Jumamosi hii: Dawati la jinsia

Jumamosi hii: Dawati la jinsia

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,505
Reaction score
860,526
Kutokana na vitendo vya kikatili vinavyomea kwenye jamii yetu serikali imeamua kuanzisha madawati ya jinsia karibu kwenye kila kituo cha polisi !ni jambo zuri
Shida iliyopo ni kwamba madawati yale yanachukuliwa kuwa ni kwa ajili ya wanawakr na watoto tu ,,hii sisawa kuna wanaume wengi tu nao wanapaswa kwenda kushtaki kwenye haya madawati
Wananyanyaswa na kuteswa mno na wake zao
Hawapewi haki yao ya ndoa
wanachapiwa live
Wanapangiwa matumizi kwa mishahara yao wenyewe
Wanapigwa
Wananyimwa chakula
Wanabakwa
Wanapangiwa majukumu wasiyoyaweza na wake zap wababe
Jamani kina baba msife na kihoro moyoni nendeni mkapate msaada. Madawati ya jinsia ni kwa ajili ya wote
 
Binafsi, Nimeshajaribu sana kufanya kazi na dawati la jinsia. Nimeshapeleka kesi 4 na sikuwahi kupata msaada hata kidogo... Namaanisha 0% cooperation. Kwa uzoefu wangu naamini hawa nao ni polisi tu kama polisi wengine ambapo weledi bado ni tatizo sana na pili hawa nao ni sehemu ya jamii ambapo ukatili wa kijinsia ni sehemu ya kawaida ya utamaduni....... Nakumbuka hili dawati linaitwa dawati la wanawake na watoto.

Lakini pia hata miongozo ya uanzishaji na uendeshaji wa dawati inaonesha kuwa dawati hili limetengenezwa kuhudumia akina mama na watoto...
 
Ukienda kushtaki ujue wewe ni bushoke na huna maamuzi,tena upigwe tu.
 
Binafs Nikinyanyaswa Na Mwanamke Naondoka Na Sanduku La Nguo Zangu Nasepa Mbali, Wala Cmwambii M2 Hata Hilo Dawat Sitopenda Lipate Taarifa,
 
Kwenye kubakwaa siaminii hapo hua mnapenda tu,toka lini mwanaume abakwee na mwanamke khaa!!
 
Hee mwanaume ukashtaki polisi umebakwa na mkeo inahuu!!
 
Mimi kwakweli siwezi hata kuthubutu kwenda huko hata mwanamke aninyanyase vp siendi. Ng'o yakizidi na mwachia nyumba watoto nasepa kuwanza maisha kwenye geto la kupanga
 
hata TARIME wanaume wananyanyaswa???
 
..tumszoea kusikia cases za wanawake kubakwa, je mwanamme aweza kubakwa???

Ndio kwakuwa kubaka ni kitendo na hakihusiani na jinsia ila kuna kubaka kubakwa na kubakana
 
Back
Top Bottom