Juma Duni kubaki CHADEMA?

Jiulize kwanza wewe mleta mada nini hatima yako ndani ya nchi hii kutokana na haya tuyaonayo sasa likiwemo na tatizo la umeme? kwani kwa kufanya hivyo utakuwa angalau utaonyesha umejijali kuliko kuwajadili watu ambao maisha yao ni mazuri kuliko wewe unayehangaika.
 
juma duni haji ndio nan? ahahahaha OK kumbe ni yule mchezaji wa chadema walomchukua kwa mkopo kutoka cuf
je utanipendagaaaaa
 

Siku zote kaa ukijua Haki na Batili haviwezi kaa pamoja. Cuf ni Haki na cdm ni Batili.

Sasa ona walivyobusy kumtoa mnyika ofisini
 
Vijana inabidi muielewe siasa mtoa mada inaonekana siasa huijui, ukawa ni muuondo wa vyama vinne kwa hyo walipoamua kuingia kwenye uchaguzi na kugombania urais inabidi kila chama kitoe mgombea wake lakin kwa vile wameungana haiwezekani kuweka wagombea wote 4 sasa wakaamua ww chadema una wafuasi wengi na una nguvu huku bara toa mgombea wa urais na wakaona wa pili kwa wafuasi wengi ni cuf ss wewe weka mgombea mwenza haina maana juma duni alihama chama chake,bado yuko cuf na anafanya shughuli katika chama chake cha cuf bda uchaguzi kuisha
 
Hatma yangu ni kwa kujiamini na kufanya kazi kwa bidii ( HAPA KAZI TU ) na siyo kuhamahama itikadi kwa sababu ya kuendekeza njaa!. Huyo Babu kiitikadi siyo Chadema, na sababu ya kuhamia Chadema ilikuwa ni kusaka madaraka. "A liberal is a conservative who has been arrested." Tom Wolfe
 
 
Ndugu unapotosha sana. sheria ya uchaguzi inatamka wazi, Chama kitasimamisha mgombea urais na mgombea mwenza. Ndiyo maana Babu duni ililazimu ahame CUF na achukuwe uanachama wa Chadema kwa kibali cha Maalim Seif. Tume ilishatoa onyo hakuna chama kinaitwa UKAWA na hakitambui uwepo wake na ndiyo sababu ya mgogoro wa jimbo la Segerea tume ilipoamua kurejesha majina mawili yote ya Ukawa.

Duni alichukua kadi ya Chadema tume ikaridhika na kumpitisha kuwa mgombea mwenza wa Lowassa
 
Tumeona babu Duni akirudi CUF na kuiponda chadema. Kulikoni?

Tumeona Mwapachu akirudi CCM na kujilaumu kuwa alifanya makosa na ametubu. Kulikoni?

Kingunge kimya, NPS mashakani. Kulikoni?

Lowassa kimya, Meneja wake wa kampeni katoroka nchini, mkwe wake "ananyea debe" keko. Kulikoni?

Jee, kutolewa Rished Bade TRA kuna uhusiano wowote wa umasai wake na Lowassa? Cha kushangaza kwa Bade ni kuwa mpaka sasa hajapatikana na kosa lolote la kumpeleka mahakamani kama ilivyo kwa wasaidizi wake akina Masamaki. Kulikoni?

Siasa za Tanzania ni kizungumkuti.
 
Endelea....
 

Nakuonaga makini pamoja na udini wako lakini huna lolote
Rished Bade ni mtanzania mwenye asili ya kisomali kama walivyo kina Kinana,Bashe,Rage na wengineo wengi ndani ya CCM na wala sio mmasai.
Lowassa Edward naye ni Mmeru kwa kabila aliyekulia umasaini.
 
Huna haya? Wala hujui vibaya?

CCM mbele kwa mbele.

Jibu maswali, au mtawapa ubunge wa viti maalum?

Kwi kwi kwi teh teh teh!


sasa si ukamuulize juma duni sisi tunajuaje anawaza nini au imemuathiri vipi? by the way kabla ya kuja chadema sikuwahi kumsikia alikuwa ana cheo gani au kazi gani?
 

Rished Bade hana asili ya kisomali, Rished Bade ni mmasai wa ukoo wa Laseko, mbona hao ni maarufu sana Arusha. Uliza watu wa Arusha wakujuze.

Huwa sikisii.
 
Rished Bade hana asili ya kisomali, Rished Bade ni mmasai wa ukoo wa Laseko, mbona hao ni maarufu sana Arusha. Uliza watu wa Arusha wakujuze.

Huwa sikisii.
Unamjua vizuri bade au unamuona kwenye picha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…