanya harakati zao katika maeneo ya Kariakoo.Vyama vya TAA,TANU,Congress vilizaliwa Kariakoo.Kwa sasa Kariakoo ni business district,biashara za kila aina zinafanyika pale na watu mbali mbali.
 
Nimepita mda si mrefu pale kariakoo nikakuta baadhi ya watu wanaangalia kama kuna uwezekenao wa kumburuza mahakamani Spika Makinda kwa madai ya kuwatukana, na wengine wanataka kuandamana kupinga kauli yake aliyoitoa bungeni kwa wabunge akiwaasa waache kujidharau kwa kufanya mambo hovyohovyo mithili ya watu walioko Kariakoo Dar es Salaam. "Huyu mwanamke amevuka mipaka ameacha kushughulika na bunge ameamua kupolomosha matusi dhidi yetu tumemkosea nini?" Analalamika mfanya biashara mmoja
 
Back
Top Bottom