Juma Duni - London 13 Jan 2009 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Juma Duni - London 13 Jan 2009

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Feb 4, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Makala yake imekuwa attached hapo Chini jisomee kwauangalifu.

  0.1 Katika gazeti la Rai (Toleo Na.667 (ISSN 0856-4973) la 11/5/ 2006 ) muliandikwa makala ndefu sana ya Mhe. Hussein Siyovelwa yenye kichwa cha maneno yasemayo "Muungano wetu hauna mwisho mwema ".

  0.16 Hivi karibuni imetangazwa kwamba aliyemtesa Mbwa wa mzungu kule Mererani amefungwa muda usiopungua mwaka mmoja.....Habari zinaendelea kwenye attachment.

  1.19 Mwaka 1993 kundi lilojiita G55 walijaribu kurejesha Serikali ya Tanganyika kwa Azimio la Bunge. Mhe. Njelu Kasaka alieleza kwa ufasaha kabisa hoja hii. Amri ya Mwalimu Nyerere ambae wakati ule hakua Mbunge wala Rais akazuia Azimio la Bunge kutekelezwa badala yake Bunge likaazimia kukitaka chama na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kutayarisha mazingira ya kuifanya Tanzania kua na Serikali moja.Yaani badala ya kusahihisha makosa ya miaka yote ya uhai wa Muungano wakubwa hao wakalenga kumaliza pale palipo baki pa kuuwa taifa la Zanzibar ambalo 1964 waliungana nalo kwa hiari.
   
  Last edited: Feb 4, 2009
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Feb 4, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mbona imechukuwa kitambo hivyo au mpaka kufanye edit
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kikao kilikuwa cha Kimataifa kwa kiasi chake,hivyo makala zote zilibidi zipitiwe na kuhakikiwa na kupatiwa ruhusa yakuenezwa au kuchapishwa,na ni watu wengi kila mmoja ametayarisha yake ,na hata waandishi na watu mashuhuri hapa Tz walialikwa ,hivyo hakuna editing yeyote ,ila zilikuwa copy right kwa muda fulani.
   
 4. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Asante bwana.
  Mie bahati mbaya kama walivyo waZanzibar na Watanganyika wengi, sijui kilichomo ndani ya muungano, hata kuwafanya watawala wawakatalie wananchi kuamua juu ya hatma ya muungano wao.

  Mimi naona tuanze na kura ya maoni kuhusu muungano halafu ndio tumalizie na kura ya serikali ya mseto!

  Safari rahisi ni "kuruka (kudondoka) kutoka juu na sio kuruka kutokea chini kwenda juu"
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli nilikuwa nimetulia na kuusoma waraka mzima uliowasilishwa na Juma Duni au aliousoma huko London ,aliyoyazungumza kwa upande wangu (Simlazimishi mtu kuukubali) naona ni mambo mazit0 sana na kwa yeyote ambae atakuwa na akili timamu ataweza kuyaona na kwa ufupi kufahamu haya matatizo yapo wapi na amani ipo wapi ,na hata kuona kuwa hawa mafisadi wa leo kiasi nao wachote humohumo maana BOT yenyewe kumbe ni fisadi.
   
 6. K

  Koba JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...ni wazi Wazanzibar hawataki huu muungano,na wengi bara we just dont care na wala hatuoni faida wala hasara za huu nuungano labda mafisadi wa CCM peke yao,naona tuwape nafasi hawa jamaa wa visiwani wapige kura kama wanataka huu muungano au laa,na uamuzi wa majority ndio utakaoamua!
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Feb 5, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  ..Wazanzibari hao kila siku wana madai mapya. ukitatua hili wanakuja na lingine, ilimradi vurugu tu.

  ..halafu Juma Duni analalamika kwamba Mkapa hakurithiwa na Mzanzibari!! mbona chama chake CUF hakijawahi kusimamisha Mzanzibari kugombea Uraisi wa Muungano??

  ..kwa maoni yangu nadhani Muungano uvunjwe. Watanganyika hatuna habari nao, na maana yake ni kwamba hatuuhitaji.
   
 8. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sio kweli kama kila siku wana madai mapya. Ukweli ni kuwa katika madai yetu yale ya msingi hayatatuliwi bali yanafanyiwa njama za kukwepwa.

  Nakupongeza Ndugu yetu -Mshirazi wa Kitumbatu (J. Duni) -kwa kuthubutu kueleza yale ya msingi ambayo hayatekelezwi. Hayo tutaendelea kuyaeleza kila siku hadi pale Wa-Tanganyika mtakapokubali yarekebishwe. Wazanzibari tumeingia katika Muungano kwa nia njema. Inasikitisaha kuona wenzetu wanavyotutaka (kutulazimisha kwa ujanja wao) tuipindishe nia hiyo njema na kutamka kuwa hatuutaki.
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Suala hapa sio WaZanzibari hawataki Muungano ,bali ni kuonekana maslaha mengi au yote yanavutiwa upande wa Tanganyika na Juma Duni ameelezea kwa ufasaha zaidi ili hata nyie mnaokaa na kurapu muelewe tatizo lipo wapi. Ametoa mfano kuwa hizi ni nchi mbili,Zilizoungana kama Nchi na hakuna uhusiano kati ya ukubwa na udogo huku kuna watu kama upupu na kwengine kuna watu kama uyoga.

  Sasa majumuisho ya taabu na raha yakijumlishwa na kulinganishwa inaonekana kuwa upande mmoja unateka sehemu za mwingine na kuhatarisha maendelea na hivyo kila hatua inaonyesha uchumi wa Zanzibar unabanwa kila pembe ,sasa mambo haya vipi ? Hivi hapa kutakuwa na udugu kwa kumkamua mwenzio na sio kumkamua bali kumziba punzi au pumzi ,huu ni ufisadi wa nchi moja kuifanyia nyengine.
   
 10. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mheshimiwa Joka Kuu. Ningekuomba ufanye home work kidogo-yaangalie madai yote hayo ya Wazanzibari (kuanzia wanasiasa hadi wanamichezo). Si mapya hayo. Bali yote yanalenga katika dai moja la msingi nalo ni "Sovereignity" (samahani sijui tafsiri yake sahihi kwa kiswahili). Wazanzibari hawajauza sovereigninty yao. Wanayo (popote pale walipoiweka kama amana na iwe hapo) Sasa tatizo ni kuktaa hao watu watumie sovereignity hiyo.
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Yaani unahubiri kama vile CUF iliwahi kushika madaraka ya nchi na hapa ndipo wengi wenu mnapokwenda mchomo ,halafu isimamishe wakati inafahamu kuwa Tanzania haipo ila iliopo ni Tanganyika iliyobatizwa ,huu muungano umetoka nje ya system hivyo yote hayo yanawezekana ikiwa utakuwepo kwenye system na uptodate ,hii nchi imeshapotea na imeshatoka katika dira inaendeshwa kivyakevyake tu ,mwenye nguvu mpishe mwenye feza si mwenzako ,polisi anaweza akakubambikia kesi na fisadi akakufilisi.
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Feb 6, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  mwiba,

  ..soma vizuri manunguniko/malalamiko/masimango aliyoyatoa Juma Duni.

  ..kama CUF ilikuwa inaamini kwamba baada ya Mkapa ni zamu ya Wazanzibari kuwa Raisi wa Muungano, kwanini hawakusimamisha mgombea toka Zanzibar?

  ..masuala ya CCM waachieni wenyewe. inaelekea mnalalamika tu lakini nyinyi wenyewe CUF hamyafanyii kazi malalamiko yenu.

  ..Watanganyika tumechoka na malalamiko yenu. Ondokeni, kama ni 'talaka' itawafuata mkiwa kwenu.
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Feb 6, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  Pakacha,

  ..sovereignity haidaiwi hotelini London.

  ..kama Zanzibar wanataka kujitenga basi wapeleke madai yao kwenye Bunge la Tanganyika na Baraza la Wawakilishi.

  ..kama mnataka kujiunga na OIC fanyeni hivyo, na serikali ya Muungano ikiwahoji kataeni kujitoa.

  ..na kama mko makini kweli na kujitawala basi ondokeni ktk ardhi ya Tanganyika mkaijenge Pemba yenu.
   
 14. K

  Kwaminchi Senior Member

  #14
  Feb 7, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wanasema, ukitaka kujua ulipo, hunabudi ujue utokako na kabla hujajua uendako ni muhimu kwanza upatazame vizuri ulipo. Tumetoka wapi, tupo wapi na tunakwenda wapi?

  Kabla ya muungano, yalikuwapo mataifa mawili yenye hadhi sawa. Mataifa haya mawili yalikuwa na dola kamili na serikali zake mbili, kila mmoja na yake.

  Nini ilikuwa dhamiri ya Muungano huu? Kwa nini waasisi wa muungano huu walikuwa wasiri na wenye haraka, kiasi ya kufikia kukubaliana na kuutangaza kabla ya wananchi na serikali zao kushauriwa au/na kuulizwa?

  Hata pale serikali hizi mbili zilipoidhinisha muungano huu, mambo yalikwenda kimkanda mkanda tu bila ya maoni ya wananchi wake kupatikana.

  Kwa nini muungano huu ulikubaliwa uwe wa mambo machache tu ya muungano na mengine kubaki kwa serikali zake za awali? Na swali kubwa sana kwangu ni kwa nini Tanganyika ilitaka mambo yake yote yaendeshwe na serikali ya muungano na Zanzibar kutaka ijiendeshee yenyewe mambo yake yote yasiyokuwa ya muungano?

  Sababu ya gharama ya kuendesha serikali tatu, kwangu mimi, haizuii maji. Huwezi kutaka mtoto, kisha useme hutaki gharama za malezi.

  Kila nikitafuta majibu ya maswali haya yote, naona kuwa maswali zaidi yanapatikana kuliko majibu. Hali hii inanifanya nione kuwa muungano wetu huu ulikuwa muungano wa mashaka "from the word go."

  Hali hii ya mashaka ndiyo iliyotuleta hapa tulipo, njia ya panda. Tunakwenda wapi katika hali hii?

  Wanasema, huwezi kumsaidia mgonjwa, sharti mgonjwa mwenyewe atambue kuwa ni mgonjwa na kisha akubali kuwa anahitaji msaada.

  Je, tunakubali kuwa tuna muungano wa mashaka? Inavyoonekana Zanzibar wengi ndio wanaokubali kuwa muungano huu kama ulivyo hauwaridhishi. Kwa upande wetu sisi Watanganyika ndio tunaotaka zaidi muungano huu kama ulivyo hivi sasa kuliko wenzetu.

  Sisi Watanganyika ndio tuliokubali kuzamisha mambo yetu yote ndani ya serikali ya muungano. Tumelizamisha Taifa letu la Utanganyika ndani ya Utanzania na Tumelizamisha jina la nchi yetu ya Tanganyika na kukubali kuwa Tanzania au Tanzania Bara au "just plain" Bara. Kwa faida gani au ya nani?

  Kama ni kwa nia ya kufikia lengo la awali la Kwame Nkrumah la kuipata serikali moja au nchi moja ya muungano wa Afrika, mbona sioni kipengele hata kimoja katika katiba yetu ya muungano kinachokaribisha au kinachotoa mwanya kwa nchi nyingine kujiunga nasi katika muungano wetu huu?

  Kama tunashindwa kupata muungano wenye nchi moja, serikali moja na Taifa moja na/au tunashindwa kuunda shirikisho lenye serikali tatu na nchi mbili lenye Taifa moja, mimi naona huu muungano wa nchi mbili lenye Taifa moja la Watanzania na sub-taifa la Wazanzibari halina manufaa kwa Mtanganyika wala kwa Mzanzibari. Muungano huu utatukuzia chuki na uhasama, ili hali sisi ni majirani wazuri tangu siku za dahali.
   
 15. F

  Fataki Senior Member

  #15
  Feb 7, 2009
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mwiba, shida hapa ni umdebwedo wa Wazanzibari, wote wanataka kuwa viongozi na wale biriani ya kuku kila siku bila kufanyakazi! Unajua mtumwa wa jana akipata, ni kufuru tupu!

  Huu ni ushirikiano wa ndovu (tembo) na panya! Sasa panya anadai mlo sawa na ndovu pamoja na kwamba mchango wake ni insignificant kwa maslahi ya ndovu! Akina Mwiba, mtapasuka msamba!
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ukweli ndio huo umishaelezwa ,sasa nyinyi endeleeni kuweka pamba masikioni mkiendela kubeza,kikao cha London ndio hicho kimeshapita,halafu wewe unaebeza mambo kufanyika London hivi umesahau hata yule mjanja mmoja alichukua chake mapema kule London ,yaani mna sahau za halaka sana ,siwashangai ,na hii kupasuka msamba sio WaZanzibar watakao pasuka bali hawa wanaowapigia kelele mafisadi maana hakuna la maana hata moja lililofanywa kama ni kina Lowasa ,jamani wao ndio wa mwanzo mbona hata hawana habari na hawa wengine si tumeshaona wapo uraiani kesho na kesho kutwa wanakuwa huru na fedha waliyokwiba ndio wataila bila kificho.

  Kwani mnafikiri Zanzibar hakuna mafisadi ? Wapo wengi tu na fedha inaliwa ,kwani wakubwa wengi wamefungua mahoteli ya kitalii ya kisasa ,fedha wamepata wapi ?Lakini huu sio wakati wa kuwakurupusha ,wakati ukifika wataitwa kwa upole kabisa wajieleze na si kwa mahoteli yao bali kwa mahesabu yaserikali ambayo yatafanyiwa utafiti wa kina kabisa.

  Tatizo ambalo WaTanganyika mnakumbana nalo ni kuwakurupusha hawa mafisadi wakati upinzani wenyewe haupo katika msimamo uliojengeka,yaani bado upinzani kwa Bara haujawateka wananchi wa kuaminika ambao wameshabwaga manyanga ya kuwa na CCM tofauti na Zanzibar ambako ukiwaamsha watu usiku kwenda kupiga kura basi CCM haishindi hata kwa robo ya kura na huo ndio ukweli ambao naamini kabisa kila mmoja wetu analijua hilo.

  Uwajengee utakachowajengea Zanzibar hawaipigii kura CCM kwani wananchi wake walio wengi sana wameshachoka na utawala wa CCM,hilo lipo wazi na mtu anaeweza kufanya utafiti wa kweli na aende sio utafiti huu wa akina Nipashe,wengi wa hao CCM mnaowaona ni wabeba kadi tu kwa maslahi yao binafsi lakini ukienda kwenye kura anajua wapi pa kuipeleka kura yake japo ana uhakika kuwa majeshi na polisi wakisaidiwa na vyombo vya usalama vitabadilisha matorokeo lakini haipi kura CCM hata siku moja.

  Kikwete ,Karume ,Pinda,Shein na wengineo wanalijua hilo kuwa CCM Zanzibar hawana ushindi ndio hapo alipowambia wananchi na wabunge wapinzani wachague watakapo lakini upinzani hautashika madaraka kwa karibu au hawatopata kuongoza kabisa.

  Na wao wanaambiwa wajenge maendeleo,wapeleke umeme wafanye kila wanaloliona jema lakini CCM haitoshinda kwenye uchaguzi wowote,sasa hao ni wananchi ambao wanasema kwa uwazi kabisa,utawala wa CCM basi,miaka walioka madarakani imetosha waondoke.

  Na wewe KWAMINCHI unajua unachokisema au unarapu tu na kungoja kutiliwa mziki ? Katika hati ya Muungano hakuna TANZANIA ipo Tanganyika na Zanzibar tu,sasa kujidai kuwa mumeitumbukiza Tanganyika ndani ya Tanzania huo ni wizi ,tena wizi wa kiini macho,ndipo pale mnapoambiwa kuwa kinachopewa serikali ya Muungano kigaiwe nusu kwa nusu hakuna huyu mdogo au huyu mkubwa,najua mtasema kuna mambo ya Muungano na yasio ya Muungano,na haya yasio ya Muungano hayamo katika Muungano haya ni ya Zanzibar tu, yaliomo kwenye Muungano hayo ni ya Zanzibar na Tanganyika,lakini ninyi mmeyaondoa yale ya Muungano na kuyafanya hayawahusu WaZanzibari hilo ni kosa !!! Maana kama hayawahusu WaZanzibari yatamuhusu nani ? Waziri wa Kilimo wa Tanzania au sio huyu anatakiwa awe na data za Zanzibar pia na akipewa matrector 50 ajue 25 yanakwenda Zanzibar lakini sivyo anasema Zanzibar wana wizara yao ya kilimo sasa hiyo ya Muungano ilikuwaje ikaitwa ya Muungano ,Muungano gani huo,au utanipeleka kwenye hati ya Muungano ?

  Ndipo mkaambiwa kuwa Tanganyika mumejiingiza kwenye serikali ya Muungano na kujiita Tanzania ili kuiba ni wezi,na mnaendelea kuiba mpaka pale Tanganyika itakapopatikana hivyo fedha mnayopata na kupokea mishahara na kugawana mitambo na fedha za misaada zinazopata wizara za serikali mnakula na kulisha watoto wenu fedha ya haramu kwani kiasi cha fedha hizo ni za Zanzibar na Tanganyika ,kama umesoma hiyo attachment uneweza kuona namna wizi ulivyofanyika,ulaghai ulivyofanyika na barua za kutekeleza ili kuwepo na dhulma na fedha iliyoibiwa na BOT ni wizi tu hakuna jingine Serikali ya Tanganyika imejivalisha koti la Muungano na kuiba mapato ya Muungano kwa njia za hadaa na maneno mengi kama si wizi ni kitu gani,Muungano huu ni wa nchi mbili Nchi moja imejichomeka wapi ?Nani aliwapa ruhusa ya kujichomeka huko kama si kutaka kuiba ni kitu gani , ,wizmtwup !! Ni lazima iwepo Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanibar ya Zanzibar ipo ya Tanganyika iko wapi,tuamini kwamba haipo kwa misingi gani ? Mabadiliko gani yalioifuta Tanganyika ? Kama huku kujichomeka si kwa hila za kuiba kinachoingia kwenye Muungano ni nini ? Ni wizi tu hakuna jingine sasa wizi unafanyika kwenye Serikali ya Muungano hivi unafikiri Zanzibar haiathiriki na wizi huu ?

  Muungano umechezewa na umevurugwa lakini hatukumsikia Kikwete akiwatisha wanaovuruga Muungano na badala yake amewatisha wanaotishia kuvuruga Mapinduzi ,hivyo huu Muungano kwa hapa ulipofikia si Muungano bali ni wizi ,wizi tu hakuna jingine ,kwani Zanzibar wakipiga mahesabu kama mnavyopiga nyie kuhusia na EPA na menginetele kinachopatikana ni wizi ,Serikali ya Zanzibar inaibiwa katika Muungano uliokuwepo ,fedha za Zanzibar zinazopotea zingeweza kuikwamua Zanzibar katika matatizo inayoyakabili, lakini serikali ya Tanganyika iliyojikita ndani ya Muungano inaiba fedha hiyo kwa maendeleo ya upande mmoja. Badala ya Zanzibar kuwa na Muungano na Tanganyika sasa imekuwa na Muungano na wezi unafikiri nani atakubali ,kila kitu kina mwisho kama mlivyodhamiria kuwafikisha mafisadi katika ulingo na kuwaweka kona ndivyo hivyohivyo Serikali fisadi ya Tanganyika ndani ya Tanzania itakavyofikishwa kwenye mahakama za kimataifa ,kesi ipo mbioni kufikishwa kunako husika.

  Na na shangaa wale walioidai Tanganyika wakati ule wapo wapi au ndio tuamini kuwa wamekatiwa chao na kuonjeshwa fedhas za wizi zinazopatikana kwa kuibia Zanzibar ? Wapo wapi kama nawao walikuwa sio wezi waliokuwa hawapati mgawo ?
   
  Last edited: Feb 7, 2009
Loading...