CCM Music
JF-Expert Member
- Dec 5, 2018
- 1,036
- 1,782
Hizi ndio nyakati bora kabisa za kuunganisha nguvu. Hapa nalenga watu waaminifu pekee.
Dunia ya sasa inawatesa sana watu waaminifu. Kila aina ya baya ama ovu linalofanyika waathirika wakubwa ni watu waaminifu.
Kuanzia utapeli, kuumizwa moyo kimahusiano, kibiashara, kikazi, kimasomo, kiuchumi kwa ujumla wake, kidini, na kimaisha kiujumla wahanga wakubwa ni watu waaminifu.
Maisha yanazidi kuwa magumu kwa sababu watu waaminifu wamekuwa adimu sana. Wapo lakini ni waaminifu mioyoni mwao pekee. Watu wasio waaminifu wanawaumiza sana watu waaminifu kwa namna isivyoelezeka.
Watu hawasaidiani tena kwa sababu ya kukosekana uaminifu baina ya watu. Na hivi ndivyo maisha yanakuwa magumu kuliko kawaida .Kama hakuna tena kusaidiana tafsiri yake ni kwamba maisha yataendelea kuwatesa watu tofauti na kusudio la Mungu ambapo alitaka watu wafurahie maisha yao na wamtukuze Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi.
Kwa msingi huo, kuna haja kubwa sana ya kuunda Jumuiya ya siri ya watu waaminifu likiwa na lengo moja tu: 'Kushikamana pamoja kukabili changamoto za kimaisha eneo la kiuchumi, kiafya na kijamii kwa ujumla'.
Jumuiya hii itaendeshwa kwa mithili ya ki freemason (ila sio freemason). Yenyewe, ni Jumuiya ya siri inayoamini katika uaminifu, na haitasajiliwa popote duniani.
Wanajumuiya hawa wataunganishwa na falsafa moja tu ya 'Waaminifu wanapaswa kuishi maisha bora kwa sababu ya uaminifu wao'. Hivyo ni jukumu la wanajumuiya kupigania maslahi ya wanajumuiya kwa nguvu zote katika uaminifu wao.
Kutakuwa na kiapo kikali sana kwa wale watakaofuzu kuingia katika Jumuiya maana kuna hatua kuu tatu za kupitia ndipo uwe mwanajumuiya kabili.
Kuna ngazi ya Bronze, halafu inafuata ya Silver na ya mwisho ni ngazi ya Dhahabu. Ngazi ya Dhahabu ndio ya juu zaidi na ndio ya mwisho.
Kufikia ngazi ya Dhahabu kunakuwepo na kiapo kikali sana mithili ya hiki hapa:
(Na ndio maana juzi nilileta uzi nikitafuta kiapo kikali kuliko chote ili kitumike katika Jumuiya hii)
Kama kuna jamii ya watu wanaounganishwa kwa kumuamini Mtumishi fulani wa Mungu, ama kuna watu wanaounganishwa kwa mapenzi yao juu ya mpira, ama kwa imani yao juu ya mapenzi ya jinsia moja, na vyovyote vile, Je, ni kitu gani kitakachoshindikana kuwaunganisha watu kwa 'Uaminifu' wao?
Naombeni sana mni challenge katika hili.
Na zaidi nakaribisha rasmi maombi ya watu waaminifu kujiunga katika Jumuiya hii.
Idadi ya wanachama ni limited

Kile kiapo cha damu hiki hapa
WRITTEN IN BLOOD I act this spell upon you From my whole heart Wishing you to never rest No eat no sleep the rest part of your life I hope your will waste away And I hope you will never spend another penny I ought to have WISHING THIS FROM MY WHOLE HEART Haya ni maneno mabaya mno! Ni spell...
www.jamiiforums.com