Jumuia ya wakristo watoa tamko kuhusu mchakato wa katiba

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,436
4,429
JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA-TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA KUTOKA CCTJumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) inachukua fursa hii kuvishukuru vyombo mbalimbali vya habari kwa jinsi ambavyo vimekuwa vikitoa taarifa mbalimbali kuhusu kazi na matamko ya CCT.

Kuhusiana na mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya, CCT inaamini kuwa suala hili ni la MARIDHIANO na sio la ubabe wa kikundi au chama fulani cha siasa.-Kama ambavyo ilitangazwa na Mhe. Rais Januari 2014 kuwa Taasisi mbalimbali zipeleke mapendekezo ya wajumbe wanaoweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, CCT ilipeleka mapendekezo ya wajumbe tisa na kati ya hao Mhe. Rais alimteua mjumbe mmoja tu ambaye ni Bibi Esther Msambazi.

Mjumbe huyu aliyeteuliwa ni Mkristo wa kawaida (lay Christian) na wala si Kiongozi wa Dhehebu lolote la Wanachama wa CCT na pia hata sio Mzee wa Kanisa analotoka bali Mkristo mwaminifu wa kawaida. Huyu ndiye mwakilishi wa CCT kwenye Bunge Maalum la Katiba. Viongozi wengine wa Dini ya Kikristo (Maaskofu na Wachungaji) waliopo katika Bunge hilo HAWAKUTUMWA NA CCT na wala CCT haina taarifa ni vipi walichaguliwa kuwa wajumbe wa Bunge hilo Maalum.

Aidha, pia Jukwaa la Wakristo Tanzania haliwatambui Viongozi hao kwani Jukwaa hilo linaundwa na Taasisi za TEC, CCT, PCT na SDA. Kutokana na misingi ya imani ya taasisi hizi kwa umoja wake, Viongozi wakishakubaliana jambo fulani kwa pamoja na kwa umoja wao wanalisimamia na kulitekeleza. NDIYO YAO NI NDIYO NA HAPANA NI HAPANA kwa kuwa hawana ndimi mbili na wala hawatumikii Mabwana wawili.

Kwa mantiki hiyo, CCT ikiwa mmoja wa taasisi zinazounda Jukwaa la Kikristo Tanzania inaendelea kusisitiza kuwa msimamo wa viongozi wa dini kama ulivyotolewa na Jukwaa la Kikristo Tanzania kuhusiana na Maoni waliyopeleka kwa Tume ya Kukusanya Maoni ya Wananchi chini ya Uenyekiti wa Mhe. Jaji Mstaafu Warioba na Matamko waliyotoa ni sahihi na itaendelea kuyasimamia na kuyasambaza hadi yamfikie kila Mkristo ili wananchi wa Tanzania wapate Katiba wanayoitaka.

Aidha, Viongozi hao wa Jukwaa la Wakristo Tanzania haliwezi kutafuta maoni ya Viongozi wa Dini walioko katika Bunge Maalum la Katiba kwa sababu hawawatambui kama wawakilishi wa taasisi zao na hivyo kukataa kwa nguvu zote yale ambayo viongozi hao waliopo Bungeni watakuwa wakiyasema. Mwisho kabisa tunawaomba viongozi hao wajiulize, "hivi sisi tumetumwa na tunamwakilisha nani humu Bungeni?"-Imetolewa leo-September 05, 2014Na: JUMUIYA YA KIKRISTO
 
Kwa hiyo chokochoko n kwa sababu hawakuchaguliwa viongoz wa hyo CCT duuhh mbona hatarii hawa viongoz wa dini, kwani aliechaguliwa si n muumni tatizo liko wap? Waachee uchonganishi
 
Nawashauri waende mbele zaidi ya tamko ilo la sivyo wamepigwa changa la macho. Magamba kupitia tamko la hao 'wawakirishi wa dini' wanajua wanachokifanya.
 
Magamba jifanye wagumu kuelewa ili 2015 iwe rahisi maana HAMSIKII wa la HAMUONI kama FARAO vile.
 
mtukufu rais wetu okoa fedha za walipakodi zinazotafunwa bure mle ndani twakuomba mungu ibariki tanzania
 
Kumbe wapinzani walikuwa sahihi kusisitiza taasii zenyewe ndo zichague hao watu ni si Rais, na poa wako sahihi wanaposema kuwa kati ya wajumbe 201 kati yao wajumbe 166 ni makada wa CCM. Loh ..ama kweli hakuna siri chini ya jua !!!
 
JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA-TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA KUTOKA CCT

Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) inachukua fursa hii kuvishukuru vyombo mbalimbali vya habari kwa jinsi ambavyo vimekuwa vikitoa taarifa mbalimbali kuhusu kazi na matamko ya CCT.

Kuhusiana na mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya, CCT inaamini kuwa suala hili ni la MARIDHIANO na sio la ubabe wa kikundi au chama fulani cha siasa.-

Kama ambavyo ilitangazwa na Mhe. Rais Januari 2014 kuwa Taasisi mbalimbali zipeleke mapendekezo ya wajumbe wanaoweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, CCT ilipeleka mapendekezo ya wajumbe tisa na kati ya hao Mhe. Rais alimteua mjumbe mmoja tu ambaye ni Bibi Esther Msambazi.

Mjumbe huyu aliyeteuliwa ni Mkristo wa kawaida (lay Christian) na wala si Kiongozi wa Dhehebu lolote la Wanachama wa CCT na pia hata sio Mzee wa Kanisa analotoka bali Mkristo mwaminifu wa kawaida. Huyu ndiye mwakilishi wa CCT kwenye Bunge Maalum la Katiba.

Viongozi wengine wa Dini ya Kikristo (Maaskofu na Wachungaji) waliopo katika Bunge hilo HAWAKUTUMWA NA CCT na wala CCT haina taarifa ni vipi walichaguliwa kuwa wajumbe wa Bunge hilo Maalum.-

Aidha, pia Jukwaa la Wakristo Tanzania haliwatambui Viongozi hao kwani Jukwaa hilo linaundwa na Taasisi za TEC, CCT, PCT na SDA. Kutokana na misingi ya imani ya taasisi hizi kwa umoja wake, Viongozi wakishakubaliana jambo fulani kwa pamoja na kwa umoja wao wanalisimamia na kulitekeleza. NDIYO YAO NI NDIYO NA HAPANA NI HAPANA kwa kuwa hawana ndimi mbili na wala hawatumikii Mabwana wawili.

Kwa mantiki hiyo, CCT ikiwa mmoja wa taasisi zinazounda Jukwaa la Kikristo Tanzania inaendelea kusisitiza kuwa msimamo wa viongozi wa dini kama ulivyotolewa na Jukwaa la Kikristo Tanzania kuhusiana na Maoni waliyopeleka kwa Tume ya Kukusanya Maoni ya Wananchi chini ya Uenyekiti wa Mhe. Jaji Mstaafu Warioba na Matamko waliyotoa ni sahihi na itaendelea kuyasimamia na kuyasambaza hadi yamfikie kila Mkristo ili wananchi wa Tanzania wapate Katiba wanayoitaka.

Aidha, Viongozi hao wa Jukwaa la Wakristo Tanzania haliwezi kutafuta maoni ya Viongozi wa Dini walioko katika Bunge Maalum la Katiba kwa sababu hawawatambui kama wawakilishi wa taasisi zao na hivyo kukataa kwa nguvu zote yale ambayo viongozi hao waliopo Bungeni watakuwa wakiyasema.

Mwisho kabisa tunawaomba viongozi hao wajiulize, "hivi sisi tumetumwa na tunamwakilisha nani humu Bungeni?"-

Imetolewa leo-September 05, 2014Na: JUMUIYA YA KIKRISTO
 
Kwa hiyo chokochoko n kwa sababu hawakuchaguliwa viongoz wa hyo CCT duuhh mbona hatarii hawa viongoz wa dini, kwani aliechaguliwa si n muumni tatizo liko wap? Waachee uchonganishi
Kikwete ni muumini wa dhehebu gani la kikristu mkuu.
 
Kumbe wapinzani walikuwa sahihi kusisitiza taasii zenyewe ndo zichague hao watu ni si Rais, na poa wako sahihi wanaposema kuwa kati ya wajumbe 201 kati yao wajumbe 166 ni makada wa CCM. Loh ..ama kweli hakuna siri chini ya jua !!!

kuna wawakilish wa wagabga wa kienyeji
 
Hongera Lisu kwa kuwafumbua watanzania sasa nadhani ccm wanaanza kukuelewa
 
Hii nchi ni ngumu na kila mtu ni mnafiki. Inashangaza hao viongozi wa dini kuibuka leo na kusema hawakuwakilishwa. Huu ni unafiki wa hali ya juu. Sitetei CCM lakini naomba kuuliza tu Prof. Mahalu anawakilisha kundi gani? Na si yeye mhadhiri mwandamizi wa sheria pale SAUT? Na Askofu Muhagachi sio mwakilishi Wa Wakristo au kuna MTU ni Mkristo kuliko wenzake?
 
Back
Top Bottom