Jumuiya ya siri ya Watu Waaminifu - The Secret Society of Trustful Men (TSSTM)

Coverage yake ni kias gan, tz pekee? east Africa? Africa nzima? Dunia nzima??
 
Nafuatilia Uzi kwa umakini mkubwa mnoo

Jamani endeleeni kuuliza maswali
Yeah, doors are open nimewaomba watu wani challenge kuhusu hii Jumuiya. Wani challenge kwa nguvu sana.

Japo, nakiri kwamba namna wanajumuiya watakavyonufaika sikupenda kuweka hadharani hapa, hio itakuwa ni moja ya kiapo kikali sana na siri kubwa sana ya wanajumuiya, lakini watanufaika na kunufaika na kunufaika na kunufaika.

Lazima watu waaminifu wastawi katika maisha waliopewa na Mungu wao
 
lutoki

Kipaumbele no. 1 ya Jumuiya hii ni kuimarisha uchumi wa wanachama wa wanachama wake.

Coverage inaanzia sehemu na kusambaa taratibu kwa kadri tutakavyoona inafaa.
 
Hiki kikundi kinachotajwa na mleta mada hakina tofauti na GREEN GUARD
 
TheLobbyist sasa kama ni jumuiya ya watu waaminifu mnafanyaje kiapo tena? Kwasabu natumaini vigezo moja wapo nikua mwaminifu beyond reasonable doubt, sasa mkishaaminiana kuna haja gani ya kiapo kikali?
Na kwanini kuwe na ranks? Uaminifu una viwango?
 
Kwa msingi huo, kuna haja kubwa sana ya kuunda Jumuiya ya siri ya watu waaminifu

Ni katika maneno hayo ndipo watu watashikwa na khofu juu ya hyo jumuiya unayotaka kuianzisha, freemason ni jumuiya ya siri na wewe unaiga style ileile ya freemason kuanzisha jumuiya ya watu waaminifu---- sasa kuna siri gani humo kama sio siri za kulinda uaminifu wa kutenda uhalifu?!
 
lutoki

Kipaumbele no. 1 ya Jumuiya hii ni kuimarisha uchumi wa wanachama wa wanachama wake.

Coverage inaanzia sehemu na kusambaa taratibu kwa kadri tutakavyoona inafaa.
TheLobbyist sasa kama ni jumuiya ya watu waaminifu mnafanyaje kiapo tena? Kwasabu natumaini vigezo moja wapo nikua mwaminifu beyond reasonable doubt, sasa mkishaaminiana kuna haja gani ya kiapo kikali?
Na kwanini kuwe na ranks? Uaminifu una viwango?
Uaminifu ndio mlango wa kuingia lakini sisi ni binadamu pakitokea 'natural life confrontations' uaminifu huweza kutetereka. Sasa ili kuikazia zaidi ni lazima kiapo kikali kiwepo, tena kikali sana sana ili kulinda uaminifu ule kwa gharama ya ustawi wa uhai wa maisha ya mwanachama.

Hakuna ranks kama ranks, ila tu ni process. Lengo la process one labda tuite Bronze process zina lengo la kujiridhisha kwamba member ni muaminifu kweli na sio mbabaishaji.
 
Ni katika maneno hayo ndipo watu watashikwa na khofu juu ya hyo jumuiya unayotaka kuianzisha, freemason ni jumuiya ya siri na wewe unaiga style ileile ya freemason kuanzisha jumuiya ya watu waaminifu---- sasa kuna siri gani humo kama sio siri za kulinda uaminifu wa kutenda uhalifu?!
Well, labda nikuulize kwa nini useme tuna siri za kufanya uhalifu? Kwa nini usiseme tuna siri ya kufanya mema? Maana yake ni kwamba tayari ww ni mhanga mkubwa wa jamii isiyoaminifu kiasi kwamba kila jambo unawaza kwa upande wa ubaya pekee na huwezi kuona kama jema. Chanzo cha kuwa hv ni kukosekana uaminifu kwa jamii inayokuzunguka
 
Hiki kikundi kinachotajwa na mleta mada hakina tofauti na GREEN GUARD
Nakuelewa, fikra kama hizi ni matokeo chanya ya maisha ya mtu aliyezungukwa na jamii isiyoaminifu, kila jambo unaona kwa mrengo wa ubaya ubaya tu. Pole sana!
 
Hizi ndio nyakati bora kabisa za kuunganisha nguvu. Hapa nalenga watu waaminifu pekee.

Dunia ya sasa inawatesa sana watu waaminifu. Kila aina ya baya ama ovu linalofanyika waathirika wakubwa ni watu waaminifu.

Kuanzia utapeli, kuumizwa moyo kimahusiano, kibiashara, kikazi, kimasomo, kiuchumi kwa ujumla wake, kidini, na kimaisha kiujumla wahanga wakubwa ni watu waaminifu.

Maisha yanazidi kuwa magumu kwa sababu watu waaminifu wamekuwa adimu sana. Wapo lakini ni waaminifu mioyoni mwao pekee. Watu wasio waaminifu wanawaumiza sana watu waaminifu kwa namna isivyoelezeka.

Watu hawasaidiani tena kwa sababu ya kukosekana uaminifu baina ya watu. Na hivi ndivyo maisha yanakuwa magumu kuliko kawaida .Kama hakuna tena kusaidiana tafsiri yake ni kwamba maisha yataendelea kuwatesa watu tofauti na kusudio la Mungu ambapo alitaka watu wafurahie maisha yao na wamtukuze Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi.

Kwa msingi huo, kuna haja kubwa sana ya kuunda Jumuiya ya siri ya watu waaminifu likiwa na lengo moja tu: 'Kushikamana pamoja kukabili changamoto za kimaisha eneo la kiuchumi, kiafya na kijamii kwa ujumla'.

Jumuiya hii itaendeshwa kwa mithili ya ki freemason (ila sio freemason). Yenyewe, ni Jumuiya ya siri inayoamini katika uaminifu, na haitasajiliwa popote duniani.

Wanajumuiya hawa wataunganishwa na falsafa moja tu ya 'Waaminifu wanapaswa kuishi maisha bora kwa sababu ya uaminifu wao'. Hivyo ni jukumu la wanajumuiya kupigania maslahi ya wanajumuiya kwa nguvu zote katika uaminifu wao.

Kutakuwa na kiapo kikali sana kwa wale watakaofuzu kuingia katika Jumuiya maana kuna hatua kuu tatu za kupitia ndipo uwe mwanajumuiya kabili.

Kuna ngazi ya Bronze, halafu inafuata ya Silver na ya mwisho ni ngazi ya Dhahabu. Ngazi ya Dhahabu ndio ya juu zaidi na ndio ya mwisho.

Kufikia ngazi ya Dhahabu kunakuwepo na kiapo kikali sana mithili ya hiki hapa:

(Na ndio maana juzi nilileta uzi nikitafuta kiapo kikali kuliko chote ili kitumike katika Jumuiya hii)

Kama kuna jamii ya watu wanaounganishwa kwa kumuamini Mtumishi fulani wa Mungu, ama kuna watu wanaounganishwa kwa mapenzi yao juu ya mpira, ama kwa imani yao juu ya mapenzi ya jinsia moja, na vyovyote vile, Je, ni kitu gani kitakachoshindikana kuwaunganisha watu kwa 'Uaminifu' wao?

Naombeni sana mni challenge katika hili.

Na zaidi nakaribisha rasmi maombi ya watu waaminifu kujiunga katika Jumuiya hii.

Idadi ya wanachama ni limited
Dunia ya Leo watu waaminifu ktk sekta zote wanachukiwa hawapendwi kabisa, MTU mwaminifu kila MTU anamwangalia vibaya, wakati mwungine anahitwa mkuda, mnonko,
 
Dunia ya Leo watu waaminifu ktk sekta zote wanachukiwa hawapendwi kabisa, MTU mwaminifu kila MTU anamwangalia vibaya, wakati mwungine anahitwa mkuda, mnonko,
Hii ni moja kabisa kati ya test za awali za kubaini mtu muaminifu. Tayari, una chembechembe nyingi za uaminifu, karibu kwenye Jumuiya
 
Well, labda nikuulize kwa nini useme tuna siri za kufanya uhalifu? Kwa nini usiseme tuna siri ya kufanya mema? Maana yake ni kwamba tayari ww ni mhanga mkubwa wa jamii isiyoaminifu kiasi kwamba kila jambo unawaza kwa upande wa ubaya pekee na huwezi kuona kama jema. Chanzo cha kuwa hv ni kukosekana uaminifu kwa jamii inayokuzunguka

Ni lazima utofautishe chama cha waaminifu na vyama vingine vya siri kama freemasons na skull and bones ambao hawapend mambo yao yawe wazi kwa public.

Sasa tunajiuliza siri ndani ya chama hicho ni ya nini??, siri katika uaminifu, huo uaminifu wenye siri ukoje??, unataka kuficha nini??.

Hata wezi au wahalifu ili shughuli zao za kihalifu zifanikiwe inahitajika sio uaminifu tu kati yao bali hata nidhamu.

Jambo jingine linaloonyesha chama hicho ni cha kigaidi ni pale unapoweka sharti kwamba nafasi za kujiunga ni "limited" wala hujataja ngapi!!-- hapo umeshindwa hata na freemasons, wao nafasi za kujiunga ni "unlimited" ilimuradi utimize masharti yao tu wewe utajiunga.
 
Labda nikuulize maswali haya:

Je, serikali ina siri ama haina? Na kama inayo Je, inaficha nini na inataka kufanya baya gani?

Je, taasisi zina siri? Kama ndio Je, kwa nini wafiche siri hizo? Ni kwa sababu wanataka kufanya ubaya gani?

Je, makampuni yana siri? Kama ndio wanaficha nini siri zao wasiweke hadharani?

Je, ndoa zina siri? Kama ndio kwa nini wasiweke hadharani, kwan kuna baya gani wanataka kufanya?

Hivi siri ya formula ya kutengeneza Coca Cola ipo hadharani kwa sababu Coca Cola ina manufaa kwa jamii?

Neno siri lisikuhangaishe sana
 
Back
Top Bottom