Jumuiya Ya Afrika Mashariki London

mstahiki

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
308
5
Jumapili tarehe 16 Desemba. Jioni.

Wazalendo kumi na moja toka Afrika Mashariki walijitolea mhanga toka vitongoji kadhaa vya London kuchangia mawazo katika kikao kilichopitisha katiba ya Jumuiya yenye lengo la kusaidia maendeleo nyumbani. Jumuiya hiyo itakayoitwa East African Community Networking Association (EACNA) inategemewa kusajiliwa karibuni. Mara ikishasajiliwa tovuti yake rasmi itatangazwa. Bado jumuiya inatafuta uanachama wa Wabongo na Wakenya ambao hawajashiriki hata kidogo. Wabongo hasa tumesemwa kuwa hatupendi kushirikiana. Kila mtu anataka kufanya yake peke yake na hatupeani moyo bali kuangushana…kwa wivu usio na msingi.

Baada ya kikao yalikuwepo makulaji na vinywaji na mazungumzo zaidi. Mtindo huu wa biashara ulioenea sana nchi tajiri unaitwa “networking” na umewafanya majirani wenzetu hasa Waganda kuendelea sana kimaslahi…Nilifurahi kuwepo kikaoni na kukuwakilisha mwanabongo.

By Fred Macha
 
visit site hii---http://kitoto.wordpress.com/2007/12/21/picha-mbalimbali-toka-kikao-kilichopitisha-katiba-ya-jumuiya-ya-afrika-mashariki-london/
 
Watanzania London Vipi Mbona Mmeingia Mtini? Mbona hapa JF mnaonekana mko sana mbele? Kuna utengano London over issues za EA?
 
Watanzania London Vipi Mbona Mmeingia Mtini? Mbona hapa JF mnaonekana mko sana mbele? Kuna utengano London over issues za EA?


Ndo kwanza tunasikia, sasa bila taarifa tungeazia wapi? Lilitakiwa litoke tangazo hapa na sehemu zingine la invitation halafu tusiende ndo utulaumu. Thanks lakini kwa taarifa, nime-miss sana haya malaji!
 
Watanzania London Vipi Mbona Mmeingia Mtini? Mbona hapa JF mnaonekana mko sana mbele? Kuna utengano London over issues za EA?

Fred Macha ndio alikuwa MTZ pekee, sasa wewe jiulize kulikoni? Huenda habari hazikufika na pengine agenda haijakuwa muafaka kwa wengi n.k.

Vile vile usisahau kuna aina nyingi ya EA Community hapa UK wanafunzi, professionals na wazamiaji, kwa hiyo maswala ni mengi tu. Thanks.
 
Hao waGanda wanao'network', wanaifanya hiyo networking na nani?

Nyinyi waKenya na waTanzania ni mpaka muungane ndio mnetwork?

Hayo ni mambo ya waKenya siku zote kutafuta watu wa kuwatumia kwa faida zao. Wao kila siku wanajifahamu ni Superior, superpower; mpaka wanapotaka mtu wa kumnyonya ndio wanapoanza kuwa East African.
 
Back
Top Bottom