Jumapili tarehe 16 Desemba. Jioni.
Wazalendo kumi na moja toka Afrika Mashariki walijitolea mhanga toka vitongoji kadhaa vya London kuchangia mawazo katika kikao kilichopitisha katiba ya Jumuiya yenye lengo la kusaidia maendeleo nyumbani. Jumuiya hiyo itakayoitwa East African Community Networking Association (EACNA) inategemewa kusajiliwa karibuni. Mara ikishasajiliwa tovuti yake rasmi itatangazwa. Bado jumuiya inatafuta uanachama wa Wabongo na Wakenya ambao hawajashiriki hata kidogo. Wabongo hasa tumesemwa kuwa hatupendi kushirikiana. Kila mtu anataka kufanya yake peke yake na hatupeani moyo bali kuangushana kwa wivu usio na msingi.
Baada ya kikao yalikuwepo makulaji na vinywaji na mazungumzo zaidi. Mtindo huu wa biashara ulioenea sana nchi tajiri unaitwa networking na umewafanya majirani wenzetu hasa Waganda kuendelea sana kimaslahi Nilifurahi kuwepo kikaoni na kukuwakilisha mwanabongo.
By Fred Macha