Julius Mtatiro naye anasubiri siku tu

Julius Mtatiro naye anasubiri siku tu

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,392
Kila kitu kiko tayari punde tu naye ataungana na wenzake kusaidia taifa kupitia CCM.Alipokutana na Mh Makonda kila kitu kiiwekwa sawa.

Hata ukiingia sasa katika page zake yuko anatukanana na fans wake baada ya kuwaunga mkono waliohama.

Kila la kheri Mtatiro
a95d1d4a4418b2ce0c7da7c6a00a2ebb.jpg
mm
Mwenyekiti wa CUF Julius Mtatiro, akutana uso kwa uso na Paul Makonda
 
Acheni kuzusha zusha
Julius S. Mtatiro
11 hrs ·
USHAURI WA BURE.

Msiwatukane wanaohama kwenye chama chenu ili siku wakirudi msianze kazi ya kusameheana matusi yenu na ama kununiana.

Kafulila alikulia ndani ya CHADEMA, baadaye akahamia NCCR MAGEUZI, kisha akarejea tena CHADEMA na hivi sasa amehamia CCM (amehama vyama mara 4).

Na mfano mwingine ni mwalimu wangu Prof. Kitila, amekulia ndani ya CCM (sina hakika kama aliwahi kuwa NCCR) lakini tunajua alihamia CHADEMA, akatoka CHADEMA akaanzisha ACT, na sasa ameiacha ACT amekwenda CCM.

Huo ni ushahidi thabiti kuwa wapo wanasiasa safari zao kisiasa huwa ziko namna hiyo, huhangaika sana lakini kibinadamu lazima tuwaheshimu kwa dhati. Hata binadamu anapokuwa anafariki yupo ambaye hufa kwa utulivu na yupo ambaye hufa kwa kuhangaika sana.

Msishangae kuwa baada ya mwaka mmoja au miwili Kafulila akarudi CHADEMA, Masha akaenda ACT, Patrobas akaenda CUF na Kitila akaanzisha chama kipya.

Kama mnachanganywa na hali hii ya sasa inaonekana mtakuwa wendawazimu kabisa siku mtakaposikia Kafulila ameichoka tena CCM na anahamia ACT na akitoa hoja kuwa "CCM imeshindwa kuongoza nchi!"

Msichanganywe na hali ya sasa ili msije kupumbazwa na hali ya baadaye. Nawasisitiza, waheshimuni wahamao, Songeni UGALI wenu na laleni usingizi, hakika kesho kutakucha na hali ya uchumi wa nchi itaendelea kudidimia, pambaneni na hali zenu, waacheni wahamao nao wapambane na hali zao.

Mtatiro J
 
Huy utamsubiri sana hahami maana kishaanzisha chama chake kinaitwa CUF Facebook Club na ana wanachama wengi sana. Sijajua kama atamkaribisha Maalim Seif katika chama chake kipya cha Facebook
 
Vijana wanahitajika kwa JPM kujenga nchi, ajitambue mapema! Na kwa hiyo post yake, siku chache zimebaki.
 
tatizo ni kwamba wanasiasa wanawekeza katika siasa za kutafuta masilahi badala ya kusimamia ukweli. Moyoni wanawaka tamaa za uteuzi na kutukuzwa mdomoni wanahubiri ukombozi! nadhani tuache kila mtu atimize ndoto za moyo wake. Jukumu letu ni kuwa na msimamo juu ya tunachokiamini bila kujali kinahubiriwa na nani!
 
Hata kama naye akienda inasaidia nini kwa chama cha mapinduzi kama hawa wapiga kura wanaenda upinzani?
a3d88825414e64aa1ac2855aecb25875.jpg
Hii picha ni ya mwaka 2015 iliyokiweka chadema madarakani. Umeacha kitu hapo kulikua pia na udekaji wa barabara
 
unaishi kwa kukariri,jibu ulilipata kiilichotokea!

Hii picha ni ya mwaka 2015 iliyokiweka chadema madarakani. Umeacha kitu hapo kulikua pia na udekaji wa barabara
Sasa nani hajui kuwa hata nyinyi mnajua kuwa uchaguzi ulikuwa wa aina gani? Ni kuwa mshindi ni yule aliyemtaka mwenyekiti wa tume
 
Mshindi ni yule alietangazwa na mwenyekiti wa tume kama uhuru kenyatta tu!
 
Sasa nani hajui kuwa hata nyinyi mnajua kuwa uchaguzi ulikuwa wa aina gani? Ni kuwa mshindi ni yule aliyemtaka mwenyekiti wa tume
Mbona umeshajibu hoja yangu? Tatizo kubwa unajitoa ufahamu ukidhani kujaza watu ktk mikutano ndiyo kushinda uchaguzi. Umesahau 2015 watu karibu ya zaidi ya milio sita hawakupiga kura. Wenzenu ccm walikua wanawahamasisha waende wakapige kura ninyi mlikua mnajidanganya na mafuriko na vichinjio. Mwenzenu magu na ccm walipita vijijini kwa magari ninyi mlipitia angani. Wenzenu walitawanya mawakala kila kona ninyi mliishia kuitana wala mihogo kuja kustuka siku ya uchaguzi. Mwishoni kutoka kujigamba na vichinjio mkaanza kulia mmeibiwa.

Pamoja na kuwepo uwezekano wa kuibiwa kura lakini siamini kama mngeshinda kuunda serikali maana ccm waliwatangulia mbali sana.

Makada wenu kina Wolper wa kwenye Facebook badala ya kuhamasisha watu wakapige kura wakawa wanajigamba na makundi makubwa ya waty mikutanoni rais na mbunge hachuguliwi kwa wingi wa mikusanyiko bali kwa kura.

Niligombana na wadogi zangu wengine walinitenga kwa kuwaambia ukweli nilipomlinganisha Mrema na Lowasa. Wakasema ule ulikua mwaka 1995 mwaka huu vijana wamebadilika. Lakini wamesahau sisivpia tulikua vijana mwaka 1995 na hakuna miaka serikali ilikua na ugomvi na wanavyuo kama miaka ya tisini ni mwaka huo ambaoo mr PUNCH kwa mara ya kwanza ali graduate.

Swali kwako kama unaamini 2015 uliibiwa kura na 2010 kipi kinakupatia imani kwamba hutaibiwa 2020?

Ni wapumbafu peke yao wanaweza kuamini kwamba ukawa waliibiwa kura.
 
Pamoja na watu wengi kutokupiga kura, wewe binafsi unaamini uchaguzi ulikuwa huru na haki? Kwamba vyombo vya dola havikuhujumu uchaguzi? Na kuwa Returning officers walitenda kazi yao kwa uaminifu? Kama unaamini hivyo basi acha nikuache tuu. Ni haki yako
 
Julius S. Mtatiro
11 hrs ·
USHAURI WA BURE.

Msiwatukane wanaohama kwenye chama chenu ili siku wakirudi msianze kazi ya kusameheana matusi yenu na ama kununiana.

Kafulila alikulia ndani ya CHADEMA, baadaye akahamia NCCR MAGEUZI, kisha akarejea tena CHADEMA na hivi sasa amehamia CCM (amehama vyama mara 4).

Na mfano mwingine ni mwalimu wangu Prof. Kitila, amekulia ndani ya CCM (sina hakika kama aliwahi kuwa NCCR) lakini tunajua alihamia CHADEMA, akatoka CHADEMA akaanzisha ACT, na sasa ameiacha ACT amekwenda CCM.

Huo ni ushahidi thabiti kuwa wapo wanasiasa safari zao kisiasa huwa ziko namna hiyo, huhangaika sana lakini kibinadamu lazima tuwaheshimu kwa dhati. Hata binadamu anapokuwa anafariki yupo ambaye hufa kwa utulivu na yupo ambaye hufa kwa kuhangaika sana.

Msishangae kuwa baada ya mwaka mmoja au miwili Kafulila akarudi CHADEMA, Masha akaenda ACT, Patrobas akaenda CUF na Kitila akaanzisha chama kipya.

Kama mnachanganywa na hali hii ya sasa inaonekana mtakuwa wendawazimu kabisa siku mtakaposikia Kafulila ameichoka tena CCM na anahamia ACT na akitoa hoja kuwa "CCM imeshindwa kuongoza nchi!"

Msichanganywe na hali ya sasa ili msije kupumbazwa na hali ya baadaye. Nawasisitiza, waheshimuni wahamao, Songeni UGALI wenu na laleni usingizi, hakika kesho kutakucha na hali ya uchumi wa nchi itaendelea kudidimia, pambaneni na hali zenu, waacheni wahamao nao wapambane na hali zao.

Mtatiro J
Msiahangazwe na kesho...!
 
Back
Top Bottom